Tuesday, November 13, 2012

NIMEONA TUBAKI KIDOGO HAPA SONGEA:- HAPA NI PIKIPIKI KWA AJILI YA KUWABEBA AKINA MAMA WAJAWAZITO KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA RUVUMA!!!!


Nimeupenda ubunifu huu, labda unaweza kuokoa maisha ya akina mama wengi....
Hizi ni pikipiki maalumu kwa ajili ya kubebea wajawazito toka maeneo ya vijijini na kuwafikisha hospitalini.
Nimependa hii kwa kweli kwasababu wajawazito huwa wanapata taabu sana na mwishowe hufa au mtoto kufa.

5 comments:

ray njau said...

Hakika ni msaada wenye tija kwa jamii yetu.

Emmanuel Mhagama said...

Ni kweli zaweza kuwa msaada. Lakini wasiwasi wangu ni huu; zinalenga kuwasaidia watu wa namna gani au watu wa mazingira gani. Maeneo mengi ya mjini huwa yana gari za wagonjwa, hata kama ni gari moja, lakini walao kwa kuwa matukio yanayohitaji Ambulance siyo mengi sana, kukiwa na gari moja linaweza kufanya kazi ya kutosha. Na hii sana sana ni kwa wale walio mjini na maeneo yanayozunguka mji. Wenye taabu kubwa kwa habari ya kubeba wagonjwa na watu wa maeneo ya vijijini. Kama pikipiki hizi zimekusudiwa kwa watu wa mjini, hii ni sawa ingawa ingawa bado ni upendeleo kwao maana kila kitu kinaishia mjini. Lakini kama zinalenga pia watu wa vijijini, huu ni usanii. Fikiria kwa barabara zetu za vijijini jinsi nyingi zilivyo shaghalabaghala, leo umembeba mama mjamzito na kumweka kwenye hiyo pikipiki, unapita nayo wapi kama siyo kumtakia ujifungue kabla ya wakati? Kama nia ni njea, hizo zibaki mjini halafu gari zile ziende vijiji. Ni mawazo yangu tu.

Rachel siwa Isaac said...

Kaka Mhagama nakuunga mkono!!!Jee Mjamzito ikitokea akajifungulia njiani kuna Mtu wa msaada pembeni?

Penina Simon said...

Mh!! Hawa wamependelewa sana, ndio kwanza naona kitu kama hicho wengine hubebwa na machela kwa kuomba msaada kwa vijana wenye nguvu au baiskeli hzi za kawaida miguu 2. kwa kweli wamama wanateseka sana yaani.

Justine Magotti said...

HIZO PIKIPIKI ZA WAJAWAZITO MADE FROM CHINA AU JAPAN