Friday, August 30, 2013

IJUMAA YA LEO TUSIKILIZE ZILIPENDWA ...MAYASA

NAWATAKIENI WOYE MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA HILI. NA NAPENDA KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA WEMA WAKE KWA WATU WOTE. ....IJUMAA NJEMA SANA!!

Wednesday, August 28, 2013

PALE WAZAZI WANAPOWACHAGULIA WOTOTO/MABINTI ZAO WACHUMBA!!!

Habari za jioni ndugu zanguni....Hivi karibuni nimetumiwa email kutoka kwa msomaji wa maisha na mafanikio kutoka huko nyumbani Tanzania ikiwa na ujumbe huu na kuniomba kama naweza niuweka hapa kibarazani ...karibu tujadili kwa pamoja
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kuna mdada mmoja ambaye ni miongoni mwa watu wasomi sana. Amemaliza chuo hapa mlimani. Wakati alipokuwa chuoni alibahatika kupata mchumba ambaye walikubaliana kuoana. Na walikuwa katika maelewano mazuri katika uchumba waoi.

Baada ya uchumba huo kuendelea, aliamua kumpeleka kwa wazazi wake na kuwafahamusha kuwa mimi nimepata mtu ambaye naona atanifaa katika maisha yangu. Baada ya kuwafahamisha jambo hili, mama dada huyo alikubaliana na wazo lake la kutaka kuolewa na huyo mchumba wake lakini upande wa baba yake kulikuwa na shaka. Huyo binti alikuwa karibu sana na baba yake na aligundua kuwa baba yake hataki kukubaliana na wazo lake. Baada ya mazungumzo ya hapa na pale na baadaye mvulani yule kuondoka, binti alimfuata baba na kuzungumza naye na akasema kwa jinsi nilivyomwona huyo mvulana hakufai. Binti akamwambia si vizuri kumhukumu mtu kwa kumwangalia tu. Mimi nimekuwa naye muda mrefu namfahamu vizuri sina shaka naye. Baba yake bado hakukubalina na hilo lakini upande wa mama yake hakukuwa na shida.

Uchumba uliendelea na yule mvulana akasema inaonyesha baba yako hataki kabisha, lakini nitaumia sana endapo kama bado ataendelea na msimamo wake huo. Ni mtu ambaye nimekuzoea, tumeheshimiana sana. Yule binti akamwambia kila kitu kinawezekana na itawezekana tu.

Siku moja yule binti akiwa katika mizunguko yake ya hapa na pale akiwa mjini, alikutana na kaka mmoja akiwa katika mavazi ya kijeshi, na alikuwa na mwonekano mzuri sana, lakini cha kushangaza yule kaka baada ya kumwona binti yule aliduwaa. Baada ya kuduwaa kwa kipindi aliamua kumfuata binti na kumsalimia na kumuuliza kila kitu, na baadaye walianza kuwasiliana mawasiliano ya kawaida kabisa lakini mwanajeshi huyo alikuwa na mawazo tofauti, na ndipo siku moja akamweleza kuwa angetamani siku moja awe mke wake. Yule binti akamwambia hapana, mimi tayari nina mtu wangu na tunaheshimiana sana, akamwambia sawa. Kwa vile  ni watu marafiki alimrudisha mpaka kwao, kumbe lengo lake yule kijana ni kutaka kujua binti anaishi wapi.
Na ndipo siku hiyo yule kijana aliamua kwenda peke yake nyumbani kwa wazazi wa binti huyo na kukutana na baba yake (Baba wa binti). Na ndipo alipozumza ukweli wa kile alichokiona na lengo lake ni lipi. Na mzee aliweza kumdadisi kijana na kumweleza kila kitu. Kwa  wakati huo yule binti pamoja na mama yake walikuwa hawapo na binti aliporudi akamweleza akaelezwa na baba yake kuwa kuna kijana mmoja alikua yuko hivi na hivi akanieleza kila kitu, nadhani huyo ndiye atakayekufaa. Binti akamwambia hapana, wewe ndiye umemwona na mimi itabidi nimwone. Baadaye yule mjeshi akaja wakazungumza.

