Sunday, March 17, 2013

JUMAPILI YA LEO TUSALI SALA HII:- SALA YA MUME NA MKE PAMOJA....

Ee Bwana, tuko sote wawili
Tumepiga magoti mbele yako,
Mara nyingi kila mmoja huongea nawe peke yake,
Lakini sasa tumekuja pamoja, kama mume na mke.
Tunataka kukushukuru, Bwana,
Kwani umekuwa mwema kwetu. Umetupatia zawadi na baraka nyingi sana-
Tangu baraka ile ya kwanza siku ile ya ndoa yetu.

Maisha hayakuwa matamu siku zote, wewe wajua
Kumekuwepo magonjwa na matatizo, magumu na kuto elewana kati yetu. Lakini umetusaidia.
na kuyashinda hayo yote.

Kwa njia ya kila mmoja wetu, umetupatia moyo mkuu, nguvu, faraja na furaha. kwa ajili ya raha hiyi yote, Bwana Tunasema, AHSANTE.

Na tukiangalia sasa siku za usoni, tunaomba msaada wako.
Utuwezeshe kukua katika upendo wako, na katika upendano kati yetu.
Utusaidie ili tuelewane na kupokeaana zaidi na zaidi-

Utufanye tuyajali mahitaji ya kila mmoja wetu,
Na tuwe tayari kutafuta njia mpya za kupendezana.

Na tunakuomba, Ee Bwana,
Uwe nasi, hapa nyumbani petu,
Na utujalie tuwezekukaa nawe Daima.
NAWATAKIENI WOTE DOMINIKA YA 5 YA KWARESIMA C..Na watakatifu wa juma lijalo ni
Jt. Siril wa yerusalem
Jn Yosefu, Baba mlishi
Jo Gisbert, Irmgard
Al Serapion
Ij Lea, Deograsias
Js Turibio, Rebeka
DOMINIKA IJAYO NI DOMIKA YA MATAWI C

6 comments:

Shalom said...

Jamani ss mabachela hatuna sala yetu dada!

Yasinta Ngonyani said...

Shalom..Usikonde ndugu yangu..ipo na itakuja siku nitaiweka..Jumapili njema sana kwako...

Shalom said...

Haya naingojea iyo siku kwa hamu kubwa kwani nitaomba kwa imani kubwa sana nawe pia jpili njema kwako na familia yako mungu awabariki sana.

Anonymous said...

Ameen! By Salumu

Yasinta Ngonyani said...

Shalom..we subiri utaona:-)

Salumu, Amina na jumapili njema sana

steven bulamu said...

Daa hayo yote ni mafanikio ya maisha yetu Mungu ndio kila kitu