Thursday, November 28, 2013

MWANAMTINDO WA LEO NA MTOKO WA NYEUSI ....BLACK IS GOOD !!!!

 Hivi ndivyo lilivyokuwa vazi langu leo koti ndefu nyeusi na suruali vimenunuliwa UNIQUE,blauzi/line toka Vila clothes.
 Hapa mdada anaonekana kuwa mbali kweli kimawazo.....
 ....hapa anawaza sijui nibadili kazi na kuwa mwana mtindo....anaendelea kufikiri
Na mwisho inaonekana hajapata jibu bado kwa hiyo anaendelea kufikiri. Je wasomaji mnaonanaje  kuhusu hili na kuhusu vazi la leo?....NAWATAKIENI WOTE KAMA ILIVYO HAPO ULIPO IKIWA ASUBUHI, MCHANA, ALASIRI, JIONI AU USIKU..BINAFSI NI JIONI HAPA NA NAANZA KUJIANDAA KUPIKA MLO WA JIONI.

MAISHA YA NDOA:- NIMEULIZWA SWALI HILI NA RAFIKI/MFANYAKAZI MWENZANGU!!!!

AKIWA MAWAZONI
Habari za leo Yasinta, ni siku nyingi hatujaonana. U- hali gani? Vipi familia ni wazima wa afya?  Nikamjibu, salama tu na familia wote wazima. Sijui wewe na familia yako? Akaguna...mmmhhh! Sina uhakika, sijisikii vizuri niko katika mawazo mengi. Sijisikii raha kabisa kuwa na mume wangu. Lakini ni ajabu kwa kuwa huwa hawi nyumbani muda wote. Anafanyia kazi zake mbali kidogo anaweza akawa hayupo nasi wiki moja au mbili. Kwa hiyo ilibidi nimfurahie/tufurahiane arudipo lakini ni kinyume. Yasinta, mimi bado kijana..38 na yeye 35, nipo njia panda, sifurahii maisha niliyo nayo. Pia mwenzangu naye haonyeshi kama ananijali.  Nifanye nini? Nisaidie?
Duh! Hapo Kapulya akabaki hoi maana ushauri wangu.....si wa kiataalamu wa mambo ya ndoa. Nikakumbuka Maisha na Mafanikio, kuwa nikiweka hapa kwa pamoja tutaweza kumsaidia rafiki yangu. Na ndio maana nawaombeni tujadili kwa pamoja.  Kwani kesho laweza kukupata wewe au mimi au yule n.k. Nawatakieni kila la kheri na mjadala mwema. SIKU IWE NJEMA......Kapulya

Tuesday, November 26, 2013

TULIO WENGI TUNAKUMBUKA HIKI NI NINI!!!

Lakini wengi nadhani tunakumbuka vya matete...ni vihesabio/kalukuleta za zamani hizo. Hicho ni kihesabio cha dada Camilla wakati akiwa Mdunduwalo/Ndirima shule ya msingi na ni baba yangu katengeneza. Ametengeneza kwa visoda. Je? wewe umewahi kutumia vihesabio vya aina hii?

Monday, November 25, 2013

TUANZA JUMATATU HII NA SWALI HILI KUTOKA KWA KAKA BWAYA ...KUHUSU MAISHA NA FURAHA!!!

Kama mnakumbuka mwezi uliopita niliweka picha hii hapa kibarazani na baadaye kulitokea na maoni. Na baadhi ya maoni aliyotoa msomaji mmoja ambaye ni kaka Bwaya ambaye alikuwa ameadimika kwa muda mrefu na sasa yupo nasi tena. Nachukua nafasi hii kumkaribisha Kaka Bwaya......Haya na maoni yenyewe yalisomeka hivi;-
Bwayasaid...
Tafiti zinaonyesha kuwa watu waishio katika maisha yanayoonekana kuwa duni, ndio wenye furaha zaidi. Mfano ni hawa. Swali: kwa nini? Naomba tusaidiane kujadili swali hili kwa pamoja....JUMATATU NJEMA!!!

Sunday, November 24, 2013

HIVI NDIYO ULIVYOKUWA MLO WA ASUBUHI YA JUMAPILI YA LEO /CHAPATI KWA CHAI!!

