Tuesday, December 31, 2013

SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MAMA MAISHA NA MAFANIKIO NA FAMILIA YAKE !!!

Marafiki,ndugu, na wasomaji  wapendwa!
Ukaribisheni mwaka mpya uwe wa Mafanikio, Amani, Mwanga na Furaha katika maisha yetu.
Nakutakieni wote, wewe na familia yako kila jema na furaha tele katika mwaka mpya 2014.
KHERI KWA MWAKA MPYA 2014. KUMBUKENI WOTE MNAPENDWA!!!!
Nimeona si mbaya kama tukiuvuka mwaka huu kwa kipande hiki cha mziki si mnajua mziki na kazi au mziki,sherehe aaahh ngoja tuserebuke!!.....
TUMWOMBE MUNGU TUONANE NA KUSEMA TENA MWAKA 2014..NA UWE MWAKA WA MATUMAINI----NANGONYANI/KAPULYA

Sunday, December 29, 2013

TUMALIZA JUMAPILI YA MWAKA HUU 2013 NA MWIMBO HUU WA DADA BAHATI BUKUKU :- DUNIA HAINA HURUMA.


NAWATAKIENI WOTE JUMAPILI HII YA MWISHO KWA MWAKA HUU 2013 IWE NJEMA SANA WAKATI TUKIUSUBIRI MWAKA 2014. JUMAPILI NJEMA SANA....KAPULYA

Thursday, December 26, 2013

NAPENDA KUWAKUMBUSHENI TUSISAHAU KULA MATUNDA...BOXING DAY NJEMA!!!!!

Namshukuru Mwenyezi Mungu Noeli imekwisha vizuri pamoja na kwamba Noeli yangu imeishia mzigoni. Kila la kheri. TUSISAHAU MATNDA:-D....Nangonyani

Tuesday, December 24, 2013

SALAMU ZA CHRISTMAS KUTOKA KWA KAPULYA.....

Nawatakieni wote sikukuu hii ya Christmas/Noeli iwe yenye baraka, amani, upendo na furaha. Mwenyezi Mungu na awe pamoja nanyi kwa kila mtakachofanya. CHRISTMAS NJEMA/GOD JUL!!

Monday, December 23, 2013

TUANZE JUMATATU HII KIHIVI NA NENO AMANI!!!

AMANI:- Ni kitu cha thamani sana. Ambacho kila mtu angependa kuwa naye au hata kuwa na ndoto.
NAWATAEKIENI WIKI HII YA NOEL IWE NJEMA NA NOELIENDE SALAMA. KAPULYA

Sunday, December 22, 2013

NI DOMINIKA YA NNE YA MAJILIO MWAKA A..PIA BADO SIKU CHACHE NA NDIPO ITAKUWA KUZALIWA KWAKE YESU MKOMBOZI WETU

"Bikira atachukua mimba, atamzaa mtoto wa kuime, naye ataitwa Emanuali" Maana yake "Mungu yupo pamoja nasi."
NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI HII KABLA KUZALIWA KWAKE BWANA WETU YESU KRISTO IWE NJEMA KWA WOTE. KAMA ILIVYOANDIKWA MUNGU YUPO PAMOJA NASI. WOTE MNAPENDWA....KAPULYA

Friday, December 20, 2013

MWEZI DESEMBA:- A MONTH OF DECEMBER SIMPLY STANDS FOR......

D- days of
E- evaluation
C- celebration
E- encouragment
M- memorizing the
B- blessings
E- establing next year plans and
R- renewing your relationship with God.

BASI NGOJA NIWATAKIENI MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA HILI AMBALO LINATUPELEKA SIKUKUU YA KUZALIWA BWANA WETU KRISTO.

Thursday, December 19, 2013

HATIMAYE NIMEPATA MBOGA YA LIKUNGU AMBAYO NIIPENDAYO..NYASA SAFI SANA

 Hapa ni katika maandalizi ya hii mboga tamu ya likungu ..halafu likungu ni tamu zaidi liwapo bado halijakaushwa sana yaani linatoka tu kukamatwa na kukanda na kuchemsha na chumvi  halafu ugali wa muhogo weweeeee....utajiuma kidogolo...
Na hapa tayari limekaushwa kwa moto kwa akiba au kwenda kuuza...nadhani waliowahi kula wananielewa....Ni mboga nzuri sana ..Alhamis njema kwa wote.

Wednesday, December 18, 2013

NAPENDA KUTOA SHUKRANI WA WOTE MLIOTUFARIJI KWA MSIBA WA BIBI YETU..

