Thursday, August 22, 2013

SWALI LA WIKI LILILOPENDWA NA KAPULYA...MKE AU MUME NI NANI KWAKO?

Jana jioni/usiku nikiwa kazini nilipata wasaa wa kusikiliza redio ya http://ebonyfm.com  au pia waweza kuingia http://www.radiostationstz.co na kisha bofya EBONY FM (radio ya 6 toka juu. Basi jana kulikuwa na mada- swali moja nzuri sana na kidogo ya kuchanganya...lilisema hivi:- Mke wako ni mke, rafiki au ndugu? na vivyo hivyo kwa Mume je? ni mumeo, rfikiyo au nduguyo?.....Niliipenda sana mada hii ila bahati mbaya nilishindwa kuchangia na nimeona niiweke hapa maisha na mafanikio na tuweze kujadili kwa pamoja.....KARIBUNI SANA

6 comments:

Anonymous said...

Mi naona mkeo au mmeo wa ndoa ni NGUGU yako, hawezi kuwa girlfriend au boyfriend. Hiyo ndoa ndio umeleta udugu. By Salumu.

Anonymous said...

Mke au mume ni rafiki tu. Mbona sioni kama kuna undugu. Ndugu wa damu au ndugu kivipi? Yani kama ni ndugu basi ni wa kuanzia mkifunga ndoa na ikitokea mmeachana mana yake undugu unaisha au? ukiolewa na mwingine tena anakuwa ndugu yako so you can have as many ndugu as possible! Kwa kweli hakuna undugu ni urafiki ´wa karibu sana. Mtu ambaye hukuwa unamjua anakuwaje ndugu ukubwani? Najiuliza tu naona kama hakuna undugu kabisa.

Anonymous said...

Hapo ni urafiki tu.
Ndugu hata mkipigana na kupelekana polisi na hata jela ,undugu una baki palepale.

ray njau said...

Inamaanisha Nini Kumtunza Mke Wako?
===================================
Ikiwa unamthamini mke wako, utamtunza sana kwa sababu unampenda. Unaweza kufanya hivyo kwa njia mbalimbali. Kwanza, tumia wakati wa kutosha pamoja na mwenzi wako. Ukimpuuza mke wako kuhusiana na jambo hilo, upendo wake kwako unaweza kupoa. Pia, fikiria hili, inapohusu wakati na uangalifu huenda kile ambacho unadhani mke wako anahitaji kisiwe kile anachohitaji. Haitoshi tu kusema kwamba unamthamini mwenzi wako. Ni lazima mke wako ahisi kwamba anathaminiwa. Paulo aliandika hivi: “Kila mmoja na aendelee kutafuta, si faida yake mwenyewe, bali ile ya yule mtu mwingine.” (1 Wakorintho 10:24) Ukiwa mume mwenye upendo, unapaswa kujitahidi kuelewa mahitaji kamili ya mke wako.—Wafilipi 2:4.

Njia nyingine ya kuonyesha kwamba unamthamini mke wako ni kumtendea kwa wororo, kwa maneno na kwa matendo. (Methali 12:18) Paulo aliwaandikia hivi Wakolosai: “Enyi waume, endeleeni kuwapenda wake zenu nanyi msiwakasirikie kwa uchungu.” (Wakolosai 3:19) Kulingana na kitabu kimoja, sehemu ya mwisho ya maneno ya Paulo inaweza kutafsiriwa hivi “usimtendee mke kama mfanyakazi wa nyumbani” au “usimfanye mke kuwa mtumwa.” Bila shaka, mume ambaye ni mkatili, iwe hadharani au faraghani, anaonyesha kwa kweli kwamba hamthamini mke wake. Mume anayemtendea mke wake kwa ukali, anaweza kuharibu uhusiano wake pamoja na Mungu. Mtume Petro aliwaandikia waume hivi: “Enyi waume, endeleeni kukaa nao [wake zenu] vivyo hivyo kulingana na ujuzi, mkiwapa heshima kama chombo dhaifu zaidi, yaani, mwanamke, kwa kuwa ninyi pia ni warithi pamoja nao wa pendeleo lisilostahiliwa la uzima, kusudi sala zenu zisizuiwe.”*—1 Petro 3:7.

Usipuuze upendo wa mke wako. Mhakikishie kwamba bado unaendelea kumpenda. Yesu aliwawekea waume Wakristo mfano kupitia jinsi alivyolitendea kutaniko la Kikristo. Alikuwa mwororo, mwenye fadhili, na mwenye kusamehe, hata wafuasi wake waliporudia-rudia kuonyesha sifa zisizopendeza. Hivyo, Yesu angeweza kuwaambia wengine hivi: “Njooni kwangu, . . . kwa maana mimi ni mwenye tabia-pole na mnyenyekevu moyoni, nanyi mtapata burudisho kwa ajili ya nafsi zenu.” (Mathayo 11:28, 29) Mume Mkristo anayemwiga Yesu anamtendea mke wake kama Yesu alivyolitendea kutaniko. Mwanamume ambaye kwa kweli anamthamini mke wake, na kuonyesha hivyo kwa maneno na matendo, atakuwa chanzo cha burudisho la kweli kwa mke wake.

Yasinta Ngonyani said...

Ngoja nami nisemi kili ninachojua/fikiri...Mke ni mke na rafiki lakini si ndugu...na cilevile mume ni mume na rafiki yangu lakini kamwe hawezi kuwa ndugu. Kwasababu huwezi kuoa nduguyo au kuolewa. Ila pia hii inachanganya kidogo...tuendelee kuchangia na mwisho tutaona tutagota wapi?...

Ester Ulaya said...

mimi naona ni rafiki