 Chapati zinasukumwa huku chai ikiandaliwa
 chapati zinakaangwa
 chapati tayari kwa kuliwa
Na hivi ndivyo meza ilivyoandaliwa Jumapili hii ya leo. Chapati bado zipo na chai pia karibuni kujumuika nasi. NAWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA JUMAPILI YENYE BARAKA NA UPENDO. MWENYEZI MUNGU NA AWE NANYI. AMINA......KAPULYA/KADALA.

Friday, November 22, 2013

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA HAPO KALE UJAMAA, UMOJA, USHIRIKIANO NA UNDUGU !!!

 
Lakini leo /sasa kila mtu na chake. Hakuna tena ule umoja wa kunywa pamoja, kula pamoja na kusali pamoja. Je? kwa nini umoja wetu umepotea?----Nawatakieni wote Ijumaa njema ila usiwe ugimbi/ ulanzi/ pombe...mwingi/nyingi ,,Lol

Thursday, November 21, 2013

NIMEONA TUBAKI MKOANI RUVUMA:-TATIZO LA UMEME SONGEA KITENDAWILI!!!

Katika pitapita nimekutana na habari hii ambayo imenikasirisha na kunikatisha tamaa sana maana nilikuwa katika harakati ya kuingiza umeme katika nyumba yangu. Ila najipa moyo na kuendelea ebu soma hapa habari hii iliyoandikwa Na Albano Midelo.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
 












 


 
 
 
Hapa ni baadhi ya vijana katika mji wa Songea wakifanya maandamano ya amani kudai umeme wa uhakika mjini Songea.
 
“TANESCO wanakata na kurudisha umeme bila taarifa na hata ratiba ya mgao haijulikani hali inasababisha hasara kubwa kwa wananchi ikiwemo kuungua vifaa vya umeme na vyakula vinavyohifadhiwa kwenye majokofu kuharibika’’,anasema diwani wa kata ya mjini manispaa ya Songea Joseph Fuime.
Fuime alidai kuwa tatizo la umeme Songea haliwezi kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa kuendelea kutumia mashine chakavu za kufua umeme ambazo vipuri vyake vinaharibika mara kwa mara badala yake alishauri serikali kuunganisha mkoa wa Ruvuma na umeme wa giridi ya Taifa.
“Serikali iliahidi mara baada ya kuanza kuchimbwa makaa ya mawe ya Ngaka wilayani Mbinga kutajengwa kinu cha kufua umeme katika mji wa Songea hata hivyo tangu mwekezaji ameanza kuchimba makaa ya mawe hadi sasa hakuna dalili za kufungwa kinu hicho pia mwekezaji ameshindwa hata kuwalipa fidia wananchi wanaoishi katika eneo la mgodi’’,alidai Fuime ambaye pia ni katibu wa CHADEMA mkoa wa Ruvuma.
Uchunguzi uliofanywa katika maeneo mengi ya mji wa Songea umebaini kuwa vibaka wakati wa usiku wameongezeka na kusababisha nyumba nyingi kukatwa nyanya za madirishani na wengine kuibiwa vitu mbalimbali zikiwemo simu za mikononi,mavazi,kompyuta za mkononi na samani mbalimbali.
Waandishi wanakwama kutuma habari zao kwa haraka na hata vituo vya matangazo vilivyopo mjini Songea vikiwemo Redio Maria,radio Jogoo,TBC Taifa, vinashindwa kurusha matangazo kwa wananchi kutokana na kukatika kwa umeme mara kwa mara.
John Mapunda mfanyabiashara soko kuu la Songea anasema Kukatika kwa umeme na kuwaka bila taarifa katika mji wa Songea kunawasababishia hasara kubwa wafanya biashara wa vyakula hasa wanaouza samaki wabichi kutoka ziwa Viktoria, Tanganyika, Nyasa na bwawa la Mtera ,wao wanatunza samaki hao katika makojofu ambayo yanatumia umeme wa TANESCO hivyo samaki wengi wanaoza.
"TANESCO katika manispaa ya Songea inaonyesha dhahiri kuwa mashine zao haziwezi kufua umeme wa kukidhi hata katika mji wa Songea,wananchi tunahoji kwanini umeme huo umesambazwa hadi mji mdogo wa Peramiho badala ya kusubiri umeme gridi ya Taifa’’,alihoji Mapunda. Frank Mbunda mkazi wa Mahenge mjini Songea anadai kuwa TANESCO wameshindwa kumaliza tatizo sugu la umeme ambalo linachangia umasikini kwa wakazi wa Songea ambao wanashindwa kufanyakazi zao za kiuchumi.
Mwanaharakati Mohamed Kudeka mkazi wa Songea anatoa wito kwa serikali kuachana na umeme wa majenereta ambao matatizo yake ya kuharibika kwa vipuri yamekuwa yanajirudiarudia na kusababisha kero kubwa kwa wakazi wa mji wa Songea ambao wanashindwa kufanya kazi za kiuchumi na kusababisha umaskini.
“Mchawi ni ugonjwa wa majenereta ambayo vipuli vyake vimechoka na kuchakaa,tumechoka na kero hii kama sio ubovu wa vipuri utasikia mafuta ya kuendeshea mitambo yamekwisha,mara fundi wa kufunga vipuri anatoka nje ya nchi TANESCO tuambieni ukweli tumechoka’,anasisitiza.
Brighton Mwandata mmiliki wa studio ya kurekodi muziki Matarawe mjini Songea anasema umeme katika mji wa Songea haujapatiwa ufumbuzi wa kudumu anashindwa kurekodi kutokana na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara wakati mwingine inamgharimu kukodisha jenereta kwa gharama kubwa. Ingia hapa kwa kusoma zaidi habari hii.

