Monday, March 9, 2009

SHAMBA LANGU LA MAHINDI NA MIGOMBA RUHUWIKO SONGEA

Wote nadhani mnajua kuwa si muda mrefu nimerudi toka nyumbani TZ. Pia ule msimu nilikuwa kule ulikuwa ni msimo wa kilimo kwa huyo nami sikuwa nyuma nimelima shamba la mahindi kama muonanyo.

8 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Kumbe nawe umo Dada. Naona ukulima umependeza hapo. Pengine swali ni kwamba unatamani kurejea huko baada ya kulima kwa miezi miwili?
Unaonaje KAZI ya ukulima wa nyumbani?
Kuna changamoto gani unazoamini mkulima wa kawaida anayeendesha maisha yake kwa hilo anakumbana nayo?
Hongera

Yasinta Ngonyani said...

Mzee wa Changamoto: Hapo anzcha mchezo hazitakosekana gunia ishirini za mahindi.

Ukulima wa nyumbani ni kwamba ningependa kuwashauri wakulima waache kuchoma moto waozeshe. Na pia wajaribu kupanda MAREJEA. Na kuhusu maisha kama mkulima kwa kweli ngumu. mwisho nasema ahsante kwa kunihongeresha.

Christian Bwaya said...

Hongera kwa kilimo kinachosingiziwa hadhi ya uti wa mgongo. Shamba linapendeza.

PASSION4FASHION.TZ said...

Hongera sana bidada kweli ukulima wewe unauweza, shamba lako ni zuri sana na kila ulicho otesha naona kimestawi vizuri,asante kwa kutu onyesha mfano ngoja nasie tujipange.

Bwaya hujakosea kabisa ni kweli kilimo kimekuwa kikisingiziwa eti ndio uti wa mgongo,hata mimi siamini kama kweli ndio uti wa mgongo,nibora wangesema ufisadi ndio uti wa mgongo wa Tz hapo watu wataelewa somo.

Anonymous said...

Mgunda wako wa bwina. Mwezi Juni ne nihamba kumala malombi gaku goha.
Just kidding. Salamu kwa mngwana vaku na vana.
Kakako.

Anonymous said...

He, nakakosiwi.
Ne na Ngonyani
Kakako.

nyahbingi worrior. said...

samahani fungua kurasa ya kuchangia mawazo kuhusu jumuiya ya wanablogu tanzania.

http://blogutanzania.blogspot.com/

www.ringojr.wordpress.com

Yasinta Ngonyani said...

We usiye na jina unayedai ni Ngonyani pia na ni kakangu. Kwa nini usisema jina lako kwani nina kaka wengi sanaaaa.