Monday, October 31, 2016

JUMATATU HII YA MWISHO WA MWEZI HUU WA KUMI TUMALIZE NA UJUMBE HUU KUTOKA KWA MIMI KUJA KWENU WASOMAJI WA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO

Maisha ni mtihani, kwa vile watu wengi hufeli kwa sababu wanajaribu/tunajaribu kukopi/kuiga maisha ya wengine. Tunasahau ya kwamba kila mmoja ana mtihani wake.
NAWATAKIENI WOTE MWISHO MWEMA WA MWEZI HUU WA KUMI!

Thursday, October 27, 2016

HILI NI CHAGUO LA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA HII IWE NI PICHA YA WIKI HIII...

Ebu angalia hii picha unafikiri utaweza tu kupita hapa bila kusimama na kununua  vitunguu au tu hata kuongea na watu....Binafsi nimependa sana mwonekano wa hii picha...MNAPENDWA WOTE NA KAPULYA:-)

Wednesday, October 26, 2016

JE? UNAKUMBUKA KITABU HIKI CHENYE HADITHI YA JUMA NA ROZA?

 Tia maziwa
Tia sukari
Roza ana kiu 
kunywa chai Roza"
AU HII HADITHI YA MWANASESERE

Nimekikumbuka sana hiki kitabu wale wenye umri sawa nami watakuwa pia wanakumbuka ....hivi vitabu siku hizi havipi kabisa ...TUPO PAMOJA...

Tuesday, October 25, 2016

MAISHA NI KAMA KITABU...Maisha ni kama kitabu, kuna kurasa nyingine ni za kusikitisha, nyingine za kufurahisha na nyingine kusisimua. Lakini usipofungua hizo kurasa kamwe hutaweza kujua ni nini kipo kwenye hizo kurasa zifuatazo.
SIKU NJEMA

Sunday, October 23, 2016

JUMAPILI NJEMA NA UPENDO NA FURAHA ZITAWALE KATIKA MIOYO YENU

 Ulinzi wa Mungu uwe nasi/nawe siku zote. Amina.

Thursday, October 20, 2016

ZILIPENDWA. ..UTAMU WA MAJI YA MTUNGI AUJUE NI KATA

Hakika leo  nimekumbuka mbali sana...ilikuwa kila baada ya siku mbili ni lazima kuchemsha maji na kuyachuja kwa kitambaa safi cheupe na kuyaweka mtungini kwa ajili ya kunywa. Nitaikumbuka milele domestiki hii niliyofundishwa na mpendwa MAMA yangu.. .SIKU NJEMA KWA APITAYE HAPA!

Tuesday, October 18, 2016

TUSIWE WATU WA KUSAHAU MARAFIKI MAANA SIKU MOJA UTAWAHITAJI

RAFIKI NI BORA KULIKO MWANASESERE
Nimekaa hapa huku nikiwa na mawazo mengi katika kichwa changu...najiuliza:-  Hivi ni lini nitapata fursa ya kukutana na baadhi ya marafiki zangu? Hii ingekuwa fursa murwa kwangu kukutana tena baada ya muda mrefu kupoteana na kusikia maisha yao, familia na  kuhusu kazi zao. Muhimu zaidi kwangu ingekuwa kupata fursa ya kuonana na wao pia kuongea mawili matatu kwa nia ya kubadilishana mawazo. Kwani  ni vyema sana kuwa na  marafiki wanaokujali na unaowajali katika shughuli za kila siku za kimaisha. Tukumbuke, baadhi yetu marafiki ni kama funguo ya maisha. Inawezekana kazi uliyo nayo , mke/mume uliyo nayo nk umepata kwa kupitia rafiki. Kwa hiyo, tusiwe watu wasio wajali marafiki hasa wale wa muda. Binafsi nimepoteza marafiki wengi sana wale wa kitambo...jambo ambalo natamani siku moja tuonane tena  katika utu uzima huu. Ndugu zanguni kama mna marafiki ambao hakuona umuhimu wao jaribu kuwatafuta . Katika maisha ni vizuri kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kukutana na watu mbalimbali na mwisho mkawa marafiki wa kupendana zaidi ya ndugu uliyezaliwa naye tumbo moja. Pia tuwe na tabia kuchukua fursa kukutana na marafiki ili kujenga na kudumisha urafiki wetu maana mwisho wa siku utakuwa faida. Ila isiwe tu pale kwenye shida ndiyo urafiki,  hapana...ni vyema kujuliana hali kila wakati huku tukitakiana maisha mema hasa pale tukosapo muda wa kukutana. Maana katika maisha hakuna asiyependa kukumbukwa. Nadhani wengi wengi wetu tumekwisha wahi jiuliza:- kama ungependa kusahaulika na marafiki/watu wa karibu wako? nadhani jibu unalo....

Monday, October 17, 2016

NI JUMATATU NYINGINE NA WIKI MPYA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMEONA IANZA KWA MTINDO HUU...MAMBO MAHIMU KATIKA MAISHA AMBAYO YAPASWA TUYAZINGATIE....

