Tuesday, March 31, 2009

Monday, March 30, 2009

UPENDO KWA NCHI YANGU +MAISHA

Sijui kama wenzangu mmewahi kujisikia hivi, mwenzenu leo nimeamuaka na kujiona ya kwamba:- Ninaringa kwa kuwa Mtanzania nchi yangu yenye sifa zote za ustaarabu.

Ninaringia rangi yangu nyeusi, macho meupe, ngozi yangu nyororo, ninapendeza na nywele zangu nyeusi na kiswahili ni lugha yangu.

Ninajivunia nchi yangu ya Tanzania yenye miji ya kuvutia iliyojengeka. Angalia Dar es salaam, Mwanza nayo Dodoma bila kusahau kwenye marashi mji wetu Zanzibar. Halafu ukienda Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa na Songea.

Mnajua kuna vivutio vingi ndani ya Tanzania vinavyotufanya sote tujivunie kwa mfano kuna bahari fahari ya Taifa, Ziwa nyasa, viktoria, Tanganyika pia mlima mkubwa barani afrika Kilimanjaro. Bila kusahau mbuga za wanyama Serengeti, Ngorongoro, Tarangire, Mikumi n.k.

Sunday, March 29, 2009

LEO NIMEONA NIJIPENDELEE+ JUMAPILI NJEMA KWA WOTE PIA


Maisha ni safari ndefu watu tumetoka mbali

Friday, March 27, 2009

MAISHA BAADA YA KIFO

Nimesoma mjadala uliowekwa na Shabani Kaluse uliokuwa na kicha cha habari kisemacho "BADO WATU WANA HOFU JUU YA KIFO" Nami nimeona niendeleze mjadala huu kwa mada hii.

Baada ya kifo kinatokea nini?
Kuhusu kifo kuna mitazamo mbalimbali inayotofautiana kadiri ya imani ya mtu. Katika maisha ya binadamu kwa kipindi chote cha maisha yake, amakuea akipambana vikali sana na swali hili: “Baada ya kifo changu kitaendelea nini?” Jibu la swali hili lina maana sana katika maisha yetu hapa duniani, ingawa watu wengi wanaogopa kuongea juu ya jambo hilo. Madhehebu mbalimbali ya dini yamekuwa yakitoa majibu ya swali hili kadiri ya imani ya mapokeo yao.
Wakristo wanaamini nini?
Lakini katika imani hizo zote, tumaini la wakristo ni la uhakika kwa sababu kuu mbili. Moja, Ufufuko wa Kristo na Pili ni ushuhuda wa Maandiko Matakatifu. Biblia inatupatia picha ya kweli na kamili kuhusu kitakachoendelea baada ya kufa. Hata hivyo, wakristo wengi wameelewa vibaya juu ya maisha baada ya kufa. Wengine wanaamini kwamba watakuwa miongoni mwa malaika, wengine wanaamini wataingia katika hali ya usingizi wa roho, wakati wengine wanaamini kwamba watakuwa wanaelea katikati ya mawingu.
Wakristo wanaamini kwamba Kifo sio kitu cha kuogopa, badala yake katika kufa ndipo tutafikia kilele cha maisha yetu yaani kurudi kwa Baba Mbinguni. Kuishi maana yake tunadumu katika nchi ya kigeni. Kifo kimepoteza maumivu yake na sasa kifo ni ushindi kupitia Ufufuko wa Yesu Kristo Bwana wetu.
Wakana Mungu(Atheists)
Wakana mungu(Atheists) wanaamini kwamba mtu akifa ndio mwisho wake. Hakuna maisha baada ya kifo wala kwamba kuna roho ambayo inakwenda Mbinguni na itaendelea kuishi milele. Tunachotakiwa kutegemea maishani ni kwamba kifo hakiepukiki, binadamu lazima afe na maisha ya ulimwengu huu yana mwisho.
Wale wanaoabudu miungu(Pantheistics) wanafundisha kwamba mtu yumo katika mzunguko usio na mwisho na umwisho mpaka mzunguko huo unapovunjika ndipo mtu anakuwa kitu kimoja na mwumba wake. Namna mtu atakavyokuwa katika maisha ya baadaye inategemea namna gani aliyaishi maisha ya awali. Pale mtu anapounganika na muumba wake, palepale anakoma kuwa kuishi kama mtu, ila anakuwa sehemu ya nguvu za maisha matakatifu kama vile tone la maji linalotua Baharini.
Wale wanaoshikilia dini za makabila yanayosema kwamba vitu vyote vina roho(animistic) wanaamini kwamba baada ya kifo roho ya binadamu inabaki ardhini au inasafiri kwenda kuungana na roho zilizotangulia za mababu (wahenga) zilizoko duniani. Kwa milele wanatembea na wanatangatanga katika giza wakikumbana na furaha na huzuni. Baadhi ya roho hizo zilizotangulia zinaweza kuitwa tena kuja kusaidia na kuwatesa wale wanaoishi duniani.
Waislamu wanaamini nini?
Waislamu wanafundisha kwamba, mwisho wa dunia, Mungu atahukumu maisha na kazi za bainadamu. Wale ambao matendo yao mema yanazidi matendo yao mabaya wataingia paradizini. Wanaobaki wataingia ahera. Korani inafundisha kwamba paradizini watu watakuwa wanakunywa divai na kuhudumiwa na wasichana wa mbinguni na baadhi ya wasichana hao watakuwa wake zao.

