Thursday, March 14, 2013

TUSISAHAU HADITHI ZETU TULIZOSIMULIWA PIA TULIZOSOMA:- LEO...MWANAMKE MWIZI!!!

Palikuwa na kijana moja aliyekuwa analala kwenye bwaru, hakuwa na mke. Siku moja aliondoka kwenda kutafuta mwanamke. Alifika katika mji wa watu, na katika mji ule palikuwepo wasichana watatu. Msichana moja mchawi, msichana mwingine mwongo na msichana mwingine mwizi. Basi, yule kijana akafikiri afadhali aoea nayeiba. Aliogopa mwanamke mchawi ataenda kumwua. Kadhalika, alifikiri Moyoni mwake: Kama nikioa mwanamke mwongo kutakuwa na mashauri kila siku. Akasema , afadhali nioe ayeiba nitaweza kumlimia.

Kweli akaoa mwanamke anayeiba, akaja naye nyumbani kwake. Akakaa naye. Siku moja mwanamume yule akachinja mbuzi, akakatakata maini na utumbo akampa mkewe apike. Basi, mwanamke yule akachukua ulezi akaanza kusaga kwenye jiwe. Mwanamume akaondoka akaenda kuoga maji mtoni. Mwanamke yule akaacha kusaga, akaingia nyumbani mwake pale alipokuwa amepika kitoweo, akachukua mwiko akaipua finyango moja akatoka nacho akazunguka nyuma ya nyumba akaanza kula. Mume wake alipotoka mtoni, baada ya kuona mke wake hayupo, naye akachukua finyango moja akazunguka upande wa pili akaanza kula. Mke wake alipomwona akasema :- Wa kukasirika hayupo , sote tunaiba.
MUWE NA  SIKU NJEMA SANA WOTE MTAKAOPITA HAPA. HADITHI NYINGINE ITAKUJA WIKI IJAYO PANAPO MAJALIWA....

6 comments:

Rafikio wa hiari said...

Hahhahah ina maana rafiki hawa wandugu wote wanaasili ya wizi? Na je hii inamaanisha kwamba watu wa tabia moja ndio wanashabihiana?

Shalom said...

Khekhehee wote majizi hao dada lkn kuna mafundisho hapo nimekupata vema

Yasinta Ngonyani said...

Rafiki yangu!..inawezekana ni hivyo na pia inawezekana sivyo..lakini mimi naona si kweli kwa kweli ila kwao ilitokea tu...labda tusibiri labda twaweza kupata jibu...

Shalom! Ndiyo wote majizi kwa hiyo wote wakiiba kazi twende tu ..nafurahi kama umegundua kuna fundisho...

Cathbert Kajuna said...

Fundisho

penina Simon said...

Thanks the nice one, hujambo bibie? nakutakia weekend njema.

ray njau said...

Hadithi ni nguzo muhimu katika utamaduni ndani ya tasnia ya fasihi simulizi.