Friday, November 30, 2012

TUNAKUMBUKA VIFAA HIVI VYA KUKOBOLEA NAFAKA ZETU TANGU HAPO KALE MPAKA SASA?!!!

Hapo kale kupata ugali uwe wa ulezi, mtama,mahindi au muhogo hiki ndo kilikuwa kinu cha kusagia ili kupata unga. Kama nakumbuka vizuri juzi tu nimeona huko India bado wanatumia kusagia mchele ili kupata unga wa mchele........
 
 Na baadae kikagundulika kinu kwa kukobolea nafaka na pia kupata unga kama vile wa muhogo nk.--
..na baadaye baadaye tukapata mashine ...na mikono ikawa inapumzika kidogo. Sijui  wenzangu mie binafsi nilikuwa mzembe sana hasa kukoboa mahindi. ...je? kuna kifaa kingine zaidi ya hapa unafiri?

Thursday, November 29, 2012

Aina Mpya ya Utapeli Bongo:- Habari ya kweli iliyotokea wiki iliyopita.

Kuna dada mmoja anasoma chuo buguruni na pia ni mfanyakazi hivyo jioni akitoka kazini ndipo huenda shule.Sasa akiwa njiani kuelekea chuo akapigiwa simu na mtu asiyemfahamu akajitambulisha kwamba yeye ni daktari wa lugaro hosp na kumuulizia habari za mwanae ambae alishawahi kwenda kumtibu pale na chakushangaza zaidi akataja mpaka aina na rangi ya nguo aliyovaa siku ile alipokwenda hapo hospitali na yote yalikuwa kweli.

Na zaidi akamwambia najua sasa hivi unaelekea chuo buguruni na kweli ilikuwa hivyo, lakini mwishoni akamweleza kwamba kuna mambo anataka kujua kujua kuhusu hicho chuo hivyo nae anaelekea huko hivyo akifika tu atamtafuta. Kwa muda wote huo huyo dada hakuweza kabisa kumkumbuka ila akajipa moyo kwamba yamkini huyo mtu atakuwa anamfahamu vizuri.

Baada ya kutoka chuo akiwa na wenzake watatu akawa anawasimulia habari za huyo mtu ndipo simu yake ikaita,kupokea yule mtu akamwambia akuona uko na wenzio wawili mnavuka barabara na kumueleza jinsi alivyovaa sasa wenzie wakasema huyo mtu anakufahamu haiwezekani hapa tupo watatu kweli na ameweza kukutambua. Kisha huyo mtu akamwelekeza mahali alipo ambapo haikuwa mbali na barabara.

Lakini alipomtazama hakumfahamu kabisa, basi akampa mkono kumsalimia, baada ya hapo hakujitambua na zaidi alijikuta yuko maeneo ya chuo kikuu cha DSM akiwa hoi. Kuangalia simu na kila kitu chake kilikuwa salama na hakufanyiwa kitu chochote, kwa bahati kulikuwa kuna ndugu yake anasoma chuo hivyo akawasiliana nae ili kupata msaada ikabidi awahishwe mwananyamala hosp lakini ikaonekana sumu iliyotumika ni kali na dawa yake wanayo regency hosp,hivyo akawahishwa regency na kupata matibabu.

Baada ya ufahamu kumrudia akakuta mtu huyo kachukua pesa zote kwenye mpesa,tigo pesa na bank ( NMB na CRDB) kiasi cha milioni 3, hivyo inawezekana walipompa sumu alitaja password pasipo kujijua.

Na bank walipotazama kwenye ATM Camera waliona picha ya huyo mtu na yeye alimkumbuka vizuri, lakini polisi Kijitonyama wakakiri kwamba kesi hizo sasa hivi zimetokea mara nyingi na huo mtandao ni mkubwa, walipoenda kwenye usajili wa simu walikuta ni huyo huyo na jina lake ndilo alilojitambulisha.Ingawa polisi wameshindwa kumkamata.