Baada ya mazungumzo marefu ya hapa na pale yule kijana mjeshi aliamua kuondoka, na kwa kuwa binti hakutaka kukorofishana na baba yake aliamua kukubaliana na mawazo yake na baadaye wakamwita tena kijana huyo mjeshi. Baadaye taratabu zote za kuoana na mjeshi huyo zikafanyika, kisha binti huyo alienda kwa mchumba wake wa kwanza na kumweleza yote yaliyotokea na kumrishia pete ya uchumba waliyovishana hapao awali. Kijana huyo alisikitika sana kwa uamuzi aliouchukua lakini hakuwa na jinsi aliamua kufuata shinikizo la baba yake. Hatimaye baadaye yule binti aliolewa na mwanajeshi na ndoa ilifungwa kanisani.

Baada ya ndoa tu kinachotokea sasa hivi ni kwamba kosa kidogo tu anaambulia kipigo ambacho hajawahi kukipata, kiasi kwamba inampelekea kumkumbuka yule wa kwanza ambaye walikuwa wakiongea naye kwa utaratibu kabisa.

Ndipo baadaye binti (ambaye sasa ni mke wa mwanajeshi) akamtafuta yule mchumba wake wa kwanza na kumweleza kila kilichotokea. Lakini kijana huyo alijaribu kumweleza namna ya kufanya ili waendelee kuishi vizuri na mume wake na kuzidi kumwombea ili waishi vizuri.

Kwa wakati huu kijana huyo bado hajaoa na anamweleza binti itachukua muda mrefu kwa sababu kwanza itabidi nikusahau wewe pili nikae chini nitulie tatu nijianze upya hivyo itachukua muda sana.
Kikubwa zaidi ni kuwa binti huyo amekubali kuolewa na mwanajeshi kwa shinikizo la baba yake, lakini kinachoendelea ni kwamba kosa dogo tu anaambulia kipigo kisicho cha kawaida na kinachomuuma zaidi zaidi huyo dada ni kuwa siku moja walipotoka NJE walienda sehemu ile ile ambayo walikuwa wakienda na mvulana yule wa kwanza na hivyo hii humuuma zaidi.
Sasa dada huyu anaomba mawazo, ushauri na maoni afanyeje???

Tuesday, August 27, 2013

MKWAWA SHUJUA!!

KAMA UNAKUMBUKA DARASA LA TANO WALE WENYE UMRI KAMA WANGU BASI UTAKUMBUKI UKURASA HUU WA KITABU HIKI CHA TUJIFUNZE LUGHA YETU! KITABU CHA SITA(6) KARIBU UKUMBUSHIE ENZI HIZOOOO
 
Hapo zamani palikuwa na mzee aliitwa Muyugumba. Mzee huyo alikuwa mtemi wa Wahehe. Alikuwa akipendwa sana na watu wake.

Mtemi Muyugumba alikuwa na watoto wengi. Wawili kati yao walikuwa Mkwawa na Muhenga. Siku moja aliwaita watoto hao wawili ili kuzungumza nao. Walipofika aliwaambia, "Wanangu, nimewaiteni usiku huu huu wa leo niwaeleze habari muhimu sana. Kwanza, mnajua kwamba mimi nimekuwa mtemi wa nchi hii kwa muda mrefu. Nimeweza kuwaunganisha watu wangu mpaka tumekuwa na kauli moja. Kwa ajili ya umoja wetu, tumeweza kuwashinda maaduni wetu. Tumeweza kuhifadhi uhuru wetu. Sasa mimi ni mzee. Nguvu zinaanza kumalizika taratibu. Nimetazama katika watoto wangu wote sikumwona ambaye ataweza kuendesha kazi yangu ila ninyi. Hivyo leo nimewaita kuwapeni usia wangu.

"Mimi karibuni nitakufa. Nitakapokufa nanyi mtaitawala nchi hii. Kwa hiyo, wewe Mkwawa utakuwa mtemi wa Kaskazini; nawe Muhenga utakuwa mtemi wa Kusini ya Iringa. Ninaigawa nchi sehemu mbili ili kazi yenu iwe rahisi. Jambo kubwa ninalotaka mlikumbuke wakati wotw ni kudumisha uhuru, heshima na umoja katika nchi ya Uhehe. Msiposhirikiana hamtaweza kufanikiwa; na kazi yenu itakuwa ngumu sana." Mkwawa na Muhenga wakajibu wote kwa pamoja, "Asante baba. Tutafanya kama ulivyotuagiza."

