Thursday, March 28, 2013

SWALI NILILOULIZWA NA NIKASHINDWA KUJIBU....

Leo nimeulizwa swali hili ..ilianza  hivi:- Kuna swali linanisumbua katika kichwa changu ngoja niulize ili tusaidiane...haha hivyo nikashindwa lakini nikakukumba kwenye wengi hakiharibiki kitu. Na swali lenyewe likawa kama ifuatavyo:- Laiti jana ingekuwa kesho, leo ingekuwa Ijumaa. Je? mwalimu aliyasema haya siku gani?

6 comments:

Cathbert Kajuna said...

Pole sana... hili swali ukilijadili sana kichwani mwako utaumia. Jibu ni Alhamis

Amina mzava said...

Alhamisi

ray njau said...

Inasikika kama Alhamisi?Wadau wengine sijui naona tupo pamoja au wana jipya?Acha tuone!!

Yasinta Ngonyani said...

Cathbert, Amina na Ray ...asanteni sana kwa kupita hapa na kuacha yenu yaliyo moyoni...pamoja daina....

Simba Deo said...

Ni siku yoyote, kwani hata hilo dokezo la siku ya Ijumaa limekaa kidhahania ...inge ... lakini siyo lazima iwe Ijumaa. Kwa hiyo. Unaweza kutumia swali hili kuhusu siku yoyote katika juma. Alhamisi ni moja wapo. Maana kinachotafutwa hapo ni siku aliyosema mwalimu.

Credo Paul said...

Sikh ya jumaili