Wednesday, March 27, 2013

MVUA JIJINI DAR ZAZUA MAFURIKO.....PICHA JUMAPILI 24/3

 Hapa hata kutoka nje tu huwezi labda kuwe na mtumbwi ila maji yameingia hadi ndani....
Hapa picha zote mbioli ni Tandale kwa Mtogole. Picha nimetumiwa na mdogo wangu ...

8 comments:

Interestedtips said...

Yani dada huku tunakoma kwakweli, ikinyesha tu ni maji kujaa mno

Anonymous said...

Yasinta, hayo ndio maisha yetu ya Tz. Miundo mbinu bado, na ujenzi holela vyote vinachangia! Mungu aiponye Tz.

emuthree said...

Mvua ni baraka, lkn kwa Dar, inageuka kuwa maafa. Ni tatizo la miundo mbinu.

ray njau said...

Hili tatizo la wakati huu limetokana na ujenzi unaoendelea katika barabara ya Morogoro.Ukitaka maendeleo hizi ndizo gharama zake.Pole sana ndugu zetu kwa madhara haya.Mungu awape nguvu na faraja ili muweze kundelea na mchakato wa maisha na mafanikio baada ya mikikimikiki ya mvua za wikiendi.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Da Yacinta huna haja ya kushangaa. Hayo ndiyo maisha bora kwa wote. Ni ajabu kuwa wetu na serikali yetu wanashabikia kufanya vitu vya hatari namna hii. Hivi ni kwanini serikali haiwahamishi kwa nguvu au ni kuogopa CCM itakapowahitaji wakati wa uchaguzi watapunguza kura zake?
Kusema ukweli wakati mwingine nawalaumu wananchi wenyewe kwa kuendekeza serikali ya hovyo kama hii.

Anonymous said...

Kaka Ray Njau, sudhani kama imesababishwa na ujenzi unaoendela morogor road! Kwani mvua zikinyesha miaka yote hali ndio hiyo hiyo! Tatizo ni miundo mbinu na ujenzi holela. Mungu aiponye Tanzania.

ray njau said...

Hili tatizo la wakati huu limetokana na ujenzi unaoendelea katika barabara ya Morogoro

Yasinta Ngonyani said...

Nina swali kidogo hapa ujenzi wa barabara ya Morogoro na mafuriko haya yanaingiana vipi?