Wednesday, March 25, 2009Ukiridhika na ulichonacho basi utaona maisha hayana ugumu.

Tuesday, March 24, 2009

MILA NA DESTURI/JE? KUTAHIRI WASICHANA NI HAKI?

Ni jambo la kutatanisha kidogo kwangu: Labda nianze hivi katika Tanzania tupo makabila tofauti. Na ni mengi na kila moja lina mila na desturi zake. Makabila 129 (130). Kwa hiyo hapa ninachotaka kusema ni kwamba hili jambo la kutahiri wasichana hasa wenzetu wamasai (pia nchi yenzetu jirani Somalia) lina maana gani? Kwa sababu wao wanadai wakishawatahiri ndo wanakuwa wanawake kamili na pia wanakuwa safi. Lakini papo hapo hawajui kama ni hatari sana :-

Tukianza na vyombo wanavyotumia, Je? Ni visafi au je wanabadili kwa kila mtoto hapana. Halafu kubwa zaidi je wanawapa ganzi? Hapana. Kwa sababu baada ya hapo inasemekana wanawashona na kuacha shimo ndogo sana kwa ajili ya kukojoa mkojo tu.

Je? Huyu msichana atapoolewa mnafikiri atapata maumivu kiasi gani wakati anatarajia kufanya tendo la ndoa kama sio mateso makali. Ambayo badala ya kuifurahia ndoa yake inakuwa kuijutia. Na itakuaje atapotarajia kuzaa. Kwa kweli na mateso makubwa sana atayapata. Ambayo atatamani hata asingeishi.

Kwa nini? Na je? ni safi kwa nani?. Kwa sababu msichana wa miaka mitano hawazi kuelewa ni nini kuwa mwanamke.
Na watoto wengi wamepoteza maisha yao wakati wa tendo hili, wengine wanapata tetanus, wengine wanapata mshtuko pia maambukizo mbalimbali. Tukiendelea hivi tutamaliza wasichana!!.

Monday, March 23, 2009

KUJIFUNZA KUPIKA UGALI+KUJITEGEMEA+KUMSAIDIA MAMAMtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Hapo mnaona jinsi anavyojitahidi kuusonga huo ugali ni mara yake ya kwanza. Jinsi ya kujitegemea hapo baadaye haitakuwa vigumu.

Sunday, March 22, 2009

NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA WOTE

Anayekataa kufundishwa anajidharau mwenyewe,
Bali anayekubali maonyo hupata busara.