Akiwa kituo cha polisi mara huyo mtu akampigia simu akimwambia kumbe wewe ni muoga sana tutakurudishia pesa zako’’. Sasa kumbe wanachofanya wanakuambia tutafutie mtu ambae unahisi ana pesa kuliko hizi halafu tukifanikiwa tutarudisha pesa zako’’ hivyo inawezekana nae kuna mtu anaemjua alifanyiwa hivyo akaamua kumtaja yeye.

JAMANI HEBU SOMENI NA IKIWEZEKANA TUMENI HII TAARIFA TO AS MANY PEOPLE AS POSSIBLE.
Habari hii nimeipata hapa

Hivi Kwa Nini tunacheka?


Kicheko ni njia ya mawasiliano, ambayo yanaonyesha ni ukaribu gani tunao na watu wengine. Hata kama mtu anacheka peka yake, kuna tafiti zinaonyesha kwamba hata ukiangua kicheko mara 30, kama tupo pamoja na watu wengine, kuliko tunapokuwa peke yetu.

Kwa kawaida kicheko kinaonyesha ni upamoja gani gani tunao na wale tunaocheka nao. Ni kinyume na nyani ambao wanacheka tu kwa furaha, kicheko cha binadamu kinaweza pia kumchokoza mtu , kicheko kinaweza kuwa cha dhihaka au hisia nyingine. Kicheko wakati mwingine kinaweza kuwa ni njia ya kupata huruma au huzuni pia.

Inaonekana kwamba sehemu kadhaa katika ubongo zimetawaliwa na kicheko. Mwaka 2001 huko Uingereza katika majaribio yao ya NMR X-RAY waliweza kuona sehemu ndogo ya kulia na kushoto ya paji la uso ilionekema ni zenye vichekesho/utan zaidi, lakini hizo aina za tofauti za utan hazifanyi kazi kwenye ulande moja.

Wakati utani unaposomeka, kwa kupima walakini upande mwingine wa mbele wa paji la nyuso kama ilikuwa ya kuchekesha. Inaonyesha kuna chumba cha tatu cha ubongo juu ya paji la nyuso. Ambayo kicheko kinakuja chenyewe.

Pia inaonyesha kuwa mwaka 1998 huko USA, wakati wao wenye vifaa vya umeme vilimfanya msichana wa miaka 16 bila shida kuangua kicheko. Chanzo Illustrerad Vetenskap nr 15/2010.

Wednesday, November 28, 2012

UPUMZIKE KWA AMANI HUSSEIN RAMADHANI A.K.A SHARO MILIONEA!!


SISI TULIKUPENDA LAKINI MUNGU ALIKUPENDA ZAIDI UPUMZIKE KWA AMANI TUTAKUKUMBUKA DAIMA.

NIMEIPENDA SKETI HII/ MREMBO WA LEO!!!


 
Sketi hii nimeipenda sana ni ndefu na ya heshima ...hii ni mimi!!!!:-)
 

Tuesday, November 27, 2012

MTAZAMO WA MAISHA YA ZAMANI NI TOFAUTI KABISA NA MAISHAYA SASA!!!

