Showing posts with label TOGWA. Show all posts
Showing posts with label TOGWA. Show all posts

Tuesday, August 16, 2011

VYAKULA VYA ASILI NA KINYWAJI CHA ASILI (TOGWA) AMBAVYO NIMEKULA NA KUNYWA WAKATI NIPO NYUMBANI SONGEA/RUHUWIKO!!!



Siku hii nilikuwa na furaha sana kwa kupata togwa kinywaji ambacho nakipenda sana, ila nasikitika sikuwa na kisonjo au kata (deve) ila hata hivyo ilipanda...:-)


Baadaye nikasema ni lazima nile karanga za kuchemsha kwa vile mimi si mpenzi wa mtesa wala mboga za kuweka karanga. Nipendacho ni karanga za kuchemsha au ziwe mbichi na halafu kukaanga hapa utanipatia...ni kweli nikazipata...nyumbani ni nyumbani......





Nilivyokuwa na bahati ulikuwa ni msimu wa viazi vitamu (mbatambata) au wengine wanasema makapa...basi nakwambia mikate, chapati, maandazi nk nikavitupilia mbali kabisa nikawa na vyangu nilivyovizoea tangu utoto...mihogo, ndizi na magimbi pia ingawa nilipitiwa kupiga picha kwa utamu:-) TUONANE TENA WAKATI MWINGINE ....!!!!!!