Tuesday, March 24, 2009

MILA NA DESTURI/JE? KUTAHIRI WASICHANA NI HAKI?

Ni jambo la kutatanisha kidogo kwangu: Labda nianze hivi katika Tanzania tupo makabila tofauti. Na ni mengi na kila moja lina mila na desturi zake. Makabila 129 (130). Kwa hiyo hapa ninachotaka kusema ni kwamba hili jambo la kutahiri wasichana hasa wenzetu wamasai (pia nchi yenzetu jirani Somalia) lina maana gani? Kwa sababu wao wanadai wakishawatahiri ndo wanakuwa wanawake kamili na pia wanakuwa safi. Lakini papo hapo hawajui kama ni hatari sana :-

Tukianza na vyombo wanavyotumia, Je? Ni visafi au je wanabadili kwa kila mtoto hapana. Halafu kubwa zaidi je wanawapa ganzi? Hapana. Kwa sababu baada ya hapo inasemekana wanawashona na kuacha shimo ndogo sana kwa ajili ya kukojoa mkojo tu.

Je? Huyu msichana atapoolewa mnafikiri atapata maumivu kiasi gani wakati anatarajia kufanya tendo la ndoa kama sio mateso makali. Ambayo badala ya kuifurahia ndoa yake inakuwa kuijutia. Na itakuaje atapotarajia kuzaa. Kwa kweli na mateso makubwa sana atayapata. Ambayo atatamani hata asingeishi.

Kwa nini? Na je? ni safi kwa nani?. Kwa sababu msichana wa miaka mitano hawazi kuelewa ni nini kuwa mwanamke.
Na watoto wengi wamepoteza maisha yao wakati wa tendo hili, wengine wanapata tetanus, wengine wanapata mshtuko pia maambukizo mbalimbali. Tukiendelea hivi tutamaliza wasichana!!.

5 comments:

boniphace said...

This is very interesting blog, thanks for passing through my home and I wish to be visiting this home of yours for a long time to come.

Yasinta Ngonyani said...

Asante sana! Boniphace kwa kunitembelea na karibu sana tena na tena

Rama Msangi said...

jambo moja ambalo daima nimekuwa naamini ni kuwa, hapo kale, kila kilichokuwa kikianzishwa, kililenga katika kuleta tija zaidi kuliko kuleta madhara. tatizo pekee ni kuwa, katika zama hizi, mambo mengi ya zamani yanaonekana kuwa hayafai, sio kwakuwa hayafai, bali kwakuwa yanafanyika katika mtindo, taratibu, mfumo, au namna iliyopitwa na wakati.

Mijadala mingi sana imekuwa ikilenga katika kukemea mila hii, kuwakaripia sana wazee wanaoiendeleza au kuiendekeza tuseme. Lakini, hivi ni nani ambaye amewahi kukaa na wazee wa zamani sana wale wenye kujua maana na asili ya mambo ya kale kuwa yalianza kwasababu gani na akajua kwanini ukeketaji ulianza?

Na hapa nazungumzia wale wazee wa kizamani sana wenye kujua asili yao, sio hawa wazee wetu wa kisasa, ambao nawezawaita wazee pori, ambao nao historia wameipata kupitia kuisoma kabla ya kuanza kutupotosha.

Pengine atusaidie mtu, katika hili, asake kikongwe mmoja akae naye amweleze kwa kinaga ubaga kuwa chanzo hasa kilikuwa nini, kisha tuone, huenda manufaa yalikuwa mengi zaidi kuliko hasara, halafu tukiona hivyo, basi tuendeleze mila lakini katika taratibu za kisasa za kisayansi...za ganzi, sijui ushonaji nk.

nitarejea tena, kwanza ngoja nisikie wadau wengine wanasemaje

Evarist Chahali said...

Ukeketaji sio tendo zuri.Lakini naomba niepuke kuzungumzia uzuri au ubaya wake bali niangalie kwa kifupi suala zima la baadhi ya mila na desturi zetu.

Ukeketaji, "chagulaga",kaka/mdogo kurithi mke wa marehemu kaka/mdogo wake,nk ni baadhi ya mila ambazo mara kadhaa zimeibua madai kama mila hizo "zimepitwa na wakati","ni za kinyanyasaji","zinachangia maambukizi ya ukimwi",nk.Kitaaluma hayo yana uzito hasa kwa vile yanaambatana na ushahidi wa tafiti mbalimbali.Lakini "taaluma"au "tafiti" ni mambo ya "usasa" (sijui ndio neno sahihi la kiswahili kwa "modernity"?) ambao kwa mtizamo (na pengine imani) ya wanaopigania kuenzi mila,desturi na tamaduni zetu ni tishio linalohitaji mapambano makubwa.

Nisingependa kutetea au kupinga mtazamo wowote i.e. "usasa" au "ukale" bali pengine swali la muhimu linaweza kuwa kwenye muingiliano wa maeneo haya mawili in a way that hakutakuwa na hisia za msigishano bali maendelea kwa manufaa ya pande zote.

Pengine pia ni muhimu kwa "mawakala wa usasa" kufanyia kazi hisia za "watetezi wa ukale" kwamba chanzo kikuu cha mgongano sio ukweli au uongo wa yanayohubiriwa na "usasa" bali namna mahubiri hayo yanavyotolewa...kwamba mara nyingi "ukale" huangaliwa na prejudice (maneno kama mila "POTOFU",za "KISHENZI",nk...lugha iliyotumika wakati wakoloni wanaingia kwenye jamii zetu).

Lakini pia kuna tatizo la authority katika labelling kipi ni sahihi na kipi si sahihi.Na hli ni tatizo zaidi katika jamii zinazoenzi "ukale" ambapo mara nyingi mitizamo huwa umeelemea kwenye umoja (unilateral) wa makubaliano pasipo fursa ya kutosha ya kuhoji.Hilo ni tofauti na kwenye "usasa" ambapo,kwa mfano, kanuni (theories) zinaungwa mkono,zinapingwa au kuboreshwa,na hivyo kutoa fursa ya kuhoji au kusapoti mitizamo ya aina flani.

Naomba nihitimishe kwa kushauri kuwa nafasi ya mabadiliko katika baadhi ya mila "potofu" itafanikiwa tu iwapo mila hizo zitakuwa aproached kama za watu wenye akili timamu na utashi wa maamuzi yao kwa manufaa ya jamii yao na hivyo kuepusha hisia za prejudice na hatimaye kuleta muingiliano wa "kirafiki" badala ya "confrontational" kama ilivyozoeleka.

NB: Maneno "usasa" na "ukale" yametumika tu kuwakilisha "modernity" na "traditional",respectively na hayalenga kukuza/kushusha au kutukuza/kubeza mila yoyote.

NURU THE LIGHT said...

Yaani hii kitu mimi yasinta sikubaliliana nayo kabisaaa.huwa roho inaniuma kwasababu hawajui wanavyotuumiza sisi wasichana kwa kitendo hicho na ni kitu kinatuefect maisha yetu yote..ahsante kwa kuandika juu ya hili swali