Habari hii nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mafanikio nami nimeipenda na nimeona nisiwe mchonyo pia ni vema kujadili kwa pamoja...pamoja daima...
---------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kwanini nasema hivyo:-  Nasema hivi nikiwa na maana yake, ni kwamba  zamani maisha yalikuwa mazuri na mepesi na yenye khekima kwa wakubwa na wadogo. Vyakula vilikuwa vingi pesa ilikuwa ina thamani. Ikiwa na maana watu waliishi kwa mapenzi mema tena sana. Watoto wakike walifundishwa jinsi ya usafi, kupika, kujiepusha na vitu vya anasa na kadhalika. Na pia wazee waliwapenda wajukuu wao. Wakati wa jioni walikaa nao wakiota moto wakiwa wanawasimulia hadithi nzuri ambazo zilikuwa na mafunzo na pia watoto waliburudika sana. Pamoja na kuwa palikuwa na uhaba wa huduma za jamii ila watu waliishi kwa kula vyakula asilia, na kutumia dawa za miti shamba....,,, Namalizia kusema MAISHA YA ZAMANI YALIKUWA NI BORA KULIKO YA SASA!!! Napenda kusema tena:- Maisha ya kisasa ni tofauti na zamani kwanini nasema hivyo. Maana yake siku hizi watu sio vijana sio wazee wanapenda mambo ya kisasa NA PIA YA KUIGA. Utakuta  wanavaa mavazi tofauti na zamani, wanapenda anasa sana kuliko vitu vinginne, hawapendi kukaa na watoto wao kama wazee wa zamani, hawapendi vitu asilia....! Je? Kuna ukweli kuwa  maisha ya zamani ni bora? KILA LA KHERI!!!!

Monday, November 26, 2012

MAGUNIA YA MKAA KANDOKANDO YA BARABARA..TUKUMBUKE KUPANDA MITI PIA!!!

Hapa ni magunia ya mkaa kando ya barabara yanasubiri wateja/wanunuzi. Kwa namna hii ongezeko la ukataji miti ya asili kwa ajili ya mkaa linachangia sana uhalribifu wa mazingira sehemu nyingi nchini. Basi afadhali tungekuwa tunakata miti na kupanda tena....JUMATATU NJEMA.

Saturday, November 24, 2012

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWEPO/ISHIA IJUMAA YA JANA TULIPATA WAGENI TOKA NYUMBANI TANZANIA!!!

Hakika siku ya jana ilikuwa siku ya furaha sana kwetu. Kama mzaa vile baba wa nyumba akanipigia simu na kusema nina wageni hapa andaa msosi twaja. Nikafanya hivyo muda si mrefu wakatua nyumbani. Wageni kutoka nyumbani tena NYUMBANI kabisa. Kutoka kushoto ni kaka Ludovick Chahally, katikati ni dada Elizabeth Mahinya wao ni mke na mume..na halafu mwisho ni mimi mwenyewe kapulya:-) Nimesisitiza kuwa wanatoka NYUMBANI kwa vile dada Elizabeth anatoka SONGEA pia MNGONI..tuliongea kingoni we acha tu:-) Ni furaha sana kuonana na watu wa nyumbani na kubwa zaidi mnaotoka mkoa mmoja.

Nawatakieni wote JUMAMOSI NJEMA SANA. NDUGU SI LAZIMA AWE BABA NA MAMA MMOJA. HILO MIE NAAMINI KABISA. TUPO PAMOJA DAIMA.

Friday, November 23, 2012

TUPO PAMOJA NA NAPENDA KUWATAKIENI MWANZO MWEMA WA MWISHO WA WIKI!!!

Nawatakieni wote mtaopita hapa mwisho mwema wa wiki na kumbukeni wote mnapendwa: ngoja tu tumalizie na masai raggae :-)

IJUMAA NJEMA!!!

Wednesday, November 21, 2012

MARA YA MWISHO KULA CHAKULA/MAGIMBI ILIKUWA KIHESA -NJOMBE KWA CHAI YA RANGI

Hapa ni magimbi kabla hajamenywa na ....

....hapa tayari yamemenywa na kuchemshwa tayari kwa kula. Magimbi unaweza kula kama chakula cha asubuhi, mchana au jioni. Ila mimi nimeyatamani sana leo na ningeyale kama chakula cha asubuhi hii ya leo kwa....
.

......kikombe hiki cha chai ya rangi  ila sasa.... haya ngoja nile kwa macho. Je? wewe mara ya mwisho ni lini umekula magimbi?

Tuesday, November 20, 2012

HAPA SIJUI PAPOJE? NAONA HII IWE PICHA YA WIKI HII!!!