Katika maisha kuna vitu/mambo saba ambayo wote tunapaswa kuyajua... nayo ni kama yafuatayo :-Furaha, karaha, misukosuko, majonzi, migogoro, mikasa na  chuki.
Haya yote husababishwa na viumbe hai kama mimi na wewe, ili kiyashinda haya yatupasa tuwe na mambo nne(4) nayo ni:- Subira, uelewa, uvumilivu na msamaha. Lakini pia katika maisha yako uwe karibu sana  na mambo haya manne :- msimamo, mkweli, ujasiri na Imani na halafu epuka sana mambo haya matano yafuatayo:  Udanganyifu, uchoyo, ubinafsi, wizi na ufitina
WAZAO LA LEO:- Kumbuka kumjali anayekujali hata kama yupo mbali nawe. Mpende anayekupenda hata kama hana kitu jali utu kuliko kitu.
NAWATAKIENI SIKU NJEMA

Friday, October 14, 2016

ZILIPENDWA KWELI NI TAMU...VAZI LA MAUA-MAUA NA MKANDA JUU....

Nimekumbuka sana zamani...ebu angalia hii picha. Sijui ilikuwa ni mtindo kusimama kwenye miti au maua..? Maana nimejiuliza hata jibu sijapata. Je? mnamfahamu huyu mdada?
IJUMAA NJEMA KWA ATAKAYEPITA HAPA!

Thursday, October 13, 2016

JIPE MOYO KAMWE USIKATE TAMAA KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA

"Nilikuwa naangalia mpira wa miguu katika uwanja wa shule. Nilipokaa, nilimuuliza kijana mmoja juu ya matokeo ya mchezo. Kwa tabasamu, alijibu "Wako mbele yetu 3-0"! Nikasema, Kweli!! Mbona huonekani kukata tamaa.
"Kukata tamaa? "Yule mvulana aliuliza kwa mshangao.... Kwanini nikate tamaa wakati bado refa hajapuliza kipenga cha mwisho? Nina imani na timu yangu na meneja wa timu; Nina hakika tutashinda! Na kweli, mchezo uliisha 5-4 timu ya kijana ikiwa mbele! Alinipungia mkono taratibu, na tabasamu zuri akiondoka uwanjani; nilishangaa,mdomo wazi, ujasiri mkuu kiasi hiki; nilipenda alivyojiamini ;  Nilipofika nyumbani usiku ule, swali lake lilizidi kuja kwangu zaidi.
"Kwanini niogope wakati refa hajapuliza kipenga cha mwisho?" Maisha ni kama mchezo. Kwanini ukate tamaa wakati Mwenyezi Mungu ndiye meneja wako? Kwanini ukate tamaa wakati kungalipo uhai ndani yako? Kwanini ukate tamaa wakati kipenga chako cha mwisho bado hakijapigwa? Ukweli ni kwamba watu wengi hujipulizia wenyewe vipenga vyao vya mwisho. Lakini madamu ungalipo uhai, hakuna kisichowezekana muda haujakuacha. 
Nusu kipindi si kipindi kizima na ratiba ya Mungu kwa mwanadamu si ratiba ya mwanadamu kwa Mungu.
Usijipulizie kipenga chako cha mwisho wewe mwenyewe.
UJUMBE- Maisha ni changamoto  ambapo pia ni kama mchezo...twapaswa kuwa jasiri na kujiamini.

Wednesday, October 12, 2016

LEO TWENDE NA ZILIPENDWA - SHAURI YAKO


JE? UNAUKUMBUKA HUU PIA KASONGO

NIWATAENI SIKU NJEMA ...KUMBUKENI TUPO PAMOJA.

Tuesday, October 11, 2016

Monday, October 10, 2016

TUANZE WIKI HII NA KUTEMBELEA KWETU UNGONINI SONGEA NA VITU VYAO VYA ASILI

 Kitanda cha ngozi
Na hapa ni NGOMA 
Upitapo Songea.Karibu sana katika nyumba ya makumbusho utapenda... 

Friday, October 7, 2016

NIMEKUMBUKA ZILIPENDEA...JUMAA NJEMA!

Jamani tukimbie tutachelewa ....nakumbuka jinsi  tulivyokuwa tukipata viboko kwa ajili ya kuchelewa shule....

Tuesday, October 4, 2016

SAMAKI WA NYASA ....CHAKULA AKIPENDACHO KAPULYA WENU:-)

Hawa ni samaki walionikuza mimi ....wanaitwa "magege" ni watamu sana. Nimekumbuka sana nyasa na hiki chakula

Monday, October 3, 2016

KILIMO CHA PILIPILI NA VINGINEVYO KWA KUTUMIA MAKOPO


 Hapa ni pilipili mbuzi 
 na hizi zinafanana ila ni kubwa kidogo 
 Hapa ni pilipili hoho tayari kwa kula sasa:-)
 Hizi pilipili zinafanana na pilipili hoho..yaani hazina makali sana kama kichaa na mbuzi
 Na hapa ni nyanya maana huwezi kula pilipili tu  hasa kwa kachumbali nk
Na mwisho zileee zabibu zetu nazo zimeiva na sasa ni raha tu...kwa hiyo ndugu zanguni karibuni tule pamoja ...si mnajua ule msemo usemao kulima mmoja ila kula wengi.... JUMATATU NJEMA!