PAMOJA DAIMA!
Showing posts with label wanawake. Show all posts
Showing posts with label wanawake. Show all posts
Tuesday, April 7, 2020
Wednesday, March 21, 2018
MAONI YALIYOTOLEWA NA KAKA RAY NJAU KUHUSU TAULO ZA KIKE!
HAPA NI KAKA RAY NJAU
Kukabiliana na Matatizo ya Kukoma kwa Hedhi
“Ghafula nilihisi nimelemewa na huzuni bila kujua sababu. Nililia na kuanza kujiuliza ikiwa ninarukwa na akili.”—Rondro, * mwenye umri wa miaka 50.
“Unaamka asubuhi na kupata nyumba yako ikiwa shaghalabaghala. Huwezi kupata kitu chochote unachotafuta. Mambo ambayo ulikuwa ukifanya kwa urahisi, sasa yanaonekana kuwa magumu sana, na hujui ni kwa nini hali iko hivyo.”—Hanta, mwenye umri wa miaka 55.
WANAWAKE hao si wagonjwa. Wanapitia tu kipindi cha kukoma kwa hedhi, ambacho ni badiliko la kiasili katika maisha ya mwanamke anapoacha kuwa na uwezo wa kupata watoto. Ikiwa wewe ni mwanamke, je, unakaribia kipindi hicho? Au je, unapitia kipindi hicho sasa hivi? Vyovyote vile, kadiri ambavyo wewe na wapendwa wako mnajifunza kuhusu kipindi hiki cha mabadiliko, ndivyo mtakavyoweza kukabiliana kwa njia inayofaa na matatizo yanayohusiana nacho.
Kipindi cha Kukoma Hedhi
Wanawake wengi huanza kipindi hicho wakiwa na umri wa miaka 40 na kitu, lakini wengine huanza wakiwa wamechelewa wakiwa na miaka 60 na kitu. * Kwa wanawake wengi, hedhi hukoma hatua kwa hatua. Kwa sababu ya kubadilika-badilika kwa kiwango cha homoni kinachotokezwa, huenda mwanamke akakosa kupata hedhi pindi kwa pindi, akapata hedhi wakati ambao hakutarajia, au akavuja damu nyingi isivyo kawaida wakati wa hedhi. Wanawake wachache hukoma kupata hedhi ghafula, yaani, wanakosa hedhi mwezi mmoja na huo unakuwa mwisho wa kuipata.
Kitabu kuhusu kukoma kwa hedhi (Menopause Guidebook) kinasema: “Kipindi hicho huwa tofauti kwa kila mwanamke.” Kitabu hicho kinaendelea kusema hivi: “Matatizo ya kawaida yanayohusiana na kipindi hicho ni kupata joto la ghafula mwilini,” ambalo huenda likafuatwa na kuhisi baridi. Dalili hizo zinaweza kumfanya mtu akose usingizi na kuishiwa na nguvu. Matatizo hayo huendelea kwa muda gani? Kulingana na kitabu hicho, “wanawake fulani hupatwa na joto la ghafula mwilini kwa mwaka mmoja au miwili wakati wa kipindi hicho cha kukoma kwa hedhi. Wengine hupatwa na hali hiyo kwa miaka mingi, na wachache sana husema kwamba wao hupatwa na joto la ghafula mara kwa mara maisha yao yote.” *
Kwa sababu ya kubadilika-badilika kwa kiwango cha homoni, huenda mwanamke akashuka moyo, hisia zake zikabadilika-badilika na hilo linaweza kumfanya alielie bila sababu, na pia asiwe makini sana na asahau mambo. Licha ya hayo, kitabu The Menopause Book kinasema kwamba “kuna uwezekano mkubwa kwamba mwanamke hatapatwa na mambo hayo yote.” Kwa kweli, wanawake fulani hupata matatizo machache sana na wengine hawapati matatizo yoyote wakati wa kipindi hicho.
Jinsi ya Kukabiliana na Kipindi Hicho
Kubadili mtindo wa maisha kunaweza kupunguza baadhi ya matatizo hayo. Kwa mfano, wanawake wanaovuta sigara wanaweza kupunguza mara ambazo wanapatwa na joto la ghafula kwa kuacha kuvuta sigara. Wanawake wengi hunufaika kwa kubadili mazoea yao ya kula kama vile kupunguza au hata kuacha kunywa kileo, vinywaji vyenye kafeini, na vyakula vyenye sukari au vikolezo ambavyo vinaweza kusababisha joto la ghafula mwilini. Bila shaka, ni muhimu kula vyakula mbalimbali na vyenye lishe.