Sijawahi kuona watu wakifunga kuku kamba..hapa naona dogo amesha chagua kitoweo cha sijui mchana au jioni?  au labda ndo kapata kitu cha kuchezea? MUWE SALAMA WOTE !!!

Monday, November 19, 2012

JUMATATU HII TUNANZE NA SWALI HILI? NINA KASORO GANI?

Jerome na Sesilia walikuwa wamemaliza miaka mitatu tangu waoane. Jerome alikuwa fundi wa saa. Alikuwa amejenga duka lake dogo nje ya nyumba yao. Kila siku, isipokuwa Jumapili, watu waliweza kumkuta hapo. Alipenda kuimba wakati akifanya kazi na kama hakuwa akiimba, basi redio ilikuwa ikicheza muziki kwa sauti kubwa na safi kwa wapita njia wote kusikia.

Watu waliwafahamu kama watu wawili wenye raha. kabla ya kufunga ndoa, Sesilia hakuwahi kuishi mjini. Miaka yake ya kwanza nyumbani mwao mpya ilimshangaza kwa vile alivyowaona watu wakiharakisha kwenda huku na kule. Katika kijiji chake alimokuwa, maisha yalikuwa tofauti sana na tena ya polepole zaidi. Lakini hapa kelele zilikuwa nyingi mno, milio ya honi hasa za watu wenye taksi, na sauti za watu wakiitana.

Lakini alikuwa anafurahi kuvumilia yote haya kwa ajili ya ndoa yake kwani alimpenda sana Jerome. Alijua ya kwamba Jerome alimpenda pia. Hakuongea sana juu ya jambo hilo, lakini Sesilia aliweza kuliona kwa namna alivyokuwa anamwangalia, katika utaratibu wa sauti yake na katika kumtunza kwake. Alizoea kuimba alipokuwa akifagia nyumba. Huko nje pia Jerome naye alikuwa akiimba na sauti zao kwa pamoja ziliwaambia watu waliopita karibu kwamba hiyo ilikuwa ndiyo nyumba yenye raha.

Siku moja, Sesilia akiwa sokoni, alisikia jambo lililomtia uchungu sana. Lucy, kutoka katika kijiji chake, alimwambia kwamba jioni iliyopita alikuwa amemwona Jerome akiingia katika nyumba ya wageni.

"Kwa nini lakini?" Sesilia aliwaza. "Bila shaka siyo kuwa na mwanamke mwingine" Ndiyo Lucy alikuwa na hakika alikuwa ndiye Jerome. Sesilia alijaribu kujisadikisha kwamba bila shaka haikuwa hivyo lakini hakuweza kufukuza wasiwasi mkubwa uliokuwepo moyoni mwake. Alifahamu kwamba watu wengi kati ya watu wake hawakuona kwamba ni jambo baya sana kwa mtu wa ndoa  kuwatembelea wanawake wengine. lakini aliamini ya kwamba ndoa yao ilikuwa tofauti na ndoa nyingine nyingi.

Aliamua kutosema neno lolote. Atasubiri na kufungua macho. Jerome alionekana kama hali yake ni ya kawaida lakini hapa na pale Sesilia alitambua badiliko katika mwenendo wake kwake. Ama, haya yalikuwa ni mawazo yake tu? hakuweza kusema.
Jioni moja, baada ya chakula cha jioni, Jerome alimwambia Sesilia kwamba alikuwa anakwenda kutembea. "Nimeketi kutengeneza saa kutwa kucha, na nisiponyosha miguu ninahofu nitasahau namna ya kutembea", alimwambia haya haku akifunga mlango wa duka lake.
Alipomfuata nyuma barabarani, Sesilia aliona aibu ya kufanya hivyo. Lakini ilimbidi kujua. Labda alikuwa anakwenda kwa wanawake. Walikuwa wanaelekea kwenye nyumba ambayo Lucy alikuwa amemwelezea. hata hivyo mtu aliyeweza kuwa na sababu nyingine za kutembea kwenye mtaa huu. Labda Jerome hakujali alikuwa anakwenda wapi.