Shukrani nyingi ziwafikieni wote mliokuwa pamoja nasi katika sala na kutufariji kwa kupitia hapa Maisha na Mafanikio na pia mail pia ujumbe wa simu ya kiganjani. Mwenyezi Mungu na azidi kuwapa upendo. Na sasa hivi tu nimepata taarifa kuwa zoezi la kumsindikiza bibi yetu kwenye nyumba ya milele zimeenda safi. Ahsante Mungu...Pumzika kwa amani bibi yetu mpendwa.

Sunday, December 15, 2013

TUMEPATWA NA MSIBA LUNDUSI/PERAMIHO KWA AKINA NGONYANI

PUMZIKA KWA AMANI BIBI NAPINGI
Hapa ilikuwa 2001 nyumbani Lundusi/Peramiho. Ni baba yangu mkubwa na mke wake na mjukuu wao. Lakini kwa vile baba yangu alilelewa na wao basi sisi watoto wake tumezoea tangu utoto kuwaita babu na bibi...hii ni historia fupi sana. Kwa hiyo leo asubihi mapema nimetumiwa taarifa kuwa bibi hatunaye tena. Amekuwa ameugua muda mrefu sasa. Bibi tutakukumbuka daima kwa yote mema na mazuri uliyotuachia. Sisi tulikupenda lakini Mungu anakupenda zaidi. Lihidimiwe jina lake. PUMZIKA KWA AMANI BIBI TUPO KATIKA MAOMBI.  MUNGU AIPE FAMILIA YA NGONYANI KOKOTE ILIPO NGUVU KWA KIPINDI HIKI KIGUMU.

Friday, December 13, 2013

HAPO SASA UNAUZA VIATU MWENYEWE UNAPIGA ZA KUKU......KAAZIII KWELIKWELI!!!

Hapa nimekumbuka mzee mmoja alikuwa akivua samaki halafu anaziuza zote na yeye mwenyewe na familia wanakula mboga maji au maharagwe. Au kuna wengine walikuwa wakilima mpunga basi wanauza wote na wenyewe wanakula ugali kila siku kwa raha zao zoteee! Haya ngoja niwatakieni Alhamis njema

Wednesday, December 11, 2013

HUU NI MLO WANGU WA LEO MCHANA UGALI NA SUKUMAWIKI/MBOGA MABOGA!!!

Mlo aupendao Kapulya ndo huu Ugali kwa mboga maboga. Halafu sasa napenda kupika mboga hii bila mafuta wala kitunguu. Ni maji, chumvi, nyanya na pilipili kama ipo kwa mbaliiii.....mmmhhh hapo ndo utauona utamu wa mboga hii. Mboga ni kazi ya mikono yangu mwenyewe. Awekaye akiba basi hana shida kifuku kikija:-) MUWE NA JIONI NJEMA NA WALE WENYE MCHANA AU ASUBUHI BASI NA IWE NJEMA, NA USIKU UWE MWEMA PIA. Kapulya!!!!

TUSISOME MAWAZO YA WENGINE!

Ni hatari kwa mtu kudhani kwamba, anajua kila ambacho kinaendelea kwenye mawazo au hisia za mpenzi wake. Kuna uwezekano mkubwa hisia zako zinaweza zisiwe sahihi, kama ambavyo mara nyingi imekuwa ikitokea. Kuna migogoro mingi ambayo chanzo chake ni hisia potofu, hisia zitokanazo na mtu kujaribu kuingia kwenye mawazo au hisia za mwenzake.

Hebu fikiria, umeingia ndani mwako kutoka huko utokako. Unamkuta mumeo/mkeo akiwa amekunja uso. Kabla hujamuuliza chochote unaanza kufikiria kwamba, amekasirika kwa sababu leo umechelewa kurudi nyumbani kwa nusu saa tu. Unaanza kuwaza kwa kulaani kwamba, mumeo/mkeo siyo mtu wa maana kwa sababu ya wivu. Unaweza kufikiria kwamba, usiku huo utamwambia ukweli na kama ni kugombana ni afadhali iwe hivyo, halafu unamuuliza "Vipi mbona uko hivyo, nini tena?"

