Tuesday, November 12, 2013

NIMETAMANI JIONI HII NILE/NIPIKE UGALI ILA SINA UNGA NA NDIPO NILIPOKUMBUKA MAISHA YA UTOTONI!!

Mmmmmhhh!! Mwenzenu nimeka hapa nikiwa na mawazo kibao ....maisha haya hakika nimekumbuka mno ...UGALI WA MUHOGO na samaki halafu ukiongezea na matembele au kisamvu....basi tu . Sasa leo kisa cha kukumbuka hili ni kwamba ninajiuliza nipike nini maana nilitaka kupika ugali lakini sasa UNGA sina na kama mnakumbuka nililima bustani na niliweka akiba sasa unga sina  nipo hoi hapa. Mboga ipo  ila sina unga. Basi mawazo yakaja na kukumbuka wakati nilipokuwa KADALA kama huyo binti kutwanga na kuchekecha na mwisho mtu unakuwa unga tu mwili mzima...JE KUNA ANAYEKUMBUKA KAMA KAPULYA HAPA?

5 comments:

Anonymous said...

Yani umetukumbusha mbali sana! ugali ugali ugaaaaaaaaaliiiiii hamu ya ugali kwa mboga za majani. Sasa Yasinta ina maana unga ulioleta toka Tz umeisha mara hii???????Jamani uwe unabeba mwiiiingiiiiiii saaaaaaaaana sana halafu unalipia ile uzito unaozidi ili nasie tuukute haujaisha, ona sasa unga umeisha hata sijafika kwako kula ugali jamani jamani. Haya ukanunue wa njano wa Sweden ujichane ila hauna hata ladha!

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina!..yaani hakuna chaula kitamu kama ugali na mboga za majani. Ndiyo unga niliobeba umaniishia sikubeba mwingi na unajua sasa na hizi mboga nikawa najipikia tu kila siku kwenda kuangalia mama weeee umeisha..ila kuna unga fulani si wa njano nitautafuta huwa nanunua.....mazoea hujenga tabia kwa kweli

ray njau said...

Ugaliiiiiiiiiiiiiiii,ugaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ndiyo maisha na mafanikio yetu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! Yaani haswaaa bila ugali hakuna maisha na mafanikio...Lol

obat vimax said...

vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg