Friday, October 14, 2016

ZILIPENDWA KWELI NI TAMU...VAZI LA MAUA-MAUA NA MKANDA JUU....

Nimekumbuka sana zamani...ebu angalia hii picha. Sijui ilikuwa ni mtindo kusimama kwenye miti au maua..? Maana nimejiuliza hata jibu sijapata. Je? mnamfahamu huyu mdada?
IJUMAA NJEMA KWA ATAKAYEPITA HAPA!

4 comments:

NN Mhango said...

Kumbe dada ulianza mambo ya mitindo kitambo hadi unamechisha na mazingira! Umetokelezea haswa.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango umeona mbali sana wala sikufikiria hilo la kumechisha mazingira na mavazi..Hapo ilikuwa muda kidago wakati wa ujana wangu...miaka ileeee. Ahsante kuona nimetokezea:-)

Penina Simon said...

Safi sana halafu siku hizi zimerejea na zinaonekana safi sana.
Sijui tuliachaje kuvaa magauni sasa hv ndiyo mishono ya nguvu

Yasinta Ngonyani said...

Dada P..ni kweli yaaani nimelitamani kweli hilo vazi halafu na huo mtindo wa nywele:-)