Monday, March 11, 2013

KAZI YA MIKONO YANGU:- MLO WA JIONI YA LEO LASAGNE...

 Hapa ni maandalizi :- kwanza ni aina ya mchuzi mweupe ambao nimetengeneza kwa unga wa ngano,maziwa,chumvi pilipili manga na baadaye chizi..halafu unaweka kwenye hicho chumbo kwanza mchuzi huo mweupe, halafu aina ya pasta bapa kidogo na halafu nyama ya kusaga iliyokaangwa na kuungwa na nyanya ya kusaga,kitunguu na kitunguu saumu..unafanya hivyo mara tatu au nne....
 Baada ya hapo naweka ndani ya oven 200°, dakika 30 baada ya hapo tayari kwa kuliwa

Na hapa unaona jinsi sahani ya Kapulya ilikuwa pembeni kuna spenchi, nyanya,na aina ya tango kinywaji machi ambayo yana limao kwa mbali...Chakula hili ni maalum zaidi Italia..Samahani kwa wala waiokula nyama msiogope kuja huwa kuna chakula aina nyingine kwa akiba..kama vile Kamala na Chacha ndio ninaowajua ambao hawali nyama.....JIONI YENU IWE NJEMA NA YENYE AMANI...TWIWONAGE CHILAWO BE..SIJUI NIMEPETIA...:-)

7 comments:

Anonymous said...

Yasinta, sasa naona unataka nihamie kwako kabisaaa! Mana vyakula unavyopika mbona vitaliponza tumbo langu. Hongera sana kwa chakula ambacho kwa macho kinaonekana ni kitamu sana. Ila kuna siku ntakuja ghafla kwako, endelea kutupikia nasi twala kwa macho tu. Jioni njema.

Yasinta Ngonyani said...

Hahahahahaa, Una jina ila hapa inaonekana huna jina. Umenichekesha kweli yaani hamna shida we karibu sana kuhamia hapa kwetu...Ni kweli kinainekana ni kitamu kwa macho na kitamu sana kwa kula pia. Ahsante sana kwa kuyapenda mapishi yangu:-)

Rafikio wa hiari said...

Rafiki yangu Kapulya hakika hiki chakula kwa macho tu kinaonyesha tu ni kitamu sana. Hongera kwa E & C kuwa na Mama bora anaejali familia yake. Pia sengwile kwa maelezo ila mi nitahitaji maelekezo zaidi ili niweze kujaribisha kupika weekend moja.
Kazi njema!

Mija Shija Sayi said...

Restaurant utaipa jina gani Yasinta..?

Interestedtips said...

chakula chaonekana kitamu sana kwakweli

ray njau said...

Mke mwenye uwezo, ni nani anayeweza kumpata? Thamani yake inapita sana ile ya marijani.Moyo wa mume wake umemtegemea, wala hakuna faida inayokosekana.Amemthawabisha mume wake kwa mema, wala si kwa mabaya, siku zote za maisha yake.Ametafuta sufu na kitani, naye hufanya kazi yoyote inayopendeza mikono yake.Amekuwa kama meli za mfanyabiashara. Huleta chakula chake kutoka mbali.Tena huamka kabla usiku haujaisha, na kuwapa watu wa nyumbani mwake chakula na kuwapa vijana wake wa kike fungu lao lililoamriwa.Amefikiria shamba, akalinunua; amepanda shamba la mizabibu kutokana na matunda ya mikono yake.Amejifunga nguvu viunoni, naye ameitia nguvu mikono yake.Ametambua kwamba biashara yake ni nzuri; taa yake haizimiki usiku.יAmenyoosha mikono yake kushika kijiti cha kusokotea uzi, nayo mikono yake mwenyeweimeshika gurudumu la kusokota nyuzi.Amewanyooshea mkono wenye kuteseka, na mikono yake amemkunjulia maskini.Hana wasiwasi juu ya watu wa nyumbani mwake kwa sababu ya theluji, kwa maana watu wote wa nyumbani mwake wamevaa mavazi mawili.Amejitengenezea matandiko yenye mapambo. Mavazi yake ni ya kitani na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau.Mume wake ni mtu anayejulikana malangoni, anapoketi pamoja na wanaume wazee wa nchi.Hata ametengeneza mavazi ya ndani na kuyauza, nao wafanya-biashara amewapa mishipi.Nguvu na fahari ndiyo mavazi yake, naye anaucheka wakati ujao.Hufungua kinywa chake kwa hekima, na sheria ya fadhili zenye upendo ziko katika ulimi wake.Anaangalia shughuli za nyumba yake, wala hali mkate wa uvivu.Wanawe wamesimama na kumtangaza kuwa mwenye furaha, mume wake husimama, naye humsifu.Kuna binti wengi ambao wameonyesha uwezo, lakini wewe—wewe umewapita hao wote.Uvutio unaweza kudanganya, nayo sura yenye kupendeza inaweza kuwa ubatili; lakini mwanamke anayemwogopa Yehova ndiye anayejiletea sifa.Mpeni baadhi ya matunda ya mikono yake, nazo kazi zake na zimsifu malangoni._Methali 31:10-31

Yasinta Ngonyani said...

Rafiki yangu wa hiari...najaribu kujipikilisha. Chakula kilikuwa kitamu si mchezo ukija nitakupikia..
Mija hahahaaaa jina la restaurant? jina ..sijafikiria huko kwanza njoo uonje chakula chenyewe:-)

Ester! kilikuwa kitamu sana ..siku tukionana ntakupikie
Kaka Ray nimelikubali kubali neno..ubarikiwa sana.