Tuesday, November 19, 2013

AKINA MAMA WAPO KIWANDANI KUCHAMBUA KOROSHO HUKO TUNDURU MKOANI RUVUMA!!!

Hapa ni baadhi ya akina mama wakichambua Korosho kwenye moja ya kiwanda wilayani Tunduru mkoani Ruvuma......Nimekumbuka mbali sana wakati naishi Litumbandyósi na Kingole kuilikuwa/kuna Korosho nyingi sana. Basi mimi na kaka zangu tulikuwa tukizishughulikia hizo wewe acha tu, yaani mpaka mikono pia vidole vilikuwa vinachubuka maana Korosho zina mafuta fulani hivi yaliyosababisha iwe hivyo. Ila kwa kweli ilikuwa raha sana....picha hii nimeitoa kwa mdogo wangu Ester Ulaya.

Monday, November 18, 2013

HABARI NJEMA:- NI KWAMBA LEO NIMEPATA UNGA WA MAHINDI:- LEO MLO UGALI NA MBOGAMBOGA:-)!!!

Habari za wikiendi ndugu zanguni...kama mnakumbuka vizuri niliwaambia kuwa niliishiwa unga wa ugali. Sasa katika kutafuta tafuta nimepata kama muonavyo katika picha. Unga ni mweupe kama wa mahindi ya nyumbani. Huu unatoka Venusuela...Haya sasa karibuni kula ugali:-) NAWATAKIENI WOTE MWANZO MWEMA WA JUMATATU!!!

Saturday, November 16, 2013

JUMAMOSI :- MAISHA YANA MITIHANI YAKE!!

Ukiwa MTEMBEZI utafaidi mengi ..jana nilitembela hapa na nikakutana na wazo hili ambalo nimelipenda sana na nikaona kwa nini lisiwekwe hapa Maisha na Mafanikio ..Haya karibu!!
 
WAZO LA LEO: Maisha yana mitihani yake, ukiona kwako ni kugumu, ujue kuwa kuna wenzako kwao ni kugumu mara mbili yako, ukipatwa na mitihani ka hiyo...usikate tamaa, pambana, ukijua kuwa wewe sio wa kwanza kupata mitihani kama hiyo, wapo waliopata mitihani hiyo na wakaishinda, kwanini wewe usiweze...kumbuka baada ya dhiki, mara nyingi ni faraja.
BONGE LA WAZO ....JUMAMOSI NJEMA SANA

Friday, November 15, 2013

HAYA NI MAPISHI YA IJUMAA YA LEO KUKU.....KARIBUNI

Ijumaa ya leo itakuwa kuku ambayo ni:- kuku mzima, viazi, karoti, kitunguu, kitunguu saumu, tangawizi, nyanya kopo, binzari, mafuta, chumvi na maji..... Picha zaidi zinakuja baada ya muda tu....Kwa hiyo mnakaribishwa kujumuika nasi.