Moyo wa Sesilia ulisimama alipomwona Jerome akiingia kwa mlango wa nyuma wa baa /nyumba ya wageni
maalumu ambayo waliishi wanawake. Kumbe, Lucy alikuwa amesema kweli. Akijawa na uchungu, huzuni na hasira, Sesilia alirudi nyumbani polepole. Alijiuliza: "Nina kasoro gani? kwanini Jerome ana haja ya kumwendea mwanamke mwingine? Kwa nini hakai nami? Nina kasoro gani?"
Sesilia hakuweza kujua kilichokuwemo akilini mwa Jerome. Hakuweza kujua kwamba Jerome alikuwa amezoea raha aliyokuwa nayo na kwamba sasa alitaka kuonja kitu kipya, alitaka kugundua mambo mapya na pia alitaka watu wapya wamtosheleze. Sesilia hakujua hayo lakini aliazimia atamfundisha Jerome asikose uaminifu tena----yaani hata naye Sesilia atapata mpenzi.
Je? Unafikiri nini kilimfanya Jerome afanye kama alivyofanya?


Sunday, November 18, 2012

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE MTAKAOPITA HAPA!!!


Hakuna binadamu aliyekamilika. NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA .

Saturday, November 17, 2012

NAPENDA KUWATAKIENI WOOTE JUMAMOSI HII IWE YENYE FURAHA NA UPENDO!!!!

JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE NA TUKUMBUKANE KWANI SOTE NI WATOTO WA BABA MMOJA. upEnDo DaImA.....!!!!!!!!!!!!

Friday, November 16, 2012

BAADA YA KAZI YA KAZI KWA JUMA NZIMA KWA WENGINE BASI KAA CHINI NA SIKILIZA UJUMBE HUU...NA UWE NA MWISHO WA JUMA MWEMA.....ZILIPENDWA!!!


NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA KUNA WENGI  WATAPUMZIKA MPAKA JUMATATU NA WALE WANAO ENDELEA NA KAZI JUMAMOSI NA JUMAPILI BASI NIWATAKIENI KAZI NJEMA MOJAWAPO NIKIWA MWENYEWE....WOTE MNAPENDWA...KAPULYA

Thursday, November 15, 2012

UJUMBE WA LEO!!!

Kulazimisha/kubembeleza kitu/mtu siyo vizuri ..kama Mungu amepanga basi kitatokea/itatokea tu........
NAWATAKIENI ALHAMIS NJEMA WOTE:-)

Wednesday, November 14, 2012

UMESHAWAHI KUCHEZA MCHEZO HUU?!!

Maisha siku zote huwa tofauti toka ulipokuwa mtoto hadi kufikia uzeeni. Hatua hii hupitia mambo mbalimbali haswa za kimechezo. Nakumbuka nilipokuwa mtoto tulicheza michezo mingi ya heshima tofauti na watoto wa sasa hivi.  Haya yote yanasemekana ni kutokana na utandawazi ambao huwajengea watoto ufahamu zaidi.
Huu ni mchezo wa Kuruka kamba ambao tuliucheza utotoni na pia kiafya una umuhimu. Michezo mingine ni Kombolele(Mchezo wa kujificha), Utengenezaji wa magari, Ndege wakati wa mavuno, Midoli ya kutengeneza,  Kula mbakishie baba, Kutengeneza vitu mbalimbali kwa kutumia udongo, ukutiukuti, Kioo Kioo, mdako mpira (lede ledesta) ,Kujipikilisha....................................pia katika mchezo huu wa kuruka kamba nakumbuka tulikuwa tukiimba  hivi:- Kamwambie baba baba sisi tunacheza cheza hatuogopi fimbo fimbo mtoto acha kuningínikax2.....
Sijui ndo uzee naona kama nimesahau basi tusaidiane kukumbushane ......!!!!!!!!
Tafakari juu ya mtoto wako ingawa sasa hivi tunawanunulia vitu vya kuchezea ila wanavitumia ipasavyo na halafu vinakuwa vingi mno. Nimekumbuka sana michezo hii ya utotoni ..je? nawe unakumbuka kitu?
MAISHA NA MAFANIKIO INAWATAKIA WOTE JUMATANO NJEMA SANA!!! DAIMA PAMOJA.