Mumeo/mkeo anakujibu "Hapana, nina taarifa mbaya, nimesimamishwa kazi kutokana na tuhuma fulani...." Unabaki ukiwa umepanua mdomo, kwa sababu uliingia kwenye mawazo yake na ukawa umekosea sana. Mfano huu ni wa jambo dogo, kuna wakati tunaweza kuingiza mawazoni mwetu fikra kwamba, wenzetu hawatupendi kwa kudhani kwetu kwamba tunaweza kujua yale yanayoenda mawazoni mwao. Kutokana na kufikiri kwetu hivi, tunaweza kuanza kufanya mambo ambayo sasa ndiyo yatapelekea wapenzi wetu kuacha kutupenda.
HABARI HII NIMEITOA KWENYE KITABU CA MAISHA NA MAFANIKIO KILICHOANDIKWA NA MUNGA TEHENAN...JITAMBUE
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Hii huwa inatokea mara nyingi sana na watu wengi wamepoteza marafiki zao kwa hili jambo la kusoma mawazo...ni bora kuuliza....

Monday, December 9, 2013

TUANZA WIKI HII NA TAARIFA HII/BUSTANI MPAKA MWAKANI MWEZI WA SITA :-(

 Hapa ilikuwa mwezi wa sita-tisa mwaka huu ..ni kutoka tu nje na kuchuma mboga na kula ......
THELUJI IMEANZA
Na sasa eneo hilo hilo leo linaonekana hivi. Inabidi nisubiri mpaka mwakani mwezi wa sita tena. Kaaazi kwelikweli....mmhhh labda nitumie makopo sijui?? Je mna ushauri wowotw ule?

Sunday, December 8, 2013

NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA ....LEO NA MTOKA WA NYEUPE HIVI NDIVYO NILIVYOTOKEZEA IJUMAA..!!!MWANAMTINDO KAPULYA:-)

 Leo mdada kavalia nyeupe ilikuwa ijumaa kulikuwa na sherehe na hivyo ndivyo alivyotokezea ....:-)
Anashangaa kama vile anatoka usingizini....Mpiga picha ni kaka Erik. Nawatakieni wote Jumapili njema sana na iwe yenye upendo na baraka. na pia maandalizi mema ya Noel.

Saturday, December 7, 2013

SIKU ZAKE ZIMEKWISHA :- A Tribute Poem for Nelson Mandela by Dr. Maya


TUENDELEE NA MAOMBOLEZO YA BABU YETU NELSON MANDELA ..SHAIRI HILI LIMENIGUSA SANA...DR.MAYA  AHSANTE SANA...

Friday, December 6, 2013

AFRIKA TUMEPATWA NA MSIBA BABU YETU NELSON ROLIHLAHLA MANDELA HATUNAYE TENA.

Nelson Mandela wakati wa uhai wake
 
1918-2013....ni pengo kubwa umeacha. Utakumbukwa daima. Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema. Amina.


TUTAKUKUMBUKA DAIMA MKOMBOZI WETU. AMINA

Thursday, December 5, 2013

MATUNDA NI MUHIMU KATIKA AFYA ZETU TUZINGATIE...

Huu ni mlo wangu wa leo mchana mchanganyiko wa matunda mbalimbali. Kama ilivyo ni kwamba matunda ni muhimu katika afya zetu. Usisahau kula hata tunda moja tu  kwa siku....Kila la kheri kwa wote....

Tuesday, December 3, 2013

JUMANNE YA LEO TUTEMBEE KWETU LITUMBANDYÓSI /NYUMBANI NI NYUMBANI!!!

 Hapa ni sokoni petu ukitaka dagaa, viazi vitamu, samaki nk.utapata bila matatizo:-) 
 Na hapa usipotaka dagaa au samaki basi waweza kujipatia kiti moto ...
Na hapa ndo unga tayari umeshasagwa kwa hiyo hakuna shida. Isipokuwa  ni  kuandaa chakula tu sasa....Nimeutamani huu unga basi tu...NAWATAKIENI JUMANNE NJEMA..

Monday, December 2, 2013

AKIBA HAIOZI HAPA MVUA IKIKOLEA HAKUNA SHIDA HAPA!!!

Ni Jumatatu ya kwanza ya mwezi huu nami nimeona tuanza kihivi. Akiba haiozi si mnajua mvua zikianza. Ila hapa kajiandaa haswaa hakuna shida kwa kweli.......NAWATAKIENI JUMATATU NJEMA NA MWANZO MWEMA WA JUMA. TUPO PAMOJA...KAPULYA/KADALA:-)

Sunday, December 1, 2013

JUMAPILI HII YA KWANZA YA MAJILIO MWAKA A NA IWE NJEMA KWA WOTE

Napenda kuwatakieni wote Jumapili hii ya kwanza ya mwezi huu wa kumi na mbili. Na pia ni Jumapili ya kwanza ya majilio. JUMAPILI NJEMA KWA WOTE.