Haukupita muda mrefu, Mtemi Muyugumba akashikwa na ugonjwa, akafa. Wahehe wakawa na huzuni sana kwani walimpenda sana kiongozi wao. Matanga yalipokwisha Mkwawa aliwekwa kuwa mtemi wa kaskazini ya Iringa na Muhenga kusini kama walivyousiwa na baba yao. Kwa bahati mbaya Muhenga alikuwa mchoyo. Hakuridhika na sehemu yake ya utawala. Hivyo aliyaamrisha majeshi yake yamvamie Mkwawa; nayo yakamvamia. Lakini Mkwawa hakukubali. Alipigana kiume, mwisho akamshinda nduguye akawa mtemi wa nchi yote ya Iringa kama ilivyokuwa wakati wa marahemu baba yake.

Wakati wa utawala wa Mkwawa, kulitokea wageni weupe kutoka Ulaya. Wageni hao walikuwa ni Wajerumani. Walifika katika nchi yetu ili kuondoa utawala wetu wa jadi na kuweka utawala wao wa kigeni. Kwa kweli wageni hao walikuwa katili sana. Waliwaua babu zetu bila kosa lolote. Waliwapiga bakora kama wanyama. Walifanya kazi katika mashamba yao, wakatengeneza mabarabara na kujenga majumba yao makubwa makubwa. Yote haya yalikuwa kwa ajili ya manufaa yao. Jambo lililokuwa baya zaidi ni kuwa waliwafanya babu zetu kuwa si binadamu kamili kama wao. Walitunyangánya nchi yetu kushibisha matumbo yao.

Mkwawa hakuweza kuvumilia ukatili wa Wajerumani. Hakupenda watu wake watawaliwe na wageni. Kwa hiyo, hakuwa na njia nyingine ya kufanya ili kuyakabili majeshi ya Wajerumani. Jamboo la kwanza alilofanya ni kuimarisha majeshi yake. Vijana wa Kihehe walijiandikisha kuwa askari kwa wingi sana. Ili Mkwawa awape askari wake mafunzo bora ya kivita, alijenga kambi kubwa mahali pamoja panapoitwa Kalenga. kambi hii ilizungukwa na ngome kubwa sana. Katikati ya ngome hiyo palijengwa nyumba kubwa. Hiyo ndiyo ilikuwa makao makuu ya Mkwawa. Pia mlikuwemo nyumbo za askari, mifugo na mashamba ya vyakula. Ngome hiyo ililindwa barabara na askari wa zamu usiku na mchana. Ilikuwa ikiitwa "Liringa", yaani "ngome kuu ya Vita." Kila kijiji kilikuwa na ngome za aina hii ili kuwalinda wananchi.

Baada ya kupigana kwa muda mrefu, na Wajerumani wengi kuuwawa, Mtemi Mkwawa aliweza kushinda Wajerumani. Lakini majeshi yake yalianza kudhoofika kwa sababu askari wake wengu waliuwawa. Wajerumani walipowashika viongozi wa Wahehe waliwanyonga hadharani!

Mkwawa alipoona kwamba Wajerumani wanazidi kuimarisha majeshi yao, na kwamba walikuwa wanamtafuta ili wamuue, alitoroka na kwenda msituni. Alitoroka na askari wake wawili ambao walikuwa wamekula kiapo cha uaminifu cha pamoja naye. Mara siku moja Mkwawa akajiona amezungukwa na majeshi ya Wajerumani. Alikuwa mtu shujua ambaye hakupenda kukamatwa mateka wala kuacha mwili wake uguswe na mzungu . Hivyo alijiua mwenyewe kwa bunduki kabla Wajerumani hawajawahi kumgusa.

Kweli Mkwawa alikuwa shujua. Anatukumbusha kuwa babu zetu hawakupenda kutawaliwa na wageni. Hawakupenda kupuuzwa. Hivyo walikuwa tayari kufa kuliko kutawaliwa.

Monday, August 26, 2013

HUU NI MCHANA MWINGINE YA JUMATATU .....KARIBU TUJUMUIKE HAPA JAMANI....