Tuesday, November 13, 2012

NIMEONA TUBAKI KIDOGO HAPA SONGEA:- HAPA NI PIKIPIKI KWA AJILI YA KUWABEBA AKINA MAMA WAJAWAZITO KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA RUVUMA!!!!


Nimeupenda ubunifu huu, labda unaweza kuokoa maisha ya akina mama wengi....
Hizi ni pikipiki maalumu kwa ajili ya kubebea wajawazito toka maeneo ya vijijini na kuwafikisha hospitalini.
Nimependa hii kwa kweli kwasababu wajawazito huwa wanapata taabu sana na mwishowe hufa au mtoto kufa.

Monday, November 12, 2012

TURUDI TENA SONGEA KWETU:-UVUNAJI WA MITI KATIKA MILIMA YA MATOGORO KWASABABISHA KUKAUSHA MTO RUVUMA!!!

Na Daniel Mbega, Songea
 MVUA zilikuwa zikimtendea haki Josephat Komba, mkulima katika kijiji cha Ndilima Litembo wilayani Songea, wakati pepo za kusi zilipovuma vyema na hivyo shamba lake la mpunga kupata maji ya kutosha yaliyompa mavuno mengi. Lakini hana uhakika kama atapata bahati kama hiyo msimu ujao.
“Zamani, hatukuwa na mashaka kuhusu hali ya hewa,” anasema Komba, akiwa shambani kwake kilometa kadhaa kutoka Songea mjini. “Lakini hivi sasa, tatizo ni kubwa mno.”
Komba anaitazama Milima Matogoro kwa masikitiko, na kujiuliza kama mabadiliko hayo ya hali ya hewa yameletwa na Mungu au wanadamu.
“Tumesikia mara kadhaa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, lakini nikwambie ukweli, miaka ya nyuma milima hii unayoiona hapa ndiyo ilikuwa mkombozi wetu. Tuliitegemea sana kwa ajili ya kuleta mvua, sasa hatujui kama ni laana ya Mungu au ni binadamu ndio tunaosababisha majanga haya,” anasema.
Komba anasema, zamani walikuwa wakipanda kwa wakati na mvua zilinyesha katika kipindi kile kile. “Lakini tangu walipoanza kufyeka miti kwenye milima hii, kila kitu kimebadilika. Nadhani wameikasirisha miungu.”
Misimu kadhaa iliyopita, mvua zikaanza kuadimika. Mara kadhaa mpunga wake ulikomaa bila unyevu; karibu theluthi ya mimea yake ilikauka kwa ukame na hata Mto Ruvuma ambao amekuwa akiutegemea umekuwa hauna maji ya kutosha hata nyakati za masika.
Mabadiliko hayo ya ajabu ya hali ya hewa ndiyo ambayo wanasayansi wa mazingira wanaamini kuwa ni madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa. Wakati mwingine kunaweza kuwa na ukame, lakini msimu mwingine mvua zinaweza kuwa nyingi kiasi cha kuleta mafuriko hivyo kushindwa kulima.
Komba analalamika kwamba, uchomaji wa moto kwenye msitu wa milima hiyo ni sababu nyingine inayoondoa hali ya asili ya milima hiyo ya Matogoro na hivyo kuleta wasiwasi mkubwa kwamba mito mikuu kama Ruvuma, Luhira na Luwegu itatoweka katika miaka michache ijayo.
Sehemu kubwa ya msitu wa Milima ya Matogoro imebakia vipara kutokana na uvunaji wa miti ya kigeni (exotic trees) kama Misindano (Pines) na Mikaratusi (Eucalyptus) ambayo wataalamu wa hifadhi ya vyanzo vya maji wanasema inayonya maji mengi.
Mhandisi Jaffari Yahaya wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Manispaa ya Songea (SOUWASA) anasema kwamba kuwepo kwa ukosefu wa maji wakati wa kiangazi katika Manispaa ya Songea kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na aina ya miti ambayo ipo katika misitu ya milima Matogoro ambayo hunyonya maji kwa kiwango kikubwa kwa kipindi cha mwaka
Soma zaidi hapa