Aendeye kwa unyofu huenda salama,
Bali apotoshaye njia zake atajulikana.

Malezi bora ya watoto wetu ndio msingi imara wa taifa la kesho.

NA PIA

Binadamu tunapanga mipango yetu,
Lakini kauli ya mwisho ni yake Mwenyezi Mungu.

Ana heri mtu yule amsikilizaye,
Akisubiri siku zote mlangoni pangu,
Akingoja penye vizingiti vya milango

Friday, March 20, 2009

MAISHA YA UJAUZITO+UTAMADUNI +UASILIKwa nini watu tunapoteza pesa kununua nguo za bei mbaya.Mnajua mara nyingi nimekuwa najiuliza kweli kiumbe hai kitakaaje humu tumboni miezi tisa. Mungu kweli ana miujiza yake. Ila pia akina mama tuna kazi kubwa sana. Huu mvao wake nimeupenda.
IJUMAA NJEMA KWA WOTEEEE!!!

Tuesday, March 17, 2009

MISHAHARA HAITOSHI+TUACHE UZEMBE KAZINI

Makala hii nimeipenda ndiyo maana nikaamua kumwomba http://hapakwetu.blogspot.com/ Kwani najua nakamilisha lengo lake la kuifanya isomwe na wengi.

Katika nchi yetu ya Tanzania, watu wanalalamika muda wote kuwa mishahara haitoshi. Gharama ya maisha ni kubwa kuliko mishahara. Hata kwa kuzingatia mahitaji muhimu tu, watu wengi wana haki ya kusema kuwa mishahara haitoshi.

Malalamiko ya mishahara kuwa haitoshi yanasikika duniani kote. Hapa Marekani, shida kubwa inayowakabili watu ni kulipa bili na madeni mbali mbali. Marekani ni nchi ya madeni. Kutodaiwa popote ni sifa nzuri katika utamaduni wa Tanzania. Lakini Marekani, sifa inakuja kutokana na umakini wa kulipa madeni. Mishahara ya Wamarekani wengi inaishia kwenye kulipa madeni. Kwa hivi, nao wanalalamika kuwa mishahara haitoshi.

Wako Watanzania ambao wana mishahara ambayo ingeweza kutosheleza mahitaji muhimu. Tatizo ni kuwa dhana ya mahitaji muhimu ina utata.

Tunaweza kusema mahitaji hayo ni chakula, malazi, mavazi, matibabu, elimu, na usafiri. Lakini, katika utamaduni wetu, orodha ya mahitaji muhimu ni kubwa zaidi ya hiyo. Kumlipia ada mtoto wa shangazi ni wajibu. Kuchangia gharama ya msiba kwa jirani ni wajibu. Kama una gari, kumpeleka mtoto wa jirani hospitalini ni wajibu.

Kwa msingi huo, hakuna Mtanzania ambaye anaweza kusema mshahara wake unatosha. Suala haliishii hapo. Je, ukitembelewa na marafiki, utakaa nao tu nyumbani na kuongea nao, au unatakiwa kuwapeleka mahali wakapate kinywaji? Je, unaweza kuacha kuchangia gharama za arusi ya rafiki yako?Tukizingatia hayo yote, mishahara haitoshi.

Watanzania wengi wana tabia ya kutumia fedha kwa mambo mengi mengine, ambayo umuhimu wake ni wa wasi wasi, kama vile bia. Kwa Watanzania wengi, bajeti ya bia ni kubwa sana. Kwa mtu anayekunywa sana bia, mshahara hauwezi kutosha. Lakini je, bia ni kitu muhimu namna hiyo?

Kwa upande wa pili, Watanzania tunapaswa kutafakari dhana ya mshahara. Mshahara unapaswa kuwa malipo muafaka ya kazi ambayo mtu anafanya. Kazi ndio msingi. Lakini, kuna tatizo kubwa Tanzania.