Picha hii imenikumbusha mbali sana huu ni mtindo mzuru sana kula hivi sahani moja ....Ila kuna kitu kimoja kilikuwa kinanishinda hapa nilikuwa nakula taratibu mno na ninaposhtuka ugani umeisha. Ni mtindo mzuri maana hapo ndipo wote mnaweza kukusanyika na kuongea pia ila si sana maaana kila mtu anakuwa hana nafasi ya kuongea.....isipokuwa kushiba....Je nawe msomaji unakumbuka hii?
JUMATATU NJEMA!!!!

Sunday, August 25, 2013

NI DOMINIKA YA 21 YA MWAKA C..WATOTO


Watoto wana hali ya kimbingu. kwani wana kila sababu: unyofu. utulivu. amani, upendo, furaha, mapatano. umoja, ushirikiano. usikivu na unyenyekevu. Ndiyo maana hata Bwana wetu yesu Kristu alisema: "Waacheni wadogo waje kwangu." Hali hii inatakia kwa kila mmoja wetu ili baada ya maisha haya ya sasa tukafurahi pamoja na Mungu katika utatu, milele yote mbinguni.
JUMAPILI NJAMA

Friday, August 23, 2013

TUANZA MWISHO WA JUMA NA UJUMBE HUU MUWE NA WAKATI MWEMA!!


 NA MSANII MRISHO MPOTO....

AU LABDA TUENDELEEE NA UJUMBE HUU

Tumkomboe mwanamke mimi na wewe tukomboe Taifa, kwani ni yeye mama ni yeye mwanzo Taifa...taifa bora huanzia tumboni mwa mama.....endeleee  yaani hapa nipo hoi maana  mapigo ya ngoma yanafanana na ngoma ya lizombe......
IUJUMAAA NJEMA KWA WOTE:-)

Thursday, August 22, 2013

SWALI LA WIKI LILILOPENDWA NA KAPULYA...MKE AU MUME NI NANI KWAKO?

Jana jioni/usiku nikiwa kazini nilipata wasaa wa kusikiliza redio ya http://ebonyfm.com  au pia waweza kuingia http://www.radiostationstz.co na kisha bofya EBONY FM (radio ya 6 toka juu. Basi jana kulikuwa na mada- swali moja nzuri sana na kidogo ya kuchanganya...lilisema hivi:- Mke wako ni mke, rafiki au ndugu? na vivyo hivyo kwa Mume je? ni mumeo, rfikiyo au nduguyo?.....Niliipenda sana mada hii ila bahati mbaya nilishindwa kuchangia na nimeona niiweke hapa maisha na mafanikio na tuweze kujadili kwa pamoja.....KARIBUNI SANA

Wednesday, August 21, 2013

BINADAMU NA MAZINGIRA:- KUFANYA UAMUZI NI MUHIMU KATIKA MAISHA

Nimeamka na kama kawaida nikiwa na mawazo mengi kichwani, mmmhhh nikaona ngoja niende kukimbia ili kuweza kufanya takafari. Unajua unapokimbia au tembea mstuni unaweza kuchanganua mawazo vizuri sana maana kupo tulivu. Basi nikaanza kuaendelea kuwaza hili ambalo ni muda sasa nilikuwa nikiliwaza.:- Linahusu jinsi ilivyo muhimu kufanya uamuzi...Hivi ndivyo nilivyowaza:-
Nikaanza hivi, Maish huenda bila kuamua? na nikajipa jibu mmmh:- Maishahayaendi hivyo na hata siku moja haijatokea mtu asiyejue anataka nini maishani kufanikiwa au kutulia. Kama mtu ameamua kufanya biashara  kwa mfano ya genge basi inabidi ajizatiti sana na biashara hiyo na aipange mipango yote ya kuikuza.
Na nikajiuliza je kama mtu anataka kusoma afanyeje? Kama mtu ameamua kusoma masomo fulani au kufanya kazi aina fulani, basi inabidi azingatie hilo na wala asiyumbe.
Kila siku huwa tunasikia watu wakisema , "yule jamaa alianza kuuza chapati na vitumbua tu, lakini angalia sasa alivyotajirika ana mabasi na maduka mji mzima". Au mfano mwingine utasikia wakisema "yule jamaa alianza masomo yake kwa njia ya posta tu lakini sasa yupo chuo kikuu". Hizi kauli huwa zinatamkwa sana lakini bila shaka  hatujawahi kujiuliza inakuwaje hadi mtu kama huyu kufikia juu kiasi hicho kutoka alipoanzia ambako wengi wanadhalau na kukata tamaa?
Kwa hiyo hapa nikagundua kwamba:- Tukianza kujiuliza sasa tutajua kwamba sababu kubwa ni mpango inayotokana na kujua kwamba anataka kitu gani maishani mwao. Kwa sababu wanajua wanakokwenda wanachokitafuta, hata mambo yakienda kombo watangángánia tu kufanya shughuli zao. Wale wasiojua wakiyumba kidogo tu huacha kile wakifanyacho na kukimbilia kingine.
UJUMBE:- Ninachotaka kusema hapa katika maisha mtu unatakiwa kuwa  malengo hata kama malengo hayo utafanikiwa baada ya miaka kumi. Kwa kuwa ni malengo ndiyo ambapo utaweza kwanza kutulia na baadaye kufika kule unakokutaka
KAMA HUJAWEKA MALENGO KWA UNAYOTAKA KUYAFANYA KATIKA MAISHA FANYA SASA.
NAWATAKIENI KILA LA KHERI NA TUSIWE NA TABIA YA KUKATA TAMAA: KAPULYA

