Friday, March 8, 2013

WIKI HII NI YA WANAWAKE DUNIANI NA HAPA NI HII TAREHE NANE NDO YENYEWE...NAMI NIMEONA TUISHEREKEE KIHIVI:- BILA WANAWAKE ULIMWENGU UNGESIMAMA

MAMA ANALIMA 

Bila wanawake ulimwengu huu utasimama, yaani hakuna kitu kingeenda/fanikiwa..Ukiangalia kila mahali wanawake wapo, hasa katika shughuli kama kuchota maji, kutafuta kuni, kulea watoto na hata kazi ya kulima mazao /bustani(mbogamboga ...pia hata kazi ya kutafuta madini ghafi na kazi ngingine ngingi, nying zaidi. Anatumia masaa mengi kufanya shughuli hizi. Mara nyingi inakuwa siku nyingi kuliko mwanaume afanyavyo kazi. Na hii ndiyo sababu kubwa hasa ya kupigania USAWA ulimwenguni kote.
Tuzidi kuupigania USAWA sehemu zote :- Majumbani, mashuleni, makazini, kwa watu walio jirani yetu, kwenye siasa na kiutamaduni- ULIMWENGUNI kwote. WANAWAKE OYEEEEEEEEEE..NA KUMBUKENI WANAWAKE TUNAWEZA... Lakini pia tusiwasahau akina baba kwani bila wao tusingekuwepo akina mama....IJUMAA NJEMA SANA.

12 comments:

emu-three said...

Poleni sana akina mama wa kijijini, ambao hamtambulikani, ...poleni sana akina mama wa kijijini ikifikia wakati wa uchaguzi ndio mnaonekana watu. Atakayewalipa ni mungu pekeee, kwani sasa wanasiasa wataanza kuwajia, na kuwahadaa kwa mikopo nk, na wenzenu wa mjini wanawatumia kama ngazi ya kuwanufainsha wao,....Mungu yupo ...atawalipa

Emmanuel Mhagama said...

Nami nichukue nafasi huu kuwapongeza wanawake wote kwa ajili ya maadhimisho haya. Nikikumbuka kwamba Mama yangu ni mwanamke, dada zangu ni wanawake na mke wangu mpenzi pia ni mwananmke, ninakuwa na kila sababu ya kuungana na ulimwengu mzima katika kuwapongeza wanawake wote katika maadhimisho jaya ya siku ya mwanamke. Neno langu kwenu wanawake ni hili: Wanaume wanaweza kusema yote wanayotaka kusema juu yenu, ikiwa ni pamoja na kuwabeza na kuwadharau. Lakini ukweli unabaki pale pale kwamba Mungu aliyewaumba hakuwaumba kwa makosa. ALIWAUMBA KWA MALENGO na hayo malengo mnaweza kuyatimiza sawa sawa na Mungu alivyokusudia muyatimize. Swala la msingi ni kujua ni nini mlikuja kukifanya hapa dunia, mkishakujua kitekelezeni hicho. Mkiamua kufanya mnaweza, tena mnaweza sana. Maandiko Matakatifu wanawataja kama JESHI KUBWA pale mnapoamua kufanya jambo kwani hakuna wa kuwazuia.

HONGERENI WANAWAKE WOTE DUNIANI KWA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE.

Msisahau kuomba sana ISIANZISHWE KAMWE siku ya wanaume duniani kwani hali yenu ya mwisho itakuwa mbaya kuliko ile ya mwanzo. Ha ha ha ha ha

Anonymous said...

Kina mama Oyeee!
Mwanamnke wa kijijini anahitaji ukombozi wa hali ya juu, kama emu three alivyoandika. Mataifa yaliyoendelea kama Sweden wamejitahidi sana kuwapa kina mama usawa na kina baba, kwani hapa hawana maternity leave bali ni paternal leave ikimaanisha máma na baba wanatakiwa kusaidian kumlea mtoto anapozaliwa..wana utaratibu mzuri mno! Ila kwetu ni maternity leave shughuli ya mtoto yoote ni ya mama, baba akipenda kusaidia. Kwa kweli wakina mama wa Africa, na hasa kwa nchi yetu Tanzania tunahitaji ukombozi. Kweli hakuna kama mama.

ray njau said...