Watu wengi hawafanyi kazi kwa bidii. Muda mwingi wanatumia kwenye gumzo. Lakini wanategemea kulipwa mshahara, na wanalalamika kuwa mishahara haitoshi. Je, wanastahili hizo hela wanazopewa kama mshahara? Je, wakiongezwa mishahara, wataongeza juhudi kazini au wataendelea kukaa vijiweni na kupiga soga?

Huku Marekani, watu wanachapa kazi sana. Mshahara unatokana na kazi. Mtu asipofika kazini, halipwi. Akichelewa, malipo pia yanapunguzwa. Kwetu Tanzania mambo si hivyo. Mtu akishaajiriwa, anategemea kupata mshahara wake kila mwezi, hata kama anatumia masaa mengi kijiweni. Je, ni bora kuanzisha utaratibu wa kuwalipa wafanyakazi kwa yale masaa wanayokuwa kazini tu, na kupunguza mshahara kwa masaa wanayokuwa kijiweni?

Nami nataka kuongezea ni kwamba hapa Sweden ni karibu sawa na huko Marekani. Yaani hapa hata kama upo likizo hulipwi, inategemea ni likizo gani. Halafu kama unaumwa na halafu huendi kazini zile ziku mbili za kwanza hulipwi kitu kwa hiyo hapo ukiumwa basi ujue mshahara wako unapungua/unakatwa. Kwa hiyo kwa mtindo huo utakuta hata kama mtu unaumwa unajikaza na kwenda kazini. Kwani mshahara wanaokata ni mkubwa sana na ukizingatia maisha nayo yapo juu.

TUPO DARASANI+MAISHAUnaweza kuikuta hii picha kwenye postcards,kwanini mwafrika anapofanya kitu fulani wenzetu hupenda kukipeleka kwao na kuanza kuishangaa na kuto amini mbona sisi au mimi sijawahi kuona postcard zenye picha zao?

Monday, March 16, 2009

UTARATIBU WA SHULE

Ngoja leo tuangalie kuhusu utaratibu wa shule, nikiwa na maana utaratibu wa shule hapa Sweden na Tanzania. Kwani binafsi nimamaliza shule Tanzania na sasa naishi hapa. Kama si kusei nilipokuwa mdogo nakumbuka hata siku moja sijawahi kuona au kmwona au hata kusikia ya kwamba mzazi anakwenda shuleni kusikia maendeleo ya mtoto wake. Pia sijawahi kuona mzazi anakwenda shuleni siku moja kuwa na mtoto wake. Yaani kuona anafanya nini kweli yupo shuleni?

Hapa niishipo sasa nimeona na pia binafsi ni mzazi. Kwa hiyo kama mzazi nina jukumu kwabwa la kuwalea watoto wangu. Lakini pia ni sheria na pia ni utaratibu kila mzazi anaitwa shuleni kwenda kuona/kusikiliza maendeleo ya mtoto wako. Na hapo sio inaanza shule ya mzingi tu, hapana, ni tangu chekechea. Na sio mzazi/wazazi na mwalimu tu hapana na mtoto mwenyewe anakuwepo. Na jambo hili huwa linafanyika kila muhula mpya unapoanza. Unaambiwa jinsi mwanao alivyo na juhudi aa jinsi alivyo mzembe na kama anahitaji mwongozo gani. Leo nimekuwa shuleni kusikiliza maendeleo ya mtoto wangu ndio maana nimekumbuka kwa nini nilipokuwa nasoma mimi au mbona wazazi wangu walikuwa hawaji kusikiliza maendeleo yangu. Halafu nimekumbuka kumbe hakuna utaratibu kama huu.

Sunday, March 15, 2009

KARIBUNI CHAI BORA+JUMAPILI NJEMAUkitaka kukosana nami basi ninyime chai, tena bila sukari hapo tutakosana sana. Kama wasemavyo wakati wowote ni wakati wa chai.

Friday, March 13, 2009

KUMBUKUMBU + BWANA MATATA HAJUI KUSOMA/SHULE

Namshukuru babangu kwa kutunza kitabu hiki leo nimefurahi sana nadhani hata wenzangu mtafurahi pia kukumbuka hadithi hii:-
Bwana Matata yupo mjini, anauliza uliza njia ya hospital. Kuna kibao hapo njiani, lakini haui kusoma kibao.Bwana Matata anaona aibu kuuliza njia tena, anaona aibu kwa sababu hajui kusoma. Sasa anafuata njia ya bomani
Bwana Matata amechoka sana. Amechoka na safari, pia amechoka kuuliza uliza njia. Amelala kwenye kibao, kibao kinasema HATARI. Lakini Bwana Matata hajui kusoma, tena amechoka mno. Amelala njiani kwenye kibao

Bwana Polisi anapita, anamwona Bwana Matata amelala kwenye kibao. Bwana polisi anamwita, mzee vipi? Kwa nini unalala hapa? Huoni kibao? Lakini Bwana matata amechoka sana amelele kama gogo. Polisi amawita tena, kwa nini unalala hapa kama gogo? Kuna hatari hapa. Lakini bwana matata hana habari ya hatari hajui kusoma.

Bwana Matata akaamka, akasimama na kumwambia polisi, nataka kwenda hospitali. Mtoto wangu yupo hospitali ni mgonjwa sana, lakini nimepotea njia. Bwana polisi akasema, umepotea njia? Fuata hii Bwana Matata akafuata njia ile. Kinachoendelea naadhani mnajua

Thursday, March 12, 2009

MWANAMZIKI MCHANGA ERIK KLAESSON AKICHEZA FIDLA(FIOL)
Hapo juu ni kijana wangu akicheza fidla. Mwanamziki wa baadaye.

MJADALA WA LEO:- KWA NINI WATU TUTOE RUSHWA

Kichwa kinaniuma sana kila nikifikiria hili jambo la rushwa. Najua mtasema nimesahau mambo yanavyokuwa nchini mwangu. Labda NDIYO:- Ni hivi juzi tu nimetoka nyumbani Tanzania. Kusema kweli nilishikwa na butwaa, kwanza kabisa ni hivi baba yangu amestaafu mwaka juzi 2007. Amepata kiinua mgongo chake, na baada ya hapo inabidi apate (mafao) pesa kiasi fulani kila baada ya miezi mitatu. Lakini mpaka leo hizi za kila baada ya miezi mitatu hajapata. Kila akifuatilia kwenye maofisi yanayohusika wanamwambia njoo kesho au anayehusika hayupo. Yaani hapo wanachotaka babangu awape ya SODA kidogo wakati anataka HAKI yake. Je? hii ni haki kuwasumbua watu/wazee walioitumikia serikali?

Bado sijamaliza:- Jingine ni kwamba mimi ni mgonjwa nahitaji matibabu. Cha kushangaza unaambiwa nipe ya kula mchana. Kwa nini mimi nimpe ya chakula wakati yeye analipwa mshahara. Ndiyo, labda ana mshahara mdogo. Maa sasa inaonekana usipokuwa na refa basi huwezi kufanikisha kitu.

Swali:- Kwa nini inakuwa hivi? na kwa nini isiwe kinyume?

Wednesday, March 11, 2009

KARIBUNI TUJUMUIKE


Karibuni chakula ni chaguo lako ukitaka pweza chips au samaki changu chips. Kuwa nyumbani raha kweli unaweza kula chakula cha kutoka baharini mara hiyohiyo.