Tuesday, August 20, 2013

PALE MILA NA DESTURI ZINAPOPISHANA...TUMEMZIKA MAMA IRENE IJUMAA 16/8-2013 TANGU ALIPOTUACHA 3/11/2012!!!

Kama wengi mnakumbuka mwezi Novemba tarehe 3 mwaka jana nilifiwa na mama mkwe wangu ghafla tu kwa kujikumbusha inga hapa. nachotaka kusema hapa ni kwamba ijumaa ya tarehe 16/8 -13 ndiyo tumemzika mama Irene. Sababu kubwa ya kusubiri muda mrefu kiasi hiki ni kwamba:- Kwanza ardhi ilikuwa ni ngumu kuchimba kaburi baridi kali mno..Pili ni kwamba mwili wa mama Irene ulichomwa moto. Hakika hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona utamaduni huu. Kwa hiyo kwenye hicho chombo hapo chini ni masalio ya mwili wa mama Irene

Mwili/majivu ya mama Irene

 Hapa pia na mishumaa imewashwa
Na hap ndiyo safari yake ya mwisho kwenye nyumba ya milele. Walichimba kashimo tu ili kutosheleza hicho chombo kilichokuwa na majivu. Na ni kaburi alilozikwa baba mkwe pia kwa hiyo wote wamezikwa katika kaburi moja..Duh ama kweli tembea uone mengi ila kuchomwa moto..mmmhhh sijui!! UPUMZIKE KWA AMANI MAMA YETU MPENDWA IRENE.

Monday, August 19, 2013

JUMATATU HII TUANZA NA MWANADADA HUYU NA UVAAJI WA MIWANI...MTINDO


Mdada huyu si mpenzi wa mikanda tu ni mpenzi wa kuficha sura yake pia ila si wakati wote ni mara chache. Angalia picha hizi
...Hapa ni Jangwani mwamzoni mwa mwaka huu ilikuwa Raha sana

Hapa ilikuwa 2010 
NAWATAKIENI JUMATATU NJEMA. Hapa ni Silver sands Dar es salaam 2011

Sunday, August 18, 2013

HILI NI CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KWA JUMAPILI HII YA LEO :UJUMBE!!

Elimu ni mali ambayo adui hawezi kuiteka. Maana ya msemo huu ni kwamba; mtu akishapata elimu, hii ni mali yake ambayo hakuna mtu anayeweza kuiteka na kuinyang'anya kwa kuwa hiyo ni sehemu ya utu wake. Pia elimu humsaidia kumfahamu Mungu vizuri zaidi aliye asili ya elimu na maarifa yote
JUMAPILI NJEMAKWA YEYETO ATAKAYEPITA HSPA.!!!!!

Saturday, August 17, 2013

KUMBUKUMBU YA MAMA ALANA NGONYANI!