Kufanya mazoezi husaidia sana kupunguza matatizo yanayohusianishwa na kukoma kwa hedhi. Kwa mfano, mazoezi yanaweza kupunguza kukosa usingizi na kusaidia kuboresha hali ya kihisia na pia kuimarisha mifupa na afya ya mtu kwa ujumla. *
Eleza Mambo Waziwazi
Rondro aliyenukuliwa mwanzoni mwa makala hii anasema hivi: “Usiteseke kimyakimya. Ukiwaeleza wapendwa wako mambo waziwazi, hawatakuwa na wasiwasi kuhusu hali yako.” Jambo hilo linaweza kuwafanya hata wakuonyeshe subira na huruma zaidi. “Upendo ni wenye ustahimilivu na wenye fadhili,” linasema andiko la 1 Wakorintho 13:4.
chanzo:www.jw.org/sw
Maoni yanatoka katika mada hii TAULO ZA KIKE! kila la kheri kwa wote na ahsante sana kaka RAY.
Monday, November 20, 2017
NI WIKI NYINGINE NA JUMATATU NYINGINE...TUANZE WIKI NA PICHA HII YA KITAMADUNI KABISA
Wanawake wakitwanga nimekumbuka mbali sana nilikuwa nikipata shida sana kutwanga watatu au wanne....:-)
Thursday, April 16, 2015
MWANAMKE KANGA....NIMEPENDA MTINDO HUU WA KUFUNGA KANGA!!
Kanga zina matumizi mengi sana. Ni utamaduni mzuri sana ..ila naona kama unaanza kupotea. Nikisema hivi nina maana wanawake wengi wameanza kuacha kutumia kanga na kuiga mavazi mengine kabisa inasikitisha kwa kweli maana kiazazi kijacho hakitajua utamaduni huu. Tafadhali wanawake wenzangu tudumishe utamaduni huu. Kapulya.
Wednesday, July 30, 2014
WANAWAKE 280 PERAMIHO/LUNDUSI WAJITOKEZA KUPIMA KWA HIARI!!!
Baada ya kusoma habari hii sikuweza kuacha kuisambaza LUNDUSI ni nyumbani mnajua. Mtu kwao ni furaha kuona wanawake wanajitokeza kwa hiari kwa zoezi hili. Habari yenyewe ndiyo hii hapa chini, karibuni
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------
WANAWAKE 280 katika kijiji cha Lundusi kata ya Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma wanahitaji huduma ya kupimwa kwa hiari virusi vya ukimwi ili kutambua afya zao.
Wanawake hao wametoa ombi la kutaka kupimwa virusi vya UKIMWI kwa hiari baada ya kupata elimu ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yaliyoendeshwa na shirika la maendeleo ya wanawake Ruvuma RUWODA.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki moja katika vitongoji vya Ringa,Lundusi,Dodoma na Kiburungi vilivyopo katika kijiji cha Lundusi chenye wakazi zaidi ya 2500 ambapo wananchi hao wameweza kujifunza mada mbalimbali zilizotolewa na Radbord Ngonyani ambaye ni mratibu wa shirika la RUWODA.
Kulingana na mratibu huyo wa RUWODA, mada ambazo zimefundishwa katika mafunzo hayo ambayo yalishirikisha jumla ya watu 350 ni pamoja kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto(PMTCI),ongezeko la vituo vya huduma na wajibu wa jamii katika kuzuia maambukizi.
Mada nyingine ni lishe kwa mtoto aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI toka kwa mama kwenda mtoto,,uwezekano wa mama mjamzito wa kumwambukiza mtoto,namna ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na uwezo wa mama mjamzito kuzuia maambukizi kwenda kwa mtoto.
Ngonyani amezitaja mada nyingine ambazo zimefundishwa kuwa ni athari za kuishi na virusi vya UKIMWI,mahitaji ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI,wajibu wa jamii katika kuzuia virusi vya UKIMWI na UKIMWI,uaminifu katika mahusiano ya mapenzi na mkakati wa kuhamasisha umuhimu elimu na faida ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Mratibu huyo wa RUWODA amefurahishwa na wanawake wa kijiji cha Lundusi kuamua kwa hiari kutaka kupimwa virusi vya UKIMWI