Monday, March 30, 2009

UPENDO KWA NCHI YANGU +MAISHA

Sijui kama wenzangu mmewahi kujisikia hivi, mwenzenu leo nimeamuaka na kujiona ya kwamba:- Ninaringa kwa kuwa Mtanzania nchi yangu yenye sifa zote za ustaarabu.

Ninaringia rangi yangu nyeusi, macho meupe, ngozi yangu nyororo, ninapendeza na nywele zangu nyeusi na kiswahili ni lugha yangu.

Ninajivunia nchi yangu ya Tanzania yenye miji ya kuvutia iliyojengeka. Angalia Dar es salaam, Mwanza nayo Dodoma bila kusahau kwenye marashi mji wetu Zanzibar. Halafu ukienda Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa na Songea.

Mnajua kuna vivutio vingi ndani ya Tanzania vinavyotufanya sote tujivunie kwa mfano kuna bahari fahari ya Taifa, Ziwa nyasa, viktoria, Tanganyika pia mlima mkubwa barani afrika Kilimanjaro. Bila kusahau mbuga za wanyama Serengeti, Ngorongoro, Tarangire, Mikumi n.k.

8 comments:

Christian Bwaya said...

Yasinta, hongera kujivunia asili yako. Vyovyote iwavyo, katika hali yoyote, asili inabaki ilivyo.

Anayeitambua na kuikubali asili yake, amejielewa.

Koero Mkundi said...

Dada Ysinta.

Hongera kwa kujivunia Utanzania, kuna rafiki yangu mmoja tulikuwa tukisoma nae kule Morogoro, ni mmojawapo wa masuriama walioachwa na wale wakimbizi wa Afrika ya Kusini kule Mazimbu(Kwa asiyejua maana ya suriama, nitamsaidia, Suriama ni chotara)
Basi alikuwa anataka tumtambue kama Mzulu kutoka Afrika ya Kusini na sio Mtanzania, basi nilikuwa nabishana nae ile mbaya na kwa kuwa anajua kizulu cha kubabaisha duh! alikuwa anatuburuza ile mbaya.
Kuna haja ya kujivunia nchi yetu japokuwa ufisadi unatutia doa

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Safi kabisa dada Yasinta. Asiyejivunia asili yake na utamaduni wake hajielewi, au kama asemavyo Ngugi ameshakoma kuwako na au anaishi ili kuridhisha wengine. Ndiyo maana kidogo inatia wasiwasi tunapoona hiki kizazi cha dot com kinavyojibidisha kuiga "Ubritney Spears" na "Ufifty Cent" na kukana karibu kila kitu cha kiasili. Hakikisha kwamba uzalendo huu ulio nao unaurithisha kwa watoto wako. Badala ya kuwasomea hadithi za Kisikandinavia kabla hawajaenda kulala, waimbie "...Tanzania, Tanzania, ninakupenda kwa moyo wote..." natumaini hujausahau huu wimbo...

Yasinta Ngonyani said...

Bwaya kusema kweli naipenda sana nchi yangu na najivuna sana.

Ahsante pia Koero.

Matondo ahsante sana na huo wimbo wanauimba kila siku yaani bila shida na ndiyo sijasahau kabisa :ngoja nimalizie Tanzania Tanzania,
Nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania,
Jina lako ni tamu sana,
Nilalapo nakuota wewe,
Niamkapo ni heri mama wee,
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote.

Sophie said...

Yasinta, udumu!namna hii si tu kwamba unajielewa na kujithamini bali pia unapanda mbegu na msingi bora kwa watoto kwani watoto wanaokua wakijielewa watajivunia asili yao na kujiona wanakubalika katika jamii.Kazi nzuri dada na mfano wa kuigwa kwa wale ambao hawana mtizamo huu mzuri.

Anonymous said...

mwenga, Tanzania kwa bwina sana, naipenda sana Tanzania. Naipenda na kuimiss sana Songea, mhh, nikikumbuka dagaa wa ziwa nyasa, samaki mbelele toka mto Ruhuhu, mwe, mbona raha sana!! Mungu ibariki Tanzania.

Du, Koero huyo mzulu wenu nae kazi kweli kweli, mimi mwenyewe ni mzulu, nimezaliwa Tanzania na kukulia Tanzania na naipenda sana Tanzania japokuwa kizulu naongea.

ERNEST B. MAKULILO said...

SINA UPENDO NA TANZANIA

Mimi na mtazamo tofauti na upendo wa nchi yangu ya Tanzania.Binafsi siipendi Tanzania kama nchi japo ndio asili yangu, na itaendelea kuwa hivyo ni asili yangu daima.Ila nitaendelea kuwa nawapenda watu wa Tanzania kushirikiana nao daima.Ila kamwe siwezi kusema nina upendo wa dhati na Tanzania.

