Wednesday, November 14, 2012

UMESHAWAHI KUCHEZA MCHEZO HUU?!!

Maisha siku zote huwa tofauti toka ulipokuwa mtoto hadi kufikia uzeeni. Hatua hii hupitia mambo mbalimbali haswa za kimechezo. Nakumbuka nilipokuwa mtoto tulicheza michezo mingi ya heshima tofauti na watoto wa sasa hivi.  Haya yote yanasemekana ni kutokana na utandawazi ambao huwajengea watoto ufahamu zaidi.
Huu ni mchezo wa Kuruka kamba ambao tuliucheza utotoni na pia kiafya una umuhimu. Michezo mingine ni Kombolele(Mchezo wa kujificha), Utengenezaji wa magari, Ndege wakati wa mavuno, Midoli ya kutengeneza,  Kula mbakishie baba, Kutengeneza vitu mbalimbali kwa kutumia udongo, ukutiukuti, Kioo Kioo, mdako mpira (lede ledesta) ,Kujipikilisha....................................pia katika mchezo huu wa kuruka kamba nakumbuka tulikuwa tukiimba  hivi:- Kamwambie baba baba sisi tunacheza cheza hatuogopi fimbo fimbo mtoto acha kuningínikax2.....
Sijui ndo uzee naona kama nimesahau basi tusaidiane kukumbushane ......!!!!!!!!
Tafakari juu ya mtoto wako ingawa sasa hivi tunawanunulia vitu vya kuchezea ila wanavitumia ipasavyo na halafu vinakuwa vingi mno. Nimekumbuka sana michezo hii ya utotoni ..je? nawe unakumbuka kitu?
MAISHA NA MAFANIKIO INAWATAKIA WOTE JUMATANO NJEMA SANA!!! DAIMA PAMOJA.
7 comments:

Anonymous said...

kuna na mchezo wa baba na mama!??,mchezo wa kidali......na mingine mingi

Ester Ulaya said...

bilinge yooyooyooo bilinge yooyooyoox2 ingia kati tuyaone maringo yako bingili bingili mpaka chiniiiiiiiii...........umenikumbusha enzi hizo, watoto wa siku hizi wanamiss sana hayo mambo, unatumwa dukani unaenda unaimba usisahau ulichotumwa na ringi lako hulisahau.....kucheza msita(mdako), kucheza goroli...yaani vingi mno, vilikuwa vinatusaidia uwezo wetu wa kufikiri

sam mbogo said...

Hakika michezo ya utotoni ni mizuri . kaka s.

ray njau said...

Wazazi—Waongozeni Watoto Wenu
==============================
“Zamani tulikuwa na wasiwasi kwamba watoto walikuwa wakitumia wakati mwingi wakitazama televisheni. Sasa tuna michezo ya video, kompyuta, na simu za mkononi. Watoto hawawezi kujidhibiti wasitumie vitu hivyo kupita kiasi na kwa sababu hiyo ni kana kwamba wanakuwa waraibu wa teknolojia . . . Ubongo wao huzoea kusisimuliwa na mambo wanayoona na kusikia—na wanapokosa vitu hivyo, hawajui la kufanya.”—Mali Mann, M.D.

TUNAISHI katika ulimwengu “uliounganishwa” kwa sababu ya maendeleo katika teknolojia ya mawasiliano na Intaneti. Vijana wengi hawawezi kuondoka nyumbani bila vifaa vyao vidogo vya kuchezea muziki au video au simu zao za mkononi. Na kadiri vifaa hivyo na vinginevyo vinavyozidi kuwa vya hali ya juu, vyenye matumizi mengi, na kupatikana kwa bei nafuu, ndivyo vifaa vya mawasiliano ambavyo tayari viko kwa wingi vitakavyozidi kuongezeka na kufanya iwe vigumu hata zaidi kwa wazazi kuwasimamia, kuwazoeza, na kuwatia nidhamu watoto wao.

Wazazi wanaweza kukabiliana na hali hiyo iwapo watafanya mambo mawili muhimu. Kwanza, watambue ukweli wa maneno yafuatayo yanayopatikana katika Biblia kwenye Methali 22:15: “Mtoto hupenda mambo ya kijinga moyoni, lakini fimbo ya nidhamu humwondolea hayo.” (Biblia Habari Njema) Pili, waelewe kwamba teknolojia inaweza kuwa na uvutano mzuri au mbaya kwa watoto wao, na wajitahidi kuwasaidia waitumie kwa njia nzuri.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina hapo juu! kweli enzi zile kulikuwa na michezo mingi na mpaka sasa ipo ila watoto wa siku hizi hawaijali au labda ni kosa letu hatujawafundisha kama tulivyofundishwa....
Da´Mdogo Ester! Zamani ilikuwa safi sana halafu sasa kumbuka wakati kuna mbalamwezi wote mmekusanyika wakati wa usiku na kusikiliza hadithi lakini siku hizi hata kula pamoja ni kaaaazi kwelikweli....ila mweh mboga zimeungua kweli wakati ule.

Kaka Sam! Ni mizuri haswa:-)

Kaka Ray! Umenena la msingi pia hapa inategemea na wapi mtu unatoka na umelelewaje. Mjini au kijijini. Napenda kusema kijijini kutakuwa bado na baadhi ya michezo bado inachezwa na watoto..Watoto wanahitaji kuwa watoto na hii michezo si michezo tu ni moja ya kujifunza kuishi....

John Mwaipopo said...

siku hivi mambo ni video games tu

emu-three said...

Kila kitu na wakatu wake, lkn tusipokuwa macho, michezo kama hiyo, mila na desturi zetu, vitakuwa adimu kwetu!