Tuesday, August 16, 2011

VYAKULA VYA ASILI NA KINYWAJI CHA ASILI (TOGWA) AMBAVYO NIMEKULA NA KUNYWA WAKATI NIPO NYUMBANI SONGEA/RUHUWIKO!!!



Siku hii nilikuwa na furaha sana kwa kupata togwa kinywaji ambacho nakipenda sana, ila nasikitika sikuwa na kisonjo au kata (deve) ila hata hivyo ilipanda...:-)


Baadaye nikasema ni lazima nile karanga za kuchemsha kwa vile mimi si mpenzi wa mtesa wala mboga za kuweka karanga. Nipendacho ni karanga za kuchemsha au ziwe mbichi na halafu kukaanga hapa utanipatia...ni kweli nikazipata...nyumbani ni nyumbani......





Nilivyokuwa na bahati ulikuwa ni msimu wa viazi vitamu (mbatambata) au wengine wanasema makapa...basi nakwambia mikate, chapati, maandazi nk nikavitupilia mbali kabisa nikawa na vyangu nilivyovizoea tangu utoto...mihogo, ndizi na magimbi pia ingawa nilipitiwa kupiga picha kwa utamu:-) TUONANE TENA WAKATI MWINGINE ....!!!!!!


13 comments:

Anonymous said...

JASIRI HAACHI ASILI NA MUACHA ASILI NI HASIDI NA HANA AKILI.
"LIBARIKIWE SANA TITI TAMU LA MAMA YAKO MZAZI ULINYONYA"
Watu hulia:-
Mama yangu au Yarabi nafsi yangu!


R.Njawa
Kwa Wangoni
TZDAR.

Mwanasosholojia said...

Lazima utakuwa "umechana" (umenenepa) sana kwa misosi na vinywaji hivi da'Yasinta...:-)

Anonymous said...

Utafiti wa wanazuoni wa tasnia ya siha njema na lishe bora wanathibitisha kuwa chimbuko maradhi mengi katika hizi zama za teknohama ni ukosefu wa vyakula vilivyosheheni lishe asilia kama picha ya binti wa kingoni/kimatengo kutoka kule Ruhuwiko iliyojieleza.Kama hujui kusoma hata kuielezea picha nao mtihani wa mlimani wajemeni?Wadau wangu naomba kutoa hoja.

Kutoka Mamba Mkolowony
Moshi Vijijini
Msee wa kichagga
R.Njau

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana R. Njawa....

Kaka Mathew! Ha ha ha aaa nimecheka kweli..hapana sijanenepa ila nimependeza kidogo sana:-)

R.Njau! Usemacho kina ukweli ..hakuna chakula/vyakula vitamu kama vya asili...

Rachel Siwa said...

Duhh ulifaidi sana da'Yasinta!!!

John Mwaipopo said...

hakika ulikuwa na wakati mzuri. vipi likololya nanyungu nalo uliligongapo?

Yasinta Ngonyani said...

Rachel ndugu yangu nimekula kiasi chake na kuweka akiba..:-)

Kaka John..Likolo la nanyungu sikukosa pia matembele ila nasikitika sikuweza kuandika na kubeba mpaka huku:-(

chib said...

Big up

MARKUS MPANGALA said...

ha ha ha ha unidagadisi kweliiii. naunga mkono jasiri haachi asili mweee

Goodman Manyanya Phiri said...

Unene uliozidi unasababishwa na Togwa! (lol!!!)

Halafu, kuchekelea hovyo pia mwiko kama hutaki kunenepa zaidi! (lol!!!)


SIFANYI UTANI!!!

Soma hapa:
http://kamalaluta.blogspot.com/2011/08/cheka-unenepe-japo-unene-sio-dili.html

emu-three said...

Vyakula vya asili wakati mwingine ni dawa, ...Ukiangalia sana magonjwa mengi kama presha, kisukari yanashinikizwa na vyakula vilivyochakachuliwa...!

Matha Malima said...

jamani utogwa huu dada unanikumbusha mbali sana dada yangu hongera kwa kula hihi je ugali wa muhogo na mbelele JE? WE ACHA TU MTU KWAO

Sara Chitunda said...

Yaani dada Yasinta tisa kumi umenitamanisha karanga za kuchemshwa mate yanadondoka, maana ninavyopenda! we acha tu.