Tuesday, March 10, 2009

MAVAZI YETU /MAISHA YETU

Nimekuwa nikijiuliza mara nyingi juu ya mavazi yetu. Ni vazi gani ni la mwanamke na lipi ni la mwanaum? Pia siku hizi ni aibu tupu, utakuta mama na heshima yake anavaa nguo za mtoto wa miaka 10. Blauzi fupi kiasi kwamba tupo linaonekana na pia suruali ambayo inabana makalio (matako) na penginne hata nguo ya ndani (chupi) kuonekana. Wewe kama unajua ni mnene kwanini usishone/nunue nguo za saizi yako?

Hali hii haiko Ughaibuni tu, kwani sasa hadi kwetu Afrika imeshaigwa. Watu wanaacha mavazi yao mazuri ya asili, ya heshima pia utamaduni. Inasikitisha sana kuona utamaduni wetu(wa kiafrika ) unapotea. Labda pengine wengi wanafikiri vitu/nguo vitokavyo Ughaibuni ni BORA zaidi. Binafsi napenda sana utamaduni wetu na mavazi yetu. Sijui wenzangu mna mawazo tofauti nami? au?

Monday, March 9, 2009

SHAMBA LANGU LA MAHINDI NA MIGOMBA RUHUWIKO SONGEA

Wote nadhani mnajua kuwa si muda mrefu nimerudi toka nyumbani TZ. Pia ule msimu nilikuwa kule ulikuwa ni msimo wa kilimo kwa huyo nami sikuwa nyuma nimelima shamba la mahindi kama muonanyo.

Sunday, March 8, 2009

NAPENDA KUWATAKIA WOTE JUMAPILI NJEMA KWA UJUMBE HUU

Macho ya huruma hufurahisha moyo,
habari huburudisha mwili,
Kuchukiana huendekeza fitina,
Kupendana husitiri makosa yote.

Nilikuwa mgonjwa ukaja kuniona
Nilikuwa na njaa ukanilisha
Kumhudumia mgonjwa ni wito.

Jumapili njema jamani:-)

Saturday, March 7, 2009

SALAMU TOKA SONGEA TENA JE? NI KWELI?

Sidhani kama itawezekana kuacha kunywa ulanzi, hapa sitakubali kabisa kwani itakuwa wamekatisha starehe zote. Labda kuna anayekubaliana na ushauri huu.

Friday, March 6, 2009

SITASAHAU MWAKA 2004­-2005

Sitasahau:- Ghafla 18/8 2004 niletewa habari kuwa sina mama tena. Ilikuwa kama ndoto, kwani sikuletewa habari kuwa anaumwa. Kwa hiyo sikuamini kabisa. Kwa kweli ni pigo kubwa sana kuondokewa na mama. Huku mbali ugenini sikujua nifanye nini, kwenda nyumbani ni mbali. Maisha yangu yanazidi kuwa magumu;- ningebaki nyumbani NINGE. Kwani kuna mambo mengi watu wanahitaji kuongea /kupata ushauri wa mama, sasa nitaenda wapi. Kila nikifikiria hili jambo nakosa raha kabisa. Pole mama yangu hajawafaidi /hajacheza na wajukuu wake. Na pia pole mimi sijamfaidi mama. Namshukuru mume wangu pamoja na marafiki wote kwa kunifariji wakati nilipokuwa na majonzi. Naweza kusema ilikuwa si mbali sana ningechanganyikiwa kabisa. Kwani kidogo nilichanganyikiwa niliacha kula nilikataa kwenda kazini pia shuleni nilichotaka ni kulia tu kwa kweli ilikuwa hatari. Ukizingatia pia sikuweza kuhudhuria mazishi kwa maana hiyo inakuwa vigumu sana kuamini. Mwaka huu mzima ulikuwa mwaka wa majonzi na mateso makubwa sana nilipungua/ kilo 10 hivi. Ila kwa maana nyingine nasi tulihudhuria mazishi yake. Tuliwaombe wapige picha (video) lakini hata hivyo sio sawa na kuwa pale. Kwa hiyo mpaka sasa kichwani/akilini mwangu mnaniambia mama bado yupo. Nimesahau kusema mama alitutoka trehe 17/8-04 saa mbili usiku hii siku ilikuwa si siku nzuri kwani pia binti yangu ilikuwa siku yake ya kwanza kuanza shule. Mama alizikwa 19/8-04

