Saturday, March 7, 2009

SALAMU TOKA SONGEA TENA JE? NI KWELI?

Sidhani kama itawezekana kuacha kunywa ulanzi, hapa sitakubali kabisa kwani itakuwa wamekatisha starehe zote. Labda kuna anayekubaliana na ushauri huu.

7 comments:

Simon Kitururu said...

Kibao kinasema kweli ingawa nami bado sijafikia uamuzi wa kuacha Ulanzi!:-(

Story fupi....

Nakumbuka enzi hizo mimi na washikaji tulikuwa hatuna pesa za kutosha kununua bia hapo Morogoro, kwa hiyo tukaanza kununua gongo halafu tunaimix na fanta kuipa rangi kabla hatujaijaza kwenye chupa bomba za pombe tusizozijua za kichina au Kirusi ilikujifanya hatunywi gongo.

Matokeo ya kujaribu kudanganya wengine tunywacho sio gongo yalikuwa yanafikia kutudanganya sisi wenyewe kuhusu nguvu ya kilevi tunywacho. Unajua gongo inaweza kirahisi tu kuwa 70% au zaidi alcohol.

Basi mambo yaliyokuwa yakitokea baada yakujitibu unaweza usiamini. Wenye kuimba waliimba na rafiki yangu akaenda mpaka nyumbani kwa demu mmoja ambaye hawajawahi hata kuongea kuposa kwa wazazi.Wazazi waliokuwa wanajulikana kwa unoko mtaani!:-)

Kuna mengi yalikuwa yanatokea kiasi kwamba naamini kabisa kama kijiweni tungekuwa tunamiksi na akinadada walimbwende, nisingeshangaa kama watu wangeenda kuchovya nyuma ya migomba.

Mwisho wa hadithi!:-(

Pombe si chai lakini ingawa wengine hatuiachi!Na ningeshauri kwa yeyote ambaye hanywi na haihitaji asianze kuinywa kama inawezekana! :-(

Anonymous said...

Simon bora ulivyoondoka moro ama gongo ingekumaliza sasa hivi huko Sweden unakunwa kiutaratibu, kweli pombe si chai sijui na mimi nijaribu..!!??

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Chukua gongo yako na kainywee nyumbani - ukiwa na wako wa daima- dumu mpaka kufa...that way hata ukizembeka na kufanya uzembe unakuwa unazembekea kwako! Na kama hapo kwako bado hapajazembeka basi unakuwa bado hujazembeka.

Christian Bwaya said...

Masangu ni wangapi wanaweza kuinywea chumbani?

Hivi bila pombe kuna hasara yoyote?

Fadhy Mtanga said...

Ndashene wene uwulasi uwo avanu vasidoboha huuleha, ndipuliha wa winoga pa mlomo, numbula dza vanu dzikela swe!

Jamani nilipoona neno ulanzi nikadhani nipo kijijini kwetu Ilembula. Maana jioni baada ya kazi lazima tukutane kidogo tuugonge. Tamu ni siku za minada. Unauza fasta kisha unazama kwa ulanzi na nyamachoma. Baada ya hapo mabibi wawili watatu. Kondomu si rahisi kuikumbuka tena.
Ni hayo tu!

Anonymous said...

Bwana Bwaya - mimi pamoja na jamaa wachache ambao nawafahamu huinywea nyumbani! Pengine tumekaliwa ati!

Bila pombe hakuna hasara yo yote - na kuna vitu vingi tu ambavyo mtu ukiviacha hakuna hasara yo yote - sigara, madawa, nguo, ugali, NGONO...

Yasinta Ngonyani said...

Asanteni wote. Ni kweli kila kitu kina umuhimu wake,. Nakubaliana na wote si lazima kuvuta,kunywa pia ngono,lakini ugali mmh kweli itawezekana kuishi bila ugali ?

Fadhy Karibu sana kwani ulikuwa umepotea muda mrefu sana. Na naweza kukujibu kwa neno moja tu KAMWENE MTANI