Je, wanawake wamelaaniwa na Mungu?
----------------------------------
Hapana. Badala yake “yule nyoka wa zamani, yeye anayeitwa Ibilisi,” ndiye ‘aliyelaaniwa’ na Mungu. (Ufunuo 12:9; Mwanzo 3:14) Mungu aliposema kwamba Adamu ‘angemtawala’ mke wake, Mungu hakuwa akimruhusu mwanamume amkandamize mwanamke. (Mwanzo 3:16) Alikuwa tu akitabiri matokeo mabaya ya dhambi ambayo yangewapata wenzi wawili wa kwanza.
Hivyo, kutendwa vibaya kwa wanawake ni matokeo ya moja kwa moja ya dhambi ambayo wanadamu walirithi, bali si mapenzi ya Mungu. Biblia haiungi mkono wazo la kwamba ni lazima wanaume wawakandamize wanawake ili kulipia ile dhambi ya kwanza.—Waroma 5:12.
-----------------------------------
▪ Je, Mungu alimuumba mwanamke
akiwa duni kuliko mwanamume?
----------------------------------
Hapana. Andiko la Mwanzo 1:27 linasema: “Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimuumba; mwanamume na mwanamke aliwaumba.” Hivyo, tangu mwanzoni, wanadamu wote—wanaume na wanawake—waliumbwa wakiwa na uwezo wa kuonyesha sifa za Mungu. Ingawa Adamu na Hawa waliumbwa kwa njia iliyotofautiana kihisia na kimwili, wote walipokea mgawo uleule na walifurahia mapendeleo yaleyale kutoka kwa Muumba wao.—Mwanzo 1:28-31.
Kabla ya kumuumba Hawa, Mungu alisema hivi: “Nitamfanyia [Adamu] msaidizi, awe kikamilisho chake.” (Mwanzo 2:18) Je, neno “kikamilisho” linamaanisha kwamba mwanamke alikuwa duni kuliko mwanaume? Hapana, kwa sababu neno hilo la Kiebrania linaweza pia kutafsiriwa kuwa “mshirika” au “msaada unaolingana na” mwanamume. Fikiria majukumu ya daktari mpasuaji na ya mtaalamu wa dawa za kupunguza maumivu wakati wa upasuaji. Je, mmoja anaweza kufanya kazi bila mwenzake? Huenda asiweze! Ingawa daktari mpasuaji ndiye hufanya upasuaji, je, yeye ni wa maana zaidi? Hatuwezi kusema hivyo. Vivyo hivyo, Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke ili washirikiane kwa ukaribu, bali si kushindana.—Mwanzo 2:24.
----------------------------------
▪ Ni nini kinachoonyesha kwamba Mungu anawajali wanawake?
------------------------------------
Huku akijua kimbele jinsi ambavyo wanaume wasio wakamilifu wangetenda, tangu zamani Mungu alionyesha kwamba alikusudia kuwalinda wanawake. Akizungumza kuhusu Sheria ya Musa ambayo ilianza kutumika katika karne ya 16 K.W.K., katika kitabu chake La Bible au féminin (Biblia Katika Jinsia ya Kike) mwandishi Laure Aynard, aliandika hivi: “Mara nyingi, agano la Sheria linawatetea wanawake linapozungumza kuwahusu.”
Kwa mfano, Sheria iliagiza Waisraeli wamheshimu baba na pia mama. (Kutoka 20:12; 21:15, 17) Vilevile, Sheria iliagiza kwamba mwanamke mwenye mimba atendewe kwa ufikirio. (Kutoka 21:22) Hata leo, ulinzi uliotolewa na sheria hizo za Mungu ni kinyume kabisa na ukosefu wa haki za kisheria ambao wanawake wengi wanakabiliana nao katika sehemu nyingi ulimwenguni. Lakini kuna mambo mengine yanayoonyesha kwamba Mungu anawajali.

Yasinta Ngonyani said...

Hakuna kama mama...wanawake mungu awabariki..Si bora, lakini karibu sawa. Sio lazima wanawake wawe bora zaidi, lakini ni tofauti. Ni hasara kubwa kwa jamii kwa kutochukua uzoefu wa wanawake pia maarifa yao.

mumyhery said...

Shukran

ray njau said...