Mapema 2005 mwanzoni tukafunga safari kwenda nyumbani Tanzania. Ilikuwa taabu sana nilibadilika, sikutaka kutoka pale nyumbani kwenda mbali. Kama vile kusalimia marafiki Wino-Matetereka. Nilikuwa naogopa, nilikuwanamsubiri mama. Kwani ilionekena kama tu, ameondoka kidogo. Au yupo safarini. Nadhani maisha yangu hayatakuwa kama yalivyokuwa. Wakati mwingine siwezi kuamini eti mama hayupo. Wengi waliumia sana siku ile, ila kwa kuwa mbinafsi nataka kusema mimi niliumia zaidi. Naletewa habari mama hayupo, lakini siwezi kwenda kwenye mazishi pia wala kumwona mama yangu kwa mara ya mwishoyaani ile (BURIANI). Hii ndio maana siwezi/sitaki kuamini pia kusema hili neno marehemu. Kwa sababu kwa mimi mama yupo nami si marehemu.HILI SITASAHAU.

Thursday, March 5, 2009

SALAAM KUTOTKA SONGEA

Sikuweza kuacha kuchukua picha hii je? kweli tunafanya hivyo?

Tuesday, March 3, 2009

MWANAUME NA MWANAMKE MAHITAJI YAO.SEHEMU YA II

a) Usalama: Ndiyo hali ya kujisikia kuwa huna hofu yoyote au wasiwasi. Wakati ambapo hakuna kitu cha kutisha au cha kuvuruga akili. Najisikia salama hatari ikiwa mbali, maadui hawapo nami nimeshinda matatizo.
Yapo mambo mengi ambayo yanaweza kutuondolea usalama katika mioyo yetu. Ajali yaweza kutokea, vita, magonjwa yaweza kutupata; watu pia wanaweza kutudhuru, kuiba mali yetu na hata kuhatarisha maisha yetu. Hofu ipo ndani yetu kwa namna nyingi. Hofu ya mambo tusiyoyajua, hasa katika kutafuta kazi, au tukiwa ugenini, tubadilishapo mtindo wa maisha.

Ingawa yote hayo yapo, bado tunajua usalama. Kuna usalama wa mtoto kifuani kwa mama yake. Usalama wa mtoto ashikapo mkono wa baba yake. Usalama wa rafiki ambaye anajua kwamba kwa vyo vyote rafiki yake yuko tayari kumsaidia. Usalama wa mwanamke aliye na hakika juu ya mapendo ya mumewe. Usalama huu ndio msingi wa haja zetu na usalama unatakiwa hasa katika ndoa. Haja hiyo ya usalama ikitoshelezwa, amani kubwa na utulivu wa moyo hupatikana.

b)Kukubalika: Haja yetu ya pili yaitwa kukubalika. Ni haja ambayo wewe na mimi tunaijua sana. Ni ile hali ya kukubalika na watu kama tulivyo, kueleweka nao, kpokewa jinsi tulivyo na tunavyojitahidi kuwa. Kila mmoja wetu anahitaji sana mtu mwingine wa kumsindikiza, kufurahi na kuhuzunika pamoja naye. Mtu ambaye anajua matatizo na matakwa yetu; pia mwenye kuelewa tunayohofia.
Jaribu kufikiri kidogo maisha yangalikuwa ya namna gani kama hatingalikuwa na mtu ye yote wa kumkimbilia wakati wa shida, au mtu wa kutupongeza na kututia moyo.

Katika ndoa mwezi wako Mume/mke, anatazamia kupata hayo kutoka kwako. Mume wako ama mkeo anataka kuhakikishiwa kwamba kwa upande wako hatapata masharti yo yote ya kumkubali; hii ina maana kwamba unamkubali na kumpokea kwa furaha jinsi alivyo nawe unamjulisha jambo hili.

