Tuesday, August 23, 2011

MDADA HUYU /YASINTA SIO MPENZI WA SAMAKI KWA UGALI WA MUHOGO TU BALI ....

....Ni mpenzi sana wa kuchuma/kutafuta na kula UYOGA pia . Leo nimeamka nikawa najisikia hamu kweli ya uyoga basi nikaamua niende mstuni na kutafuta matokeo yako ni hayo hapo juu. Nimechuma mwenyewe kwa mikono yangu . Jambo jingine ambalo ni zuri kwenda mstuni sio kutafuta uyoga tu. Ni kwamba ni dawa nzuri sana ya kupoteza mawazo. Kama mtu una mawazo sana . Maana ukiwa mstuni unakuwa peke yako na pia kimya utakachosikia sana sana ni milio ya ndege tu. NAPENDA SANA KUWA MSTUNI NIKIWA KATIKA HALI HII YA MAWAZO. PIA KULA UYOGA...KARIBUNI TUKULE JEMENI. Ila kwa sasa ntashindwa kuupika kwani inabidi niende kubeba maboxiiiiiiiiii.....kesho tutaangalia jinsi ya kupika...Jumanne njema kwa wote.:-)


7 comments:

Anonymous said...

Da,Yasinta kuwa mwangalifu na matumizi ya maneno.mfano kuingia msituni, kwa sisi watu wa unyamwezini/usukumani,ina kwenda sambamba na kuchimba dawa au kwenda kujifungua haja kubwa. na hii, porini ndo unabeba jembe lako taratibu ukimaliza vitu vyako unarudi swafi.(natania tu usijali sana)tukirudi kwenye uyoga,hakikisha hauna sumu.porini ni pazuri sana kwa kutafakari na kupata muda wa kuwa pekeyako,wenzetu misitu yao ni salama,kwetu ukienda msituni lazima uwe makini,akina mzee nyoka nk,hawakosi.haya box jema. Kaka S.

Yasinta Ngonyani said...

Eeeh! kaka S. nawe huna dogo...LOL
Uyogo huo hauna sumu ndo maana nimechuma huo wa njano tu kwa vile naufahamu. Yaani hakuna sehemu nzuri ya kutafakari kama mstuni....Nyoka wapo ila hawana sumu pia kuna wanyama wengine wakali kama vile dobi ila leo sijamwona:-)

Simon Kitururu said...

Mmmmh!

Matha Malima said...

jamani dada yangu umenitamanisha sana sanaaa

Penina Simon said...

mh!! mimi napenda pia lakini naogopa sana nyoka/mojoka

Sara Chitunda said...

Nami napenda kula uyoga kwani unanukia vizuri na radha yake pia

ufahamu said...

duh, dada hiyo kwa kimakonde tunaita uvahe (uyoga), safi sana hiyo.