Wanawake Wana Mapendeleo Mazuri
-----------------------------------
Chini ya Sheria ambayo Mungu aliwapa Waisraeli, wanawake walikuwa na mapendeleo yao nao walikuwa huru kutumia vipawa vyao. Kwa mfano, andiko la Methali 31:10-31 linazungumza kuhusu “mke mwenye uwezo,” ambaye ananunua vitambaa vizuri na kuwashonea watu wa nyumbani mwake mavazi bora. Hata, “ametengeneza mavazi ya ndani na kuyauza”! (Mstari wa 13, 21-24) “Kama meli za mfanyabiashara,” mwanamke huyo bora anatafuta chakula kizuri, hata ikiwa itamlazimu kwenda kuleta chakula hicho kutoka mbali. (Mstari wa 14) “Amefikiria shamba, akalinunua,” naye “amepanda shamba la mizabibu.” (Mstari wa 16) Kwa kuwa “biashara yake ni nzuri,” shughuli zake zinamletea faida. (Mstari wa 18) Zaidi ya ‘kuangalia shughuli za nyumba yake,’ mwanamke huyo mwenye bidii na anayemwogopa Yehova anawasaidia wengine bila uchoyo. (Mstari wa 20, 27) Haishangazi kwamba anasifiwa!—Mstari wa 31.
Sheria ambazo Yehova alitoa kupitia Musa ziliwapa wanawake nafasi nzuri ya kukua kiroho. Kwa mfano, katika Yoshua 8:35, tunasoma hivi: “Hakuna neno lolote kati ya yote ambayo Musa alikuwa ameamuru ambalo Yoshua hakusoma kwa sauti mbele ya kutaniko lote la Israeli, pamoja na wanawake na watoto wadogo na wakaaji wageni waliokuwa katikati yao.” Kumhusu kuhani Ezra, Biblia inasema hivi: “Akaleta sheria mbele ya kutaniko la wanaume na la wanawake na vilevile la wote wenye akili ya kutosha kuweza kusikiliza, katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba. Naye akaendelea kusoma ndani ya kile kitabu kwa sauti mbele ya kiwanja cha watu wote kilichoko mbele ya Lango la Maji, kuanzia mapambazuko mpaka katikati ya mchana, mbele ya wanaume na wanawake na mbele ya wale wengine wenye akili; na watu wote wakasikiliza kwa makini kitabu cha sheria.” (Nehemia 8:2, 3) Wanawake walifaidika na usomaji huo wa Sheria. Pia, walishiriki sherehe za kidini. (Kumbukumbu la Torati 12:12, 18; 16:11, 14) La muhimu zaidi ni kwamba, kila mwanamke katika Israeli la kale angeweza kuwa na uhusiano wa kibinafsi pamoja na Yehova Mungu na kusali kwake.—1 Samweli 1:10.

ray njau said...

Katika karne ya kwanza W.K., wanawake waliomwogopa Mungu walikuwa na pendeleo la kumhudumia Yesu. (Luka 8:1-3) Mwanamke fulani alimtia Yesu mafuta kichwani na miguuni wakati wa chakula cha jioni huko Bethania. (Mathayo 26:6-13; Yohana 12:1-7) Wanawake walikuwa kati ya wale ambao Yesu aliwatokea baada ya kufufuliwa kwake. (Mathayo 28:1-10; Yohana 20:1-18) Baada ya Yesu kupanda mbinguni, kikundi cha wanafunzi 120 hivi ambacho kilikutana pamoja kilitia ndani “wanawake fulani na Maria mama ya Yesu.” (Matendo 1:3-15) Bila shaka, wengi wa wanawake hao au labda wote walikuwa katika chumba cha juu huko Yerusalemu siku ya Pentekoste 33 W.K. Siku hiyo, roho takatifu ilimiminwa juu ya wanafunzi hao wa Yesu nao wakaongea kimuujiza katika lugha mbalimbali.—Matendo 2:1-12.
Wanaume na wanawake walikuwa kati ya wale ambao unabii wa Yoeli 2:28, 29 ulitimizwa kuhusiana nao. Mtume Petro alitaja unabii huo siku ya Pentekoste: “[Mimi Yehova] nitaimimina sehemu ya roho yangu juu ya kila namna ya mwili, nao wana wenu na binti zenu watatoa unabii . . . Na hata juu ya watumwa wangu na juu ya wajakazi wangu nitaimimina sehemu ya roho yangu katika siku hizo.” (Matendo 2:13-18) Kwa muda fulani baada ya Pentekoste 33 W.K., wanawake Wakristo walipewa zawadi za roho. Waliongea na kutabiri katika lugha za kigeni. Huenda hawakutabiri mambo mapya, lakini walitangaza kweli za Kimaandiko.
Katika barua ambayo aliwaandikia Wakristo huko Roma, mtume Paulo anamsifu “Fibi dada yetu,” akimpendekeza kwao. Pia, anamtaja Trifaina na Trifosa, akiwaita “wanawake wanaofanya kazi kwa bidii katika Bwana.” (Waroma 16:1, 2, 12) Ingawa wanawake hao hawakuwekwa rasmi kuwa wazee au watumishi wa huduma katika kutaniko la Kikristo la mapema, wanawake hao na wengine wengi walikuwa na pendeleo la kuchaguliwa na Mungu ili washiriki pamoja na Mwana wake, Yesu Kristo, katika Ufalme wa mbinguni.—Waroma 8:16, 17; Wagalatia 3:28, 29.
Wanawake wanaomwogopa Mungu wana pendeleo kubwa sana leo! “Yehova mwenyewe anasema neno hili; wanawake wanaotangaza habari njema ni jeshi kubwa,” inasema Zaburi 68:11. Wanawake hao wanapaswa kupongezwa. Kwa mfano, ustadi wao wa kufundisha watu Biblia unawaongoza wengi wakubali mafundisho ya kweli yanayompendeza Mungu. Wanawake Wakristo walioolewa ambao wanawasaidia watoto wao kuwa waamini na ambao wanawaunga mkono waume zao walio na madaraka mengi kutanikoni wanastahili kusifiwa pia. (Methali 31:10-12, 28) Wanawake waseja pia wana sehemu yenye kuheshimika katika mpango wa Mungu, na wanaume Wakristo wanahimizwa ‘wawasihi wanawake wazee kama mama, wanawake vijana kama dada kwa usafi wote wa kiadili.’—1 Timotheo 5:1, 2.

Ester Ulaya said...

Katika wanawake nakukubali sana dada yangu............ujumbe mzuri na picha sambamba nzuri, bila wanawake Dunia ingegandaaaaaaaaaaa

Nicky Mwangoka said...

Nani kama mama

Rachel siwa Isaac said...

Asante sana "KADALA" Wanawake Juuuuuuuu!!

ray njau said...

KIELELEZO KWA WAKE
==========================
10 Familia ni kama shirika, na ili lifanye kazi vizuri, linahitaji kuwa na kichwa. Hata Yesu anajitiisha kwa Yule aliye Kichwa chake. “Kichwa cha Kristo ni Mungu” kama vile “kichwa cha mwanamke ni mwanamume.” (1 Wakorintho 11:3) Kujitiisha kwa Yesu chini ya ukichwa wa Mungu ni mfano mzuri kwa kuwa sote tuna kichwa ambaye tunapaswa kujitiisha kwake.
11 Wanaume wasio wakamilifu hufanya makosa na mara nyingi wao hupungukiwa katika jukumu lao la kuwa vichwa vya familia. Kwa hiyo, mke anapaswa kufanya nini? Hapaswi kudharau mambo ambayo mume wake anafanya au kujaribu kumnyang’anya ukichwa. Mke anapaswa kukumbuka kwamba roho ya utulivu na upole ina thamani kubwa machoni pa Mungu. (1 Petro 3:4) Akiwa na roho hiyo, itakuwa rahisi kwake kuonyesha utii wa kimungu hata katika hali ngumu. Isitoshe, Biblia inasema: “Mke anapaswa kumheshimu sana mume wake.” (Waefeso 5:33) Lakini vipi akikataa kujitiisha chini ya Kristo akiwa Kichwa chake? Biblia inawasihi wake hivi: “Jitiisheni kwa waume zenu wenyewe, ili, ikiwa wowote si watiifu kwa lile neno, wavutwe bila neno kupitia mwenendo wa wake zao, kwa sababu wamekwisha kushuhudia kwa macho mwenendo wenu ulio safi kiadili pamoja na heshima kubwa.”—1 Petro 3:1, 2.
12 Mume awe ni mwamini au la, mke hatakuwa akimvunjia heshima ikiwa ataeleza maoni yake kwa njia ya busara hata kama yanatofautiana na ya mume. Huenda maoni yake yakawa sawa, na yanaweza kufaidi familia nzima ikiwa mume atamsikiliza. Ingawa Abrahamu hakukubaliana na mke wake Sara alipopendekeza jinsi ya kutatua tatizo fulani la familia, Mungu alimwambia: “Sikiliza sauti yake.” (Mwanzo 21:9-12) Bila shaka, mume anapofanya uamuzi ambao haupingani na sheria ya Mungu, mke wake anapaswa kuonyesha anajitiisha kwake kwa kuunga mkono uamuzi huo.—Matendo 5:29; Waefeso 5:24.
13 Mke anaweza kutimiza jukumu lake kwa kutunza familia. Kwa mfano, Biblia inaonyesha kwamba wanawake ambao wameolewa wanapaswa ‘kuwapenda waume zao, kuwapenda watoto wao, kuwa na utimamu wa akili, safi kiadili, wafanyakazi nyumbani, wema, wakijitiisha kwa waume zao wenyewe.’ (Tito 2:4, 5) Mke ambaye pia ni mama anayefanya hivyo, atapendwa na kuheshimiwa daima na familia yake. (Methali 31:10, 28) Lakini kwa kuwa ndoa ni muungano wa watu wasio wakamilifu, huenda hali fulani wasizoweza kuvumilia zikawafanya watengane au kutalikiana. Biblia inaruhusu kutengana hali fulani zinapotokea. Hata hivyo, kutengana hakupaswi kuchukuliwa kivivi hivi tu, kwa kuwa Biblia inashauri: “Mke hapaswi kuondoka kwa mume wake; . . . na mume hapaswi kumwacha mke wake.” (1 Wakorintho 7:10, 11) Msingi pekee wa Kimaandiko wa talaka ni uasherati.—Mathayo 19:9.