Thursday, November 28, 2013

MWANAMTINDO WA LEO NA MTOKO WA NYEUSI ....BLACK IS GOOD !!!!

 Hivi ndivyo lilivyokuwa vazi langu leo koti ndefu nyeusi na suruali vimenunuliwa UNIQUE,blauzi/line toka Vila clothes.
 Hapa mdada anaonekana kuwa mbali kweli kimawazo.....
 ....hapa anawaza sijui nibadili kazi na kuwa mwana mtindo....anaendelea kufikiri
Na mwisho inaonekana hajapata jibu bado kwa hiyo anaendelea kufikiri. Je wasomaji mnaonanaje  kuhusu hili na kuhusu vazi la leo?....NAWATAKIENI WOTE KAMA ILIVYO HAPO ULIPO IKIWA ASUBUHI, MCHANA, ALASIRI, JIONI AU USIKU..BINAFSI NI JIONI HAPA NA NAANZA KUJIANDAA KUPIKA MLO WA JIONI.

7 comments:

Rachel siwa Isaac said...

Hahahhaha bora ubadili kazi dada wa mimi..KADALA.Uungane na Mwanamke wa Shoka da'Mija..mimi nitakuwa mpiga picha wenu.Kampuni itaitwa MIRAYA aU YAMIRA..CHAGUENI HAPO!!!!!!!

Tukija kwenye mavazi umependeza sana..wewe hata ukivaa Gunia Mwake tuu..Mtoto umefinyangwa..MUNGU alikuingiza Vyuma vyote vya uumbaji na kazi aliifanya sana tuu.

Haya ukishapika mimi nitakuja kukutembelea..dada.

Yasinta Ngonyani said...

Hahaaaaa! nimecheka kweli mpaka...machozi yaani Kachiki una vituko wewe mimi nachagua MIRAYA...JINA NZURU ALO. Hii ya kuvaa gunia ngoja nitajaribu siku yake,...na hapa kwenye kufinyangwa nimebaki hoi ila nasema AHSANTE KACHIKI WANGU...KARIBU SANA

Anonymous said...

Umependeza sana sana sana dada Yasinta. Natamani upige bila koti then uiweke nayo!

Anonymous said...

MIE SINA CHA KUSEMA

ray njau said...

Ubunifu wako umekubalika!!

Yasinta Ngonyani said...

usiye na jina!! Ahsante sana ..Hahaaaaa umenichekesha mno eti bila koti..haya ombi lako lipo jikoni:-)
Usiye na jina wa 3:30PM ! Ahsante kwani hilo pia ni neno.
Ray ! Ahsante kwa kuukubali ubunifu wangu:-)

Rafikio said...

Rafiki yangu umenoga kweli kweli!