Monday, August 12, 2013

TUANZE JUMATATU HII KWA MLO HUU WA ASUBUHI YA LEO CHAI CHAPATI ZA KUTENGENEZWA KWA MIKONO YANGU MIMI KAPULYA...!!

 Nimekumbuka nikiwa nimeshaanza kukaanga kuwaonyesha tangu mwanzo..ni hivi unahitaji unga wa ngano, chumvi kidogo, sukari kidogo, mafuta  na maji moto hivi nifanyavyo mimi .Unakanda unga na hivyo nilivyotaja na baadaye unasukuna na hapa chapati ikiwa kwenye flampeni inakaangwa 
Na hapa tayari zipo zinasubiri walaji, chapati, kuna chai ya rangi na ya maziwa na wale wanaotumia sukari ipo kwenye hichi kibweta cheusi kwa hiyo karibuni sana tujumuuke.JUMATATU NJEMA KWA WOTE.

10 comments:

ray njau said...

Ukarimu wako ni wenye thamani sana japo kwa macho kuona; nami nasema asante sana!

Mija Shija Sayi said...

Kweli kabisa nilidhani ni yai kabla sijasoma maelezo...

Zinaonekana tamu ile mbaya.

Hongera kwa kipaji cha kupika.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! Chakula kinanoga mkiwa wengi.....karibu sana.

Dada mkuu msaidizi! ni tamu sana wahi basi ujumuike nasi...tena kimbia

Mfalme Mrope said...

kwa! huku sasa ni kuringishiana! sasa huku madongo kuinama nitakaribiaje chapati huko kwenu? Haya mi nimebaki ka mzee fisi...kudos my sis zinaonekana ni tamu kweli!

Anonymous said...

Jamani chapati zinakwisha! Msinisahau na miye! By Salumu.

Anonymous said...

Yasinta leo asubuhi ni chapatti,kwa kweli nimezitamani sana ila ndio hivyo siwezi kuwahi. Ila siku nikija ntaomba na chapatti uniandalie.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mrope! Eeeeh kwanza karibu tena maana ulipotea kiduchu. Et madongo kuinama nimecheka:-D kweli hapa. Usikond utazikuta zipo nyingiiii.
Kakangu Salumu! Haziishi na wala hujasauliwa.

Usiye na jina! Wala usikonde utapata tu. Nakusubiri kwsa hamu na mlango upo wazi

Nancy Msangi said...

Da yasinta zinatamanisha kweli, mmmh,

Nancy Msangi said...

Da yasinta zinatamanisha kweli, mmmh,

Yasinta Ngonyani said...

Karibu Nancy karibu sanatujuike di unajua chakula mkiwa wengi kinavyonoga.