TUANZE JUMATATU HII KIHIVI ...JUA...!!!

Sikumbuki ni lini nimeona jua likichomoza kama hili hapa. Au sijui linazama hapa? kama ule wimbo wa mchaka mchaka.....Jua lile litelemke mama ...litelemke mama litelemke....mmmhhh ila hapa naona linachomoza angalia tu mionzi yake,,,au Wenzangu mnasemaje?...Haya JUMATATU NJEMA...!!!

Saturday, November 10, 2012

JUMAMOSI YA LEO NAPENDA KUSEMA:- AHSANTE MAMA MUNGU AKUPE KHERI DAIMA!!!

 
AHSANTE MAMA MUNGU AKUPE KHERI DAIMA
 
Nimeyapenda maandishi haya kwenye kanga hii na hapa si kwa ajili ya mama yangu tu nawaombeni wote ambao mnaweza kuwashukuru akina mama basi chukueni nafasi hii na kuwashukuru kwani
HAKUNA KAMA MAMA. JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE!!! NIPO  NANYI!! 

 

Friday, November 9, 2012

UJUMBE WA IJUMAA YA LEO NI:-.......

Riziki ni mdudu popote hutua!
MUWE NA IJUMAA NJEMA NA MWISHO WA JUMA MWEMA....KAPULYA!!!

Wednesday, November 7, 2012

NIPO INGAWA SIPO ILA NIPO!!!!

Kutokana na taarifa niliyowapa hapo jumapili basi ndiyo maana nitakuwa kidogo sionekani sana hapa ila nipo na pia napenda kutoa SHUKRANI ZA DHATI kwa wale wote waliuotufariji. TUPO PAMOJA NA MUNGU AWAZIDISHIE UPENDO. MUWE SALAMA WOTE!!!

Sunday, November 4, 2012

JUMAPILI YA LEO NAPENDA KUSALI SALA HII KWA MAREHEMU WOTE AKIWEPO MAMA MKWE WANGU AMBAYE KATUACHA JANA!!!

Na tuwaombee marehemu
Ewe Baba Mwenyezi, Mpaji wa maisha na afya, twakuomba uwaangalie kwa rehema marehemu pia wagonjwa wote, hasa wao wanaotakiwa maombi yetu, ili kwa baraka yako juu yao, na juu ya wao wawatumikiao, ikiwa mapenzi yako warudishiwe afya yao ya -mwili na ya roho,na pia marehemu wote wastarehe kwa amani, nao wakutolee shukrani katika kanisa lako takatifu; kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Amina.
JUMAPILI NJEMA KWA WOTE NA UPENDO UTAWALE NDANI YA MIOYO YENU.

Friday, November 2, 2012

NAPENDA KUWATAKIENI MWANZO MWEMA WA MAPUMZIKO !!!

There some place in this world maybe left to be unvisted, there som worlds maybe left to be unsaid, there some story maybe left to be unnarrated, but the special one as you, you will never left to be unrembered. WOTE MNAPENDWA SANA NA IJUMAA /MAPUMZIKO MEMA KWA WOTE.
EBU PILIPILI&KELMA WAMALIZIE NA UGALI....

PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA......!!