Monday, August 29, 2011

NYIMBO ZA MCHAKAMCHAKA/KUMBUKUMBU

Leo nimekumbuka wakati nasoma shule hasa shule ya msingi saa kumi na moja alfajiri kuwahi shule, kisa nini? Kuwahi namba na kukimbia mchakamchaka huku mnatweta kama nini na mkiimba nyimbo:- Kwa mfano:-1. Panda mlima panda, panda, panda, panda usichoke........x2 wimbo wa 2. . Iddi amin akifa mimi siwezi kulia nitamtupa kagera awe chakula cha mamba.x2 wimbo wa 3. . Jua lille literemke mama, mwezi nao uteremke mama haiyahiyaaa hiyaa hiyaa mamaaaa.....x2wimbo wa 4. Alisema, alisema, alisemaaa Nyerere alisema vijana wangu wote mwalegea shart tuanze mchakamchakax2.....Kama kuna mtu anakumbuka nyimbo nyingine basi karibu kuongezea hapa.........Ila kuna kitu nimeumia sana. Ni kwamba safari hii nilipokuwa nyumbani, nimejaribu kuwahoji shangazi zangu kuhusu swala hili la kukimbia mchaka mchaka. Wakanijibu kuwa wao hawajui mchakamchaka, yaaniHAWAKIMBII KABISA...Sasa sijui ni Ruhuwiko tu au?..Nikaanza kujiuliza sasa wanafunzi hawa watakuwa kweli wakakamavu au? Sijui wenzangu mnalionaje hili swala? Tuendako kweli kuzuri?....Mmmmhh !!!

7 comments:

Anonymous said...

nyimbo,ni nyingi sana,mfano-kaburumatata hiya-unaitikia hya... sasa makaburu wenyewe kibao bongo,sijuwi wanajuwa tulikuwa tunawaimba!? wimbo mwingine-sikutegemea mamaa ee,kama ungekuwa hivyoo,kiitikio-oomwambi,ooomwambie ......
-mwingine-kimbunga nichanini watu kuvamia mpakani.
-mwingine-vijana mmechoka,kiitikio-bado mbonahamuimbi -kiitikio,tunaimba.
ngoja niishie hapo.Ila tukirudi kuhusu faida za mchakamchaka,zina eleweka,ila kwa sasa naona yawezekana mazingira pia yana changia.mfano mfumo wa wakati ule uliwezesha mambo haya yawe,lakini sasa hivi mazingira kidogo yamebadirika,maeneo yakufanyia michakachaka hiyo wakati huo yaliruhusu,mwingiliano wa watu na makazi haukuwa kama sasa,sasa hivi shule kupata kiwanja cha mpira nikazi.pia ongezeko lawatu/watoto mashuleni,siyo rahisi kwa wakati mmoja ukawa tia barabarani kwa mchakmchaka.jambolingine,walimu nao ule morali wa ukakamavu hakuna,na wakati mwingine siyo kosa lao.iliyo baki sasa hivi nijuhudi za watoto wenyewe binafsi wakitaka kuwa fiti kimazoezi wafanye nawala wasitegemee shule.mwisho kabisa mifumo ya uendeshaji michezo mshuleni sidhani kama inafuatwa ama haipo kabisa sinahakika na hilo. Kaka S.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka S. kwa kweli inasikitisha kidogo kwani inaonekana kama watoto siku hizi hawana ukakamavu sana kama wao wenyewe hawajikakamui. Pia inasikitisha zaidi kuona/kusikia watoto wanapenda lakini ndo hivyo sasa...kama ndo hivi basi maisha ya zamani nayatamani sana...ila siku hizi nako hizi shule za kata zinajengwa mno kweli kuna walimu kutosha? nawaza tu kwa sauti sijui kama inawezekana kuwa ni sababu pi?---

Anonymous said...

-Kipara cha Banda kina ukoko..x2

Anonymous said...

NYINGINE NI MWENYEKI MWALIMU NYERERE BAABA IMARISHA UKOMBOZI WAAFRIKA MAADUII WA BARA LA AFRIKA WAMEANZA KUWAHUJUMU VIONGOZI MWALIMU EE UHURU WETU HAUWEZI KUWA SAFI MPAKA AFRIKA YOTE IWE HURU MWALIMUEE ULIKUWA WIMBO MZURI JAPO ZIJAWEZA KUPANGILIA

Anonymous said...

NYOTE UMEKWENDA UMETUWACHA WENYEWE NYOTA WATUACHA TUNALIA NYOTA NYOTE WEWE NYOTE WATUACHA WENYEWE HUU WIMBO NI MZURI MTU AMBAYE AJUA INAPATIKANA WAPI ANIJUZE HUU WIMBO ULIIBWA WAKATI WA MAOMBOLEZO YA HAYATI JULIAS KAMBARAGE NYERERE ULIHUZUNISHA SANA

Goodman Manyanya Phiri said...

@Kapulya: Umeuliza suali zuri sana, Mdogo Wangu. Na sidhani utapata jibu la haraka. Lakini ukweli ni kwamba ujinga, uvivu wa kimawazo na kushindwa mitihani vyote vipo pamoja na watoto wasiefanya mchakamchaka wala mazoezi yoyote yale.


@ Anonymous: "Kipara cha Banda kina ukoko"?

Hiyo kali sana aiseeee! Sasa Banda aliwakosea nini WaTZ? nipashe tafadhali.

Nauliza kwa kuwa ya Idi Amin na mamba zake huko Kagera naelewa kabisa...!

Anonymous said...

Mm nimwanajeshi na ulinzi wa wananchi ninailinda nchi na ulinzi wa wananchi na dumisha uhuru na umoja wa wananchi.