Na hapo ndivyo ilivyoonekana sahani yangu...wali, kuku, kiazi, karoti na mboga majani /figili ambayo imeliwa na mikono yangu mwenyewe......Karibuni chakula kipo kingiiiii kweli. Jioni njema sana na panapo majaliwa tutaonana tena kesho.

NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA NA IJUMAA IWE NJEMA KWA WOTE..


IJUMAA NJEMA KWA WOTE...KAPULYA...KADALA ...

Tuesday, November 12, 2013

NIMETAMANI JIONI HII NILE/NIPIKE UGALI ILA SINA UNGA NA NDIPO NILIPOKUMBUKA MAISHA YA UTOTONI!!

Mmmmmhhh!! Mwenzenu nimeka hapa nikiwa na mawazo kibao ....maisha haya hakika nimekumbuka mno ...UGALI WA MUHOGO na samaki halafu ukiongezea na matembele au kisamvu....basi tu . Sasa leo kisa cha kukumbuka hili ni kwamba ninajiuliza nipike nini maana nilitaka kupika ugali lakini sasa UNGA sina na kama mnakumbuka nililima bustani na niliweka akiba sasa unga sina  nipo hoi hapa. Mboga ipo  ila sina unga. Basi mawazo yakaja na kukumbuka wakati nilipokuwa KADALA kama huyo binti kutwanga na kuchekecha na mwisho mtu unakuwa unga tu mwili mzima...JE KUNA ANAYEKUMBUKA KAMA KAPULYA HAPA?

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMECHAGUA NGOMA HII IKIWA IMECHEZWA NA "ZAMBIA NGONI" IMENIKUMBUSHA LIZOMBE.....NGOMA YA ASILI


Msione kimya nipo  niseme tu nilikuwa nimebanwa  ila sasa nipo. Napenda kuwatakieni wote kila la kheri.Kapulya

Friday, November 8, 2013

SARESARE MAUA....IJUMAA NJEMA KWA WOTE

 Nimependa sana vazi hili
Kwa hiyo katika pita pita kwenye maduka nikaona hii blauzi(tunika) nikanunua ila  nimeipenda zaidi ya huyu dada hapo juu. Mimi nimenunu indiska, mpiga picha kaka Erik:-).NAWATAKIENI WOTE MWISHO MWEMA WA WIKI HII....IJUMAA IWE NJEMA KWA WOTE.

Wednesday, November 6, 2013

HUU NI UJUMBE WA JUMATANO YA LEO...tABASAMU/KICHEKO

 
Utamu wa maisha hutegemea hali ya nchi. Lakini Uzuri na kichekesho sio bima ya kufaulu katika maisha. Huu ni ujumbe wangu wa leo jumatano hii..Kila la kheri kwa wote mtakaopita hapa.

Monday, November 4, 2013

TUANZE JUMATATU HII KIHIVI :- KAPULYA SI MDADISI WA MASWALI TU BALI NA UTAMADANI WAKE PIA ANGALIA HAPA

Msifikiri anakusanya scalf na mawe tu kama mlivyoona hapa hapana anakusanya na vingine kama ,,,,,angalia hapa.....

 Hapa ni baadhi ya bangili za mdada huyu alizokusanya/nunua  napenda sana bangili na bado naendelea kukusanya....
 Hapo ni baadhi ya mikufu niliyonayo zawadi na nyingine ni kazi ya mikono ya wanangu
Na hapa ni baadhi ya heleni ambazi ni kazi ya mikono ya watu ambao wamebarikiwa kuwa na kipaji kama hiki.....TUDUMISHE UTAMADUNI WETU....JUMATATU NJEMA KWA WOTE

Saturday, November 2, 2013

JUMAMOSI YA LEO NA UJUMBE HUU...

Katika maisha vitu si muhimu.
NAWATAKIENI WOTE JUMAMOSI HII YA KWANZA YA MWEZI HUU IWR NJEMA..NA TUWAOMBEE MAREHEMU WOTE MAANA NI SIKUKUU YA MAREHEMU LEO.