Mimi nifahamvyo siwezi kuwa mapenzini na mtu au kitu ambacho kinanitesa, kinanikera kila wakati.Kwa hali ilivyo Tanzania ya ukweli wa mambo, nchi kuwa personalised na watu wachache kuamua nichi iende vipi kwa maslahi yake, ufisadi uliopo wa kuwatesa raia wengi nchini, sera za nchi kuwa za kuwagandamiza watu wengi masikini, ubabe wa serikali dhidi ya wanafunzi wa vyuo, ubabe dhidi ya wafanyakazi wa East Africa na walimu nk inaumiza sana.Siwezi kuendelea na kuwa na upendo wa namna hii ambao unanitesa.

Ukiangalia mfano, baba yangu ni mmoja wa wazee wa iliyokua ile jumuiya ya Afrika Masharaiki, haki yake hadi leo ni kizungumkuti, lakini wabunge kila baada ya miaka mitano wanapewa kiinua mgongo cha zaidi ya milioni 30.Mfanyakazi wa serikali mwingine akifanya kazi miaka 30 kiinua mgongo chake hakizidi milioni 20,huo ni uonezi.Kama ukisoma dfetails alizotoa Dr.Slaa, kwa siku moja mbunge anapewa allowance ya kwenda "kusinzia" bungeni ya 350,000/= ambayo ni zaidi ya mshahara wa mwalimu wa high school (mwenye bachelor's degree) kwa mwezi mzima.Huo ni uonezi.Walimu waliojiriwa tangu mwaka jana (nami nilikuwemo, japo sikwenda) hawajapewa mshahara wake tangu mwaka jana Septemba hadi leo hii, watu hawa wanaishje??Eti ualimu ni wito??hahahah hakuna wito hapa, tuanze kusema basi ubunge nao ni wito tuondoe hayo maslahi tuone kama nao watakua wanakimbilia huko bungeni.

Ukija kwenye sekta ya elimu, tangu chekechea kila mtu atajijua kivyake kujigharamia hadi chuo kikuu.Mimi nimesoma kwa mfumo huu.Tangu lini baba anamkopesha mwanaye hela ya matumizi, hela ya matibabu, hela ya malazi nk?Kama baba anamkopesha mwanaye, maana yake ni kwamba mara baada ya huyo mtoto aliyekopeshwa kurudisha hela kwa baba yake, mkataba wa ubaba nao unaondoka tena.Hii ndio inapelekea watu kuingia ktk rushwa na kutoipenda nchi yao kwa namna nyingine kwani mtu tangu chekechea hadi chuo kikuu hajawahi kula matunda ya serikali yake.Hii ni tofauti na nchi nyingi za ughaibuni.Mfano ukiwa na mtoto wako marekani una uhakika anapata elimu bora ya shule ya msingi hadi high school bure.Hiyo imetulia kwangu.Nikimpeleka huko Norway ndio usiseme ni kusoma tu kupiga shule fresh.Unakuta mtoto anakua ana furaha na nchi yake, anaona jinsi nchi imtendeavyo vyema.Kwanini mtoto wangu nisije mzaa nchi hizi naye akala matunda ya kuwa mzawa wa nchi hizo??

Mimi mwaka jana wakati nataka kuja marekani kuanza kufundisha kupitia Fulbright program, tulipewa barua na mkataba rasmi toka ubalozi wa marekani.Hivyo ilinilazimu niwe na bendera ya taifa kwani nakuja kuliwakilisha taifa kupitia mkataba wa nchi mbili Marekani na Tanzania wa kielimu.Nilienda wizara ya mambo ya ndani nipate bendera ya taifa, walininyima kwakuwa mimi sio mtu nayeruhusiwa kuwa na bendera, wakasema niende wizara ya mambo ya elimu, nao walininyima wakasema hadi iwe kikundi cha watu NGO.Niliwauliza, mbona Miss Tanzania naye hupewa bendera ya taifa, je naye ni NGO au??Mbona tena huyo Miss Tanzania aendapo huko mashindanoni hatuwahi kuona hata mara moja kaibeba hiyo bendera?Mimi naenda kufundisha mwaka mzima kuhusu Tanzania, kwanini nisiwe nayo hiyo bendera?Mwishoni baada ya debate kubwa na kuwaonesha vielelezo vyote walisema niende kwenye ofisi ya waziri mkuu ndio ana ruhusa ya kunipa bendera hiyo.kwa elimu yangu ya sayansi ya siasa nilishangaa sana kusikia kuwa miongoni mwa kazi za waziri mkuu wa Tanzania ni kugawa vitambaa vya taifa (bendera ya taifa).Mtu mwingine alinidokeza niende Bohari kuu ya serikali kule zinapatikana.Nikaenda huko Bohari.Nikaulizia nikaambia ni kweli zinauzwa.Nikachagua za kununua.Ile natoa hela ninunue, inatakiwa iwe approved na bosi wao ununuzi huo, bosi wa pale akasema sina hadhi ya kununua bendera hiyo kwani naweza kuwa ni mvuta bangi wa kwenda kuidhalilisha bendera.Nikamuonesha barua ya Balozi wa marekani, Mr.Green kunitambulisha kama cultural ambassador and teaching assistant at Marshall University, nikamuonesha mkataba ni vitu gani nitakua nafunda huku mambo ya culture, nikamuonesha visa na tiketi, jamaa akogoma.Alichosema ni kwamba inabidi balozi wa marekani, Mark Green (kwa wakati huo) amuandikie barua huyo jamaa wa Bohari kuwa nahitaji bendera kwani kwenye barua imesema mimi ni cultural ambassador lakini haikusema nipewe bendera.Ilinishangaza sana wandugu.Nikamwambia unajua kuwa balozi wa marekani Tanzania ni rais wa Marekani nchini Tanzania?Akasema ndio anfahamu hilo.Nikamwambia kama unajua hilo, kamwe rais wa nchi iwe Tanzania au wa Marekani hawezi kukuandikia barua wewe direct, wewe hii barua inatoa taarifa mimi ni nani, maana yake inahitaji msaada wowote ule.Akisema aandike barua kwa kila mtu, itakua kituko sasa.Balozi atakua kazi yake ni uandishi wa barua na kuachana na kazi za ubalozi.Mwishoni nikanyimwa bendera hiyo.Nilichokifanya ni kucheza dili, mfanyakazi mmmoja akaiba bendera ya taifa ile kuwa akatoka nayo nje na nikamlipa shilingi elfu 10.

