Thursday, November 29, 2012

Hivi Kwa Nini tunacheka?


Kicheko ni njia ya mawasiliano, ambayo yanaonyesha ni ukaribu gani tunao na watu wengine. Hata kama mtu anacheka peka yake, kuna tafiti zinaonyesha kwamba hata ukiangua kicheko mara 30, kama tupo pamoja na watu wengine, kuliko tunapokuwa peke yetu.

Kwa kawaida kicheko kinaonyesha ni upamoja gani gani tunao na wale tunaocheka nao. Ni kinyume na nyani ambao wanacheka tu kwa furaha, kicheko cha binadamu kinaweza pia kumchokoza mtu , kicheko kinaweza kuwa cha dhihaka au hisia nyingine. Kicheko wakati mwingine kinaweza kuwa ni njia ya kupata huruma au huzuni pia.

Inaonekana kwamba sehemu kadhaa katika ubongo zimetawaliwa na kicheko. Mwaka 2001 huko Uingereza katika majaribio yao ya NMR X-RAY waliweza kuona sehemu ndogo ya kulia na kushoto ya paji la uso ilionekema ni zenye vichekesho/utan zaidi, lakini hizo aina za tofauti za utan hazifanyi kazi kwenye ulande moja.

Wakati utani unaposomeka, kwa kupima walakini upande mwingine wa mbele wa paji la nyuso kama ilikuwa ya kuchekesha. Inaonyesha kuna chumba cha tatu cha ubongo juu ya paji la nyuso. Ambayo kicheko kinakuja chenyewe.

Pia inaonyesha kuwa mwaka 1998 huko USA, wakati wao wenye vifaa vya umeme vilimfanya msichana wa miaka 16 bila shida kuangua kicheko. Chanzo Illustrerad Vetenskap nr 15/2010.

5 comments:

2hmnzava.blogspot.com said...

Hakika kucheka ni sehemu ya afya!

Yasinta Ngonyani said...

2hmnzava.blogspot.com! nimewahi kusikia kuwa kuna watu wengine hawacheki kabisa je hao hawana afya?......

EDINA J KIBOMA said...

duu hao wasiocheka kabisa sijui kama nitaweza kukaa nao...mimi napenda kucheka...napenda kuwa nawatu wenye furaha...kucheka kuna faida kubwa kiafya...kuna mahala nilisoma kuwa eti mtu kila ukipiga mswaki asubuhi utabasamu kwenye kioo itakufanya uwe na mood nzuri kwa siku nzima... LOL....nadhan hao wasiocheka kabisa wanahitaji hilo zoezi.

Yasinta Ngonyani said...

Dada Edna! kwanza laribu tena maana ulipoteaaa. Nakubaliana nawe bila kucheka siku nzima kwangu kwa kweli itakuwa taabu sana. Nitajaribu hiyo ya kujiangalia kwenye kioo....

Anonymous said...

ogopa wasio cheka huwaga wanakuwa na uamuzi mbaya anawezakufanya kitu ukamshangaaaa