Thursday, December 19, 2013

HATIMAYE NIMEPATA MBOGA YA LIKUNGU AMBAYO NIIPENDAYO..NYASA SAFI SANA

 Hapa ni katika maandalizi ya hii mboga tamu ya likungu ..halafu likungu ni tamu zaidi liwapo bado halijakaushwa sana yaani linatoka tu kukamatwa na kukanda na kuchemsha na chumvi  halafu ugali wa muhogo weweeeee....utajiuma kidogolo...
Na hapa tayari limekaushwa kwa moto kwa akiba au kwenda kuuza...nadhani waliowahi kula wananielewa....Ni mboga nzuri sana ..Alhamis njema kwa wote.

9 comments:

Nancy Msangi said...

Da yasinta pole kwa msiba NW ndio nimepita hku na kuona tumuombee MN sote tu njia moja. Apumzike kwa Amani.

Nancy Msangi said...

Da yasinta pole kwa msiba NW ndio nimepita hku na kuona tumuombee MN sote tu njia moja. Apumzike kwa Amani.

Anonymous said...

Inaelekea ni tamu maanake ulivyoisifia basi ni tamu, angalau wala siijui na wala sijawai kuiona wala kuisikia,na ningekua jilani yako ningeomba unikaribishe nami nionje hiyo mboga likungu

Yasinta Ngonyani said...

Nancy ahsante ni kweli ni kumwombea tu sasa.

Usiye najina ni tamu sana ungepnja siku moja ungeniamini...najua unatamani..na ukipata ugali wa muhogo weweeeeee

Anonymous said...

Hata mimi siijui hii mboga ya likungu. Nitumie kwenye email yangu shedhany@yahoo.com nipate kuionja!By Salumu.

Anonymous said...

Sijaila siku nyingi mboga ya likungu lakini naijua ni tamu kweli. Ina ladha ya kipekee na pengine siyo rahisi kupata kitu cha kulinganisha ladha yake

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu usikonde nitakutumia na uonje halafu usimulie utamu wake....:-)

Usiye na jina wa 4:48PM..Nakukubalia kabisa ni kweli ngumu kuelezea ladha yake inabidi kila mtu aonje mwenyewe--ila ni mboga tamu sana:-)

Anonymous said...

Dada Yasinta hiyo mboga huko ulipo umeipata wapi? haya kila la heri.

plotz4sale said...

Aisee hii kitu ni nouma,ukionja hutaacha kui miss. Umenikumbusha mbali sana ndugu.