Tuesday, August 30, 2011

NILIPOKUTANA NA MWANABLOG MARKUS MPANGALA

Baada ya kukutana na kaka S hapa Ruaha safari ikaendelea kufika Dar es Salaamau, ikawa bahati tena nika/tukakutana na mwanablog mwingine pia ni mjomba na rafiki wa karibu sana. Si mwingine tena ni Mzee wa Lundu Nyasa.


Alijitahidi na akaja hapa Silver Sands kutusalimia hapa ni yeye Mzee Lundu Nyasa/Markus Mpangala, Yasinta na Kijana Erik.
Na hapa ni Markus na wajomba zake Erik na Dada Camilla.... Ilikuwa ni furaha kukutana na yeye. Kwani kama kawaida huwa furaha sana kuonana tulibadilisha maneno mawili matatu na muda ukawa ni mdogo ....

8 comments:

emu-three said...

Safi sana, alituwakilisha ambao hatukupata bahatii ya kukuona

MARKUS MPANGALA said...

Najua ile siku,
furaha ilidumu,
vicheko vitamu,
soga adimu,

mioyo iloja hamu,
hamu kufahamu,
muda gani utadumu,
lakini siku tamu,

Camilla ulicheka,
utani nlokulazimisha,
ukacheka kwa nukta
Erik mwana wa Yasinta,
Soka analipenda.

naweza kuandika mengiiiiiiiii lakini ni raha sana kuona ana marafiki na wale tupendanao. Erik mjomba kazana hadi umpiku Zlatan nawe Camilla Lol...... kama Naomi Campbell. Hakika binti Yasinta anafaa kuwa mwanamitindo. Nitafurahi siku nikimwona anafanya kazi hiyo. ila chaguo lako...... utunze.

Fadhy Mtanga said...

ayaaaaah! atakuwa alijidai kweli..we mtani shemeji hii sikukuu mie mgeni wako sasa ole wako uzime simu kisa kulewa ulanzi

EDNA said...

Furaha iliyoje jamani.

PASSION4FASHION.TZ said...

Hongereni wanablog!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Hii safi sana! Ni fursa adimu na adhimu pia!

ray njau said...

Haya ndiyo maisha na mafanikio bi mkubwa wetu!

Goodman Manyanya Phiri said...

TOUCHING BASE!

Tunashukuru sana mumekuja kututembelea. Mbona lakini mumekimbia haraka na kurejea ng'ambo? Muliogopa joto nini...?

Haya, karibuni tena, Watoto Wazuri!