Sasa unaona tu upatikanaji wa bendera ya taifa, kitambaa tu ilinigharimu muda zaidi ya siku tano naenda mjini, na mwishoe nainunua kwa wizi.Je, mimi niipendee kitu gani hiyo nchi ya Tanzania??

Kupata passport ni kimbembe kingine.Wakati nchi za uarabuni mfano Oman, mtoto akizaliwa tu anapewa birth certificate na passport moja kwa moja.Na kifikisha miaka 21 anapewa state ID.Lakini kwa Tanzania kuwa na passport ni mpaka uoneshe documents zote za kwenda kuombea visa, kama ni shule uoneshe I-20, admission, nk.Huo wote ni upuuzi ambao hauna maana hata kidogo.Wangekuwa labda wanabana hivyo huku mtu labda ana utambulisho mwingine kama state ID nk kidogo ingeleta maana.Ni watanzania wangapi wenye passport?Maana watu wengi hawana birth certificate, na mtu hana passport, na nchi haina state ID (Ndio hizo zinazoanza kufanyiwa ufisadi wake), sasa hivi mtu ukifunguliwa kesi wewe sio raia utaonesha nyaraka gani kusema wewe ni raia?

Angalia maisha ya chuo kikuu.Tango mwaka 1994 mwanafunzi alikua anapewa 2500/= kwa siku hadi ilipofika 2006.Inamaanisha kuwa maisha yalikua hayapandi miaka yote hiyo?Inamaana kuwa mishahara ya watu ilikua haipandi miaka yote hiyo?Sasahivi ndio hiyo 5000/= kwa siku, ila fahamu mahitaji sasa ni makubwa mno kwa hela hiyo kutosha.Wanafunzi wanatakiwa kukata hela kiasi humo humo kulipia ada.Walipofanya mgomo, ni kufukuzwa na kulipishwa hela na chuo na serikali yenyewe.Nakumbuka pale UDSM mwaka 2007 kulikua na mgomo tulifukuzwa chuo, na kuambiwa ili kurudi lazima ulipe laki moja ya medical fee.Na ahadi ilikua kama tukisitisha mgomo basi hiyo laki moja tutapewa offer hatutolipa.Kumbe sasa ile ni adhabu.Kunyanyaswa vile bado tu niendelee kuipenda nchi hiyo???oooh no, siwezi kuwa na mpenzi anayenitesa, mwenye roho mbaya sana kiasi hicho.Na kamwe sitaki mtoto wangu aishi huko Tanzania kwani ili kuja kutoka na kuwa mtu ktk system ya kitanzania inatakiwa atokee ukoo bora, au koo fisadi flani.Ngoja tulee watoto huku ambapo juhudi za mtu zinalipa.

Ngoja niishie hapa.
Samahani kwa maelezo mengi sana.

MAKULILO Jr,
www.makulilo.blogspot.com
West Virginia, USA

NURU THE LIGHT said...

YASINTA YAANI U COULDNT HAVE SAID IT BETTER THAN MYSELF..mimi pia napenda sanaaaaaaaa nchi yangu and am proud japo kuwa nimechanganya lakini mama yangu alikuwa makini sanaa kunifunza asili na historia yangu..kaka hapo juu i feel you na ninakuelewa kabisa kwasabau ni vitu hivi mimi pia huwa vinanisikitisha sanaaaa...lakini like a person once said..no one is going to save africa but a black man or woman..its up to us to make a change na kuwa na upendo kwa nchi yako ndio mwanzo wa nyakati ya kubadilisha mabadiliko..