Saturday, November 24, 2012

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWEPO/ISHIA IJUMAA YA JANA TULIPATA WAGENI TOKA NYUMBANI TANZANIA!!!

Hakika siku ya jana ilikuwa siku ya furaha sana kwetu. Kama mzaa vile baba wa nyumba akanipigia simu na kusema nina wageni hapa andaa msosi twaja. Nikafanya hivyo muda si mrefu wakatua nyumbani. Wageni kutoka nyumbani tena NYUMBANI kabisa. Kutoka kushoto ni kaka Ludovick Chahally, katikati ni dada Elizabeth Mahinya wao ni mke na mume..na halafu mwisho ni mimi mwenyewe kapulya:-) Nimesisitiza kuwa wanatoka NYUMBANI kwa vile dada Elizabeth anatoka SONGEA pia MNGONI..tuliongea kingoni we acha tu:-) Ni furaha sana kuonana na watu wa nyumbani na kubwa zaidi mnaotoka mkoa mmoja.

Nawatakieni wote JUMAMOSI NJEMA SANA. NDUGU SI LAZIMA AWE BABA NA MAMA MMOJA. HILO MIE NAAMINI KABISA. TUPO PAMOJA DAIMA.

8 comments:

sam mbogo said...

umewapikia nini wageni wako. safi sana unaonekana u mkarimu kwa wageni.hongera,pia nawapa pole nahali ya hewa waliyo ikuta(baridi). jumamosi njema wewe na wageni wako na familia yako pia. sisi huku uk ni mafuriko tu! mvua zina nyesha balaa. kaka s

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! Tulifurahi kweli kwa kweli walikuja tu kwa jioni hata hawakulala..hata hivyo tulifurahi sana na lizombe juu...Ni kweli walisema ilikuwa baridi mno ..chakula tulikula pilau. Kweli ujio wao ulitufanya wote tuonekana kama tupo nyumbani kabisa na sio "ugenini"...pole na mafuriko..

Anonymous said...

Ni furaha sana kuwa na ugeni wa nyumbani. Muendelee na moyo huo mzuri wa kukaribisha wageni na Mungu atazidi kuwabariki. Nimeitamani sana pilau na mie siku moja ntakuwa mgeni wako da Yasinta.

Anonymous said...

Ni furaha sana kuwa na ugeni wa nyumbani. Muendelee na moyo huo mzuri wa kukaribisha wageni na Mungu atazidi kuwabariki. Nimeitamani sana pilau na mie siku moja ntakuwa mgeni wako da Yasinta.

Anonymous said...

Thanks in support of sharing such a fastidious opinion, piece of writing is nice, thats why i have
read it entirely
Feel free to surf my blog post ; panic attack treatment

ray njau said...

Daima undugu ni kufaana na siyo kufanana.

luddo17 said...

Ilikuwa ni raha na furaha ya pekee kuwa pamoja nanyi na kula chakula cha jioni pamoja. Tulijihisi tuko nyumbani Tanzania, kwani licha ya kuongea lugha yetu adhimu ya Kiswahili, pia tulikula msosi wa Kitanzania. Mmbarikiwe sana

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina wa 5.36 na 5:37 hamna taabu unakaribishwa sana tu.
Anony..9:46 thank you

Ray! ni kweli kabisa ulichosema.

Shem Luddo..yaani ile siku ilikuwa ya furaha mno twasikitika ilikuwa ni masaa machache ila tulifurahi sana kwa kweli...nanyi mbarikiwe sana