Namshukuru babangu kwa kutunza kitabu hiki leo nimefurahi sana nadhani hata wenzangu mtafurahi pia kukumbuka hadithi hii:-
Bwana Matata yupo mjini, anauliza uliza njia ya hospital. Kuna kibao hapo njiani, lakini haui kusoma kibao.Bwana Matata anaona aibu kuuliza njia tena, anaona aibu kwa sababu hajui kusoma. Sasa anafuata njia ya bomani
Bwana Matata amechoka sana. Amechoka na safari, pia amechoka kuuliza uliza njia. Amelala kwenye kibao, kibao kinasema HATARI. Lakini Bwana Matata hajui kusoma, tena amechoka mno. Amelala njiani kwenye kibao
Bwana Polisi anapita, anamwona Bwana Matata amelala kwenye kibao. Bwana polisi anamwita, mzee vipi? Kwa nini unalala hapa? Huoni kibao? Lakini Bwana matata amechoka sana amelele kama gogo. Polisi amawita tena, kwa nini unalala hapa kama gogo? Kuna hatari hapa. Lakini bwana matata hana habari ya hatari hajui kusoma.
Bwana Matata akaamka, akasimama na kumwambia polisi, nataka kwenda hospitali. Mtoto wangu yupo hospitali ni mgonjwa sana, lakini nimepotea njia. Bwana polisi akasema, umepotea njia? Fuata hii Bwana Matata akafuata njia ile. Kinachoendelea naadhani mnajua
10 comments:
Yasinta, asante kwa kumbukumbu murua. Jumuisho lake: Ujinga ni Mzigo!
Oh! kaka Ansbert karibu tena. Ni kweli ujinga ni mzigo. Nakumbuka wimbo mmoja uumbwao kujua kusoma naona furaha.
AISEE ELIMU NI KITU MUHIMU SANAA..IN LIFE KUNA SHULE ZA AINA MBILI MOJA ILE AMBAYO UNAJIFUNZA HESABU NA ABC NA ILE NYENGINE NI MAISHA...WE NEED BOTH
BY THE WAY YASINTA TUNIKAN KAN DU HITTA PÅ GINA TRICOT OM DU BOR I STOCKHOLM MEN JAG TROR ATT DE HAR EN HEMSIDAN OXÅ..kolla upp det,,kram
Ni kweli elimu ni muhimu katika maisha. Tack så mycket, jag bor i Karlstad men det finns Gina tricot. Jag ska kolla Kram tillbaka
Dada Yasinta,
Hiyo lugha muliyowasiliana na Nuru naomba na mimi nikiri kuwa nimekuwa bwana Matata.
DUH!!!!!!!!!!!!!!!!
Hata mimi umenikumbusha mbali. Mwalimu Nyerere alifanikiwa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza duniani kwa idadi ya watu wanaojua kusoma na kuandika. Sijui sasa tuko wapi. Hizo hadithi za Bwana Matata na Tumbo niache nimwachie Manenge zilikuwa zinafurahisha sana.
Dada Yasinta,
Nami nimepita hapa kukujulia hali.
Bwana Matata alipata mtoto bila kujua kusoma!
Hivi ukijua kusoma huwezi kuogopa kupata mtoto ambaye unaweza kushindwa kumsomesha ajue kusoma?
Hapana Shabani sio umekuwa bwana matata. Kwani wewe umegundua ni lugha nyingine kwa hiyo unaweza kusoma ila labda hujaelewa.
Masangu nashukuru kama umekumbuka mbali.
Evarist Asante sana kwa kunijalia hali karibu tena na tena.
Simon:-( kupata mtoto huhitaji kujua kusoma na kama hata hujui kusoma si kwamba mtoto naye hatajua kusoma.
Kadiri miaka inavyosonga mbele, si tu kwamba wajinga wanaongezeka, lakini hata wale wanaopata hiyo inayoitwa elimu, nao wanajikuta hawana tofauti ya msingi wa wale wasiojua kusoma.
Yote haya zao la siasa za kishamba za kutwa kujiandaa na uchaguzi unaofuata.
Post a Comment