Wednesday, December 18, 2013

NAPENDA KUTOA SHUKRANI WA WOTE MLIOTUFARIJI KWA MSIBA WA BIBI YETU..

Shukrani nyingi ziwafikieni wote mliokuwa pamoja nasi katika sala na kutufariji kwa kupitia hapa Maisha na Mafanikio na pia mail pia ujumbe wa simu ya kiganjani. Mwenyezi Mungu na azidi kuwapa upendo. Na sasa hivi tu nimepata taarifa kuwa zoezi la kumsindikiza bibi yetu kwenye nyumba ya milele zimeenda safi. Ahsante Mungu...Pumzika kwa amani bibi yetu mpendwa.

4 comments:

Nicky Mwangoka said...

Pole sana dadangu. Nimechelewa kupata taarifa hizi. Mungu akupe wepesi na faraja katika kipindi hiki cha majonzi. Ampokee bibi yetu kwake mbinguni Amina.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mwangoka ahsante..wala hujachelewa...pole ni pole.

Manks said...

Poleni sana Dada Yasinta,Mwenyenzi Mungu awape faraja na nguvu katika kipindi hiki cha majonzi.Pumzika kwa Amani Bibi.

Yasinta Ngonyani said...

Manks...ahsante sana kwa pole.