Monday, March 18, 2013

MSONGAMANO WA MAGARI/FOLENI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM!!!

Nimekuwa nikijiuliza muda mrefu sasa kuhusu foleni katika Jiji letu la Dar es salaam. Nianze hivi hivi kwanini watu wanaishi nyumba moja na kila mtu anakuwa na gari lake? Kwanini wasitumie gari moja?
Kwanini tusiwekeane zamu kutumia gari moja kwa wiki na hata mwezi..kwa mfano mfanyakazi mwenzako au jirani..hii ingepunguza sana gharama za mafuta pia foleni zingepungua kwa kiasi fulani. Haya ni mawazo yangu..karibuni sana tujadili kwa pamoja...Kapulya

6 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Tatizo la msongamano wa mikweche jijini Dar na miji mingine ni matokeo ya uongozi mbovu usio na visheni. Kama rais alifikia kusema kuwa msongamano ni dalili za maisha bora unategemea nini? Angalia wenzetu Nairobi walivyojikwamua kwa kujenga Thika Super Hwy. Sisi uchumi tunao lakini tumeukalia so to speak. Sidhani kama utawala mchovu na mbovu kama wa sasa unaliona hili inavyotakiwa.

Salehe Msanda said...

Habari.
Kuhusu kila msongamano wa magari na ulichosema cha kutumia gari moja katika familia au na jirani.
Du! Wabongo ubinafsi umetutawala na kushika kasi lakini pia tunaponzwa na kudhani kuwa thamani ya binaadamu ni vitu anavyomiliki hata kama uhitaji wa vitu husika si muhimu sana kwa maisha ya kawaida.
Kwa wabongo tuliowengi tunaongozwa na kudhani kuwa malengo yetu makuu kama binaadmu ni kuwa na nyumba na kuwa na gari na si vinginevyo.
Tusubirie ujio wa mabasi ya mwendo kasi labda Serikali itakuja na mpango wa kuhakikisha kuwa magari madogo hayaingii sehemu za mjini bila sababu maalum maana suala la msongamano wa magari linaathiri uchumi na pata la mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Kila la kheri na kazi njema.

ray njau said...

Uboreshaji wa miundombinu ya barabara za pembezoni mwa jiji la Dar es salaam siyo wa kiwango cha kuridhisha na matokeo yake ni magari yote kuingia kwenye barabara za kiwango cha lami ambazo kwa sasa zimeendelea kulemewa na idadi kubwa ya magari kutokana na ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi.Msongamano wa huduma za kijamii na shughuli za kiuchumi katika maeneo ya katika ya jiji na ofisi nyingi kuanza na kufunga kazi kwa wakati mmoja unatajwa kuwa chanzo kingine cha misongamano ya magari.Usafiri wa umma usio na utaratibu wa umakini katika viwango vya kimataifa unawafanya wakazi wa jiji la Dar es salaam kuwekeza katika usafiri binafsi ili kuweza kukidhi malengo na matarajio yao katika ratiba ya shughuli za kila siku.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka zangni..nipo pamoja nanyi na hili tatizo ni kubwa mno ambalo nchi yenyewqe sijui kama inaona ni tatizo..kwa vile kama viongzi wanasafiri basi wao hawasimami kwenye foleni kwa hiyo hawajui wananchi wanapata shida gani na inakuwa ngumu kwa wao kulifanyia kazi...kazi sana sana..tufunguke, hivi kwa nini hatufunguki kwa kila kitu tupo nyuma?????

ray njau said...

Yasinta;
Hakika sauti yako imesikika!!

Anonymous said...

Brandon laser treatment rosacea

my web-site - rosacea laser treatment North Freedom