Hii haina maana kwamba huwezi kuona kasoro na udhaifu alio nao mwenzako. Maana yake ni kwamba unakuwa tayari kumwambia: “Najua ya kwamba wewe si mkamilifu, lakini nakupenda jinsi ulivyo, na pia nakubali ujue kuwa wala mimi si mtu mkamilifu. Hata hivyo nina hakika kuwa unanipenda”. Unapokuwepo ukubaliano wa namna hii kila mmoja huwa na imani kubwa na mwnziye na kujiamini pia.

c) Kuthaminika: Ndilo hitaji la tatu ndani mwetu. Je, tulieleweje hitaji hilo? Unaweza kupata mwanga kidogo juu ya jambo hili kama ukikumbuka jinsi unavyojisikia wakati umekwisha fanya kila juhudi na kujisumbua ili upate kumfurahisha mwingine. Halafu mtu huyu unayetaka kumfurahisha hajali wala hatambui kwamba umefanya kitu kwa ajili yake. Katika hali hii utajisikia kama umekosa kitu fulani, na kitu chenyewe ni kuthaminika.

d) Kujikamilisha binafsi: Hiki ndicho kilele cha mahitaji yote ya hisi. Ni ile hali ya kujisikia kitu cha maana. Kujisikia kwamba nimetumia vipaji vyangu vyote kikamilifu. Nimetumia nguvu zangu zote za mwili, akili na moyo, na kweli nimefaulu kuwafurahisha wengine. Kwa kufanya hivi najiona mtu zaidi.
Si lazima kufanya mambo makubwa. Kwa mwanamke yaweza kuwa kazi ya kudarizi au kuremba kwa ushanga, kupamba nyumba kwa namna ya pekee, kutengeneza nguo za watoto zitakazomletea sifa ya wengine. Kwa mwanamume yaweza kuwa kuchukua kozi kwa njia ya posta ili kupata kazi nzuri zaidi au mshahara mkubwa zaidi.

Katika kufanya mambo haya kila mmoja anahitaji mwenzake, mume au mke. Kwa sababu kule kujikamilisha binafsi, mara nyingi, huhitaji msaada wa mwenzio. Mapendo yake yatakudhihirishia vipaji fulani ambavyo hukuvijua kwanza, na mapendo haya haya yatakupa nguvu ya kuviendeleza. Kwa pamoja utaweza kujijenga. Kwa pamoja pia mtayatosheleza mahitaji haya yaliyomo ndani ya moyo wa kila mwanamume na kila mwanamke.

Mahitaji ya kiroho
Aina ya mwisho ya mahitaji ni yale ya kiroho. Je, nina maana gani kusema hivi? Ninataka kusema, kuhitaji kitu kilicho kikubwa zaidi kuliko vile vya kibinadamu. Ni kuhitaji heri iliyo kubwa zaidi ya ile ya kibinadamu, kuhitaji amani iliyo kuu kupita moyo wa binadamu, kuhitaji Mungu Mwenyewe.

Monday, March 2, 2009

JINSI YA KUPATA (TOAST) KUCHOMA MIKATE

Ukitaka kupata (toast) basi kazi ndio hii unahitaji jiko, mkaa na waya.

Sunday, March 1, 2009

DADI WITU

Hinu nyenye pemwisali, msala naha:-

Dadi witu,
Witama kunani kulihundi,
Lihina laku lihyuwanike,
Ubambu waku utibwerele,
Chewifuna wenga vakiti vandu,
pamlima apa ngati chevikia kunani kulihundi,
Utiletele lelu chakulya chitu cha magono goha,
Utiwusile getihokili,
ngati tete tukuwawonela lipyana vevahoki kwa tete.
Ukotoka kutileka kulemala nichihaki,
nambu utiwusile vihaki.

Ndava ubambu waveve na makakala na uvaha, magono gaha. Pepayi.