Monday, March 23, 2009

KUJIFUNZA KUPIKA UGALI+KUJITEGEMEA+KUMSAIDIA MAMA



Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Hapo mnaona jinsi anavyojitahidi kuusonga huo ugali ni mara yake ya kwanza. Jinsi ya kujitegemea hapo baadaye haitakuwa vigumu.

12 comments:

Fadhy Mtanga said...

mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
safi sana nami nimeona. hup ugali ukishaiva nistue nije nifinye maana nna ubao.
mtani kamwene!

PASSION4FASHION.TZ said...

Safi sana!!!umenikumbusha mbali enzi hizo nyumbani kwetu,ilikuwa ni zamu ya kupika na kuosha vyombo kwa wote,kinadada na kinakaka hiyo inasaidia sana usawa kwa wote.

Huyo hata akija kuoa mke atapata raha sana watasaidiana kwa kila kitu.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

"Huyo hata akija kuoa mke atapata raha sana watasaidiana kwa kila kitu"

PASSION4FASHION.TZ, una uhakika kaka zako, mbali na kuwa na zamu za kupika na kuosha vyombo walipokuwa wadogo, bado wanafanya hivyo mpaka leo? Mwanaume wa Kisukuma/Kiswahili/Kiafrika apike na kuosha vyombo achekwe? Atasemwa kwamba amekaliwa a.k.a. amelishwa limbwata. Mimi nadhani mazingira na utamaduni ndivyo vinashinda hapa - kama mtu unaishi katika mfumo dume basi unasita kufanya kazi za "kike" kama kuosha vyombo na kupika hata kama ulikuwa na zamu utotoni. Kama unaishi katika utamaduni usiojali mambo haya basi utayafanya hata kama hukufundishwa wala kuyafanya utotoni. Kwa sisi tulioko huku ughaibuni ambako maisha ni ya mchakamchaka - na wafanyakazi wa ndani ni ghali sana- kuosha vyombo, kupika, kusafisha nyumba n.k. ni mambo ya kawaida - hata kama hatukufundishwa nyumbani. Pengine mtoto umleavyo sivyo akuavyo ati!

Koero Mkundi said...

hata miye napenda sana ugali dada Yasinta.
Umenikumbusha Mbali sana

Yasinta Ngonyani said...

Eeehh!! Mtani kamwene be!
Karibu tena. ulikuwa umepotea kama shilingi ya mkoloni. Ooh! ugali ushaiva karibu tujumuike.

Passion4pashion.tz nami ktk familia yangu tulikuwa tukifanya hivyo pia.

Kaka matondo, asante, na kuhusu akina kaka kusaidia kazi za nyumbani ni kweli inatokana na familia. Binafsi mpaka leo kaka zangu wananipikia ugali na kuosha vyombo pia kusafisha nyumba.

Koero, Karibu sana tena ni ugali na maharage ndio ulioandaliwa kwani kijana wangu ni mpenzi sana wa maharage.

Subi Nukta said...

Kumbe yanayofanyika kwenye nyumba zetu si ya kwetu peke yetu, hata ninyi kumbe mnafanya hivyo? safi sana. Afadhali wajifunze ili baadaye wakati wa uhitaji wasione jambo geni. Zamu hizo zipo sana, ndugu yangu wa kiume alifahamu kukamua maziwa ya ng'ombe kabla yangu na kupika keki kabla yangu vile vile, ulikuwa ni ushindani hapo umri wetu miaka 14 - 16!

Anonymous said...

Wengine husema samaki mkunje angali mbichi.Hata sisi nyumbani tulilelewa katika utaratibu huo wa kufundishwa kazi zote za nyumbani,kuanzia kupika, kuosha vyombo, kufagia uwanja na nyumba, kudeki na nyinginezo nyingi.
Kwa hilo wazazi walijitahidi.

Yasinta Ngonyani said...

Yah Subi, najitahidi angalao wajue vikazi vidogovidogo pia tamaduni zetu.

Nuru karibu sana kijiweni pangu. Na nimefurahi tupo pamoja. Ni kweli samaki mkunje angali mbichi.

PASSION4FASHION.TZ said...

Kaka Matondo, haya mambo yapo sana inategemea na familia unayotoka mimi kaka zangu wote hakuna wasichojua kupika,na kazi zote za ndani tuwalizifanya pamoja bila kujali mwamamke au mwanaume ni wote.

Sasa kati yao mmoja alioa mke bahati mbaya hajui kupika na amezaliwa Tz na amekulia Tz lakini kupika yeye kulimpiga chenga ni kaka yangu ndio kamfundisha wala sio siri wifi yangu mwenyewe anasema wazi kabisa yeye kupika kafundishwa na mume wake,sasa mtu kama huyo huwezi kumlaumu inategemea na malezi aliyokulia.

Kwakweli mnapokuwa wadogo mnakuwa hamuelewi ila mkisha kuwa wakubwa, ndio mnajua faida zake,na tangu tumekuwa wakubwa na kila mtu na maisha yake ni mara moja tuu ndio tulikutana wote nyumbani kwa pamoja kuanzia mtoto wakwanza mpaka wa mwisho na tulikumbushia hiyo ilikuwa kipindi cha pasaka,siku ya pasaka walipika wanaume na siku ya j'3 ya pasaka tulipika sisi wanawake, ilikuwa raha sana na sizani kama itakuja a kutokea tena kukutana kwa pamoja,kwa furaha kama ile sio rahisi maana baba tayari hayupo tena.

Kwa wengine mambo kama hayo ni mageni wanajifunza pindi wanakuwa nchi za nje maana hawawezi kumudu gharama za kulipa mfanyakazi wa ndani inakuwa mageni kwao.

John Mwaipopo said...

Mie ni kinyume kidogo. Nilibahatika kuwa mvulana peke yangu halafu first born. Nilikuwa 'mdebwedo' tu. Ila cha ajabu i have mastered the so-called women's chores, Usipime. Nimejifunza mwenyewe tu. Leo nguo safi zaidi ni ile iliyofuliwa na mimi, Nguo iliyonyooshwa maridadi ni ile iliyonyooshwa na mimi, chakula kitamu ni kile kilichopikwa na mimi (ndivyo ninavyoamini).

Yasinta Ngonyani said...

Hongera kaka mwaipopo. Maisha ni kujifunza

NURU THE LIGHT said...

hii safi sana yasinta....