MAREHEMU MAMA ALANA NGONYANI 1952-2004
Imetimia miaka 9 tangu ututoke ghafla usiku wa tarehe 17 Agosti 2004 wakati bado  tulikuwa tunakuhitaji. Ingawaje kimwili umetutoka, kiroho bado tunakukumbuka. Tunakukumbuka siku zote kwa upendo wako, mawazo yako yaliyojaa busara , ukarimu/ucheshi na malezi bora. Tulikupenda lakini Mungu alikupenda zaidi.
Tunamwomba Mwenyezi Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi. AMINA
Na tumkumbuke mama yetu kwa wimbo huu

+TUTAKUKUMBUKA MILELE MAMA YETU MPENDWA ALANA NGONYANI+


Friday, August 16, 2013

IJUMAA YA LEO TUTEMBELEA BAGAMOYO KATIKA SHULE YA MZEE DIGALO´S YA MUSIKI WA ASILI/UTAMADANI WETU!!

Nimependa sana huyu mzee alivyoamua kuwafunza hawa watoto hawa uasili. Maana hawa watoto wetu ndio watakaoeneza utamaduni wetu, kwa watoto wao na wao kwa watoto wao tukiacha tu utakufa... Hakika inapendeza sana. Na ndio nimeona tuanza mwanzo wa mwisho wa juma kinamna hii. NAWATAKIENI WOTE MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA HILÖI

Thursday, August 15, 2013

NAOMBA TAFSIRI YA NENO KIONGOZI/VIONGOZI...MAANA LINANIKERA MNO.......!!!

Nimeamka leo nikiwaza hili neno KIONGOZI/VIONGOZI nikashindwa kuliwazua nikaamua kuchukua KAMUSI  SANIFU YA KISWAHILI CHETU. Nayo ikaniambia hivi:-KIONGOZI/VIONGOZI.....
1. mtangulizi wa jambo fulani au wa kikundi cha watu, mkubwa anayesimamaia shughuli maalumu kwa kueleza au kuelekeza. AU...
2. Kitu kinachosaidia kuonyesha au kuelekeza......
Je? hawa viongozi wanaongoza kweli au wanajiongoza? Naomba tutafakari au jadili kwa pamoja.
Ndimi Kapulya wenu:-)

Tuesday, August 13, 2013

NILICHOKUTANA NACHO ASUBUHI YA LEO WAKATI NAFANYA MAZOEZI YANGU YA KUKIMBIA......ADUI KA/NYOKA!!!!

Nimekimbia nimekimbia mchaka mchaka ,chinja, mchaka mchaka chinja, alimselma Hadijax2...Bahati mbaya nzuri macho yalikuwa yakiangalia chini ..weweeeee nilipoona hako kanyoka niliruka sikumbuki hatua ngapi utadhani wale wanariadha wanapokimbia na kuruka . Ni kadogo lakini nyoka ni nyoka tu....nikasimama nikuchukua picha hii, kwanza nikakarushia aina ya jiwe, halafu hiyo fimbo muionayo kimya kusogea karibu ...kumbe amekufa. Nilikasema moyoni duh! nilikuwa na bahati sana maana siwapendi nyoka.UJUMBE WANGU:- Tuwe waangalifu tunapokuwa tukitembea na hasa mstuni na hata barabarani.

Monday, August 12, 2013

TUANZE JUMATATU HII KWA MLO HUU WA ASUBUHI YA LEO CHAI CHAPATI ZA KUTENGENEZWA KWA MIKONO YANGU MIMI KAPULYA...!!

 Nimekumbuka nikiwa nimeshaanza kukaanga kuwaonyesha tangu mwanzo..ni hivi unahitaji unga wa ngano, chumvi kidogo, sukari kidogo, mafuta  na maji moto hivi nifanyavyo mimi .Unakanda unga na hivyo nilivyotaja na baadaye unasukuna na hapa chapati ikiwa kwenye flampeni inakaangwa 
Na hapa tayari zipo zinasubiri walaji, chapati, kuna chai ya rangi na ya maziwa na wale wanaotumia sukari ipo kwenye hichi kibweta cheusi kwa hiyo karibuni sana tujumuuke.JUMATATU NJEMA KWA WOTE.

Sunday, August 11, 2013

JUMAPILI HII TUANGALIA HADITHI YA MAISHA YA YESU KWA KIBENA!!!

UDALIKE uliyerekodi hii kwa kibena. Nimefurahi kweli kusikia LUGHA YA KIBENA kwa mara nyingine nimejisikia kama nipo ubenani. HAYA NAWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA NA UPENDO NA AMANI PIA UTULIVU UTAWALA KATIKA NYUMBA ZENU. KRISTU NI TUMAINI LETU.

Friday, August 9, 2013

IJUMAA YA LEO :-KUMBUKUMBU KITABU CHA JUMA NA ROZA

Nakuambia kitabu hiki nimekisoma na nilikuwa nakipenda sana..hadithi hi imekaa kichwani utafikiri sala la baba yetu au wimbo wa Taifa...Je Unaikumbuka pia?

Thursday, August 8, 2013

MASAHIHISHO KIDOGO:- Car for hire in Dar-es-Salaam

You can hire this car in Dar.
The car with a driver will only cost you 100'000TZS (500SEK), +petrol +300TZS per mile (1,6km),
for one day in the city of Dar-es-Salaam.
About 60 Euro, 48 pounds, or 75 USD.
For trips outside Dar contact us.
Torbjörn Klaesson +46 70 2217044
or
Yasinta Ngonyani +46 70 2569176 mail: ruhuwiko@gmail.com

Wednesday, August 7, 2013

WAKATI WA KUVUNA UMEFIKA SASA YAANI MPAKA RAHA NI KUTOKA TU NJE NA KUCHUMA/KUCHUKUA NA KULA:-)

Mnaona raha ya kulima nyanya zimeanza kuiva kwa hiyo hakuna kununua nyanya kwa muda sasa. Halafu ni tamu sana..Si mnaona zilivyofungamana kwa hiyo nawakaribisha tujumuike ...
Hapa ni njegere nazo zimezaa kweli ..
Maboga nayo hayoooo  :-)
 
Vitunguu navyo havipo nyuma, kwa hiyo hakuna kununui vitunguu kwa muda. Mliopo jirani karibuni na wote wengine. Nipo kwenye mkakati wa kupanda ile vigiri nitawaonyesha hivi karibuni ni vipi kuwadhibiti wale viwavi...Nitajaribu

Tuesday, August 6, 2013

UJUMBE WA LEO JUMANNE NI KAMA UFUATAVYO!

Wakati mwingine ni bora kuwa mpweke ili kukwepa kuumizwa!!! Nawatakieni wote jioni/mchana au asubuhi na pengine usiku njema/mwema. Pia IDD NJEMA. KAPULYA

Monday, August 5, 2013

TUANZE JUMATATU HII KWA WIMBO HUU YASINTA!!!

KIJANA WANGU KANIONYESHA WIMBO HUU NIMEONA UWE HAPA KIBARAZANI...NAAWATAKIENI JUMATATU NJEMA SANA.....

Friday, August 2, 2013

IJUMAA YA LEO TUANGALIE BAADHI YA MISEMO YA KANGA..

1. Upendo na Amani Ametujalia Mungu
2. Likinifika nitakujibu.
3. Usimwingilie aliyepewa kapewa.
4. Kuolewa ni sheria kuzaa ni majaliwa.
NAWATAKIENI WOTE JIONI YA IJUMAA HII IWE NJEMA NA MWANZO MWEMA WA MWISHO WA WIKI......Kapulya

Thursday, August 1, 2013

UTAMU WA KULIMA BUSTANI NI SASA: VIAZI VYA KULIMA KWA MIKONO YANGU MWENYEWE LEO TWALA....MLO WA JANA JIONI

 Hivi ni vile viazi angalia hapa na jana jioni ndiyo ikafikia muda wa kuangalia kama vyaweza kuliwa na matokeo yako yakawa kweli vyaweza kwa hiyo jana jioni tumekula viazi vya kulima Nangonyani.......kama
....uonavyo kwenye sahani hapa ni viazi , broccoli, nyanya kidogo, limao na samaki aina ya salmon(kiswahili ) nisaidieni ......kilikuwa kitamu mno....nawashauri wote mlio  na nafasi ya kulima bustani kulima viazi mviringo....NAWATAKIENI ALHAMIS NJEMA NA MWANZO MWEMA WA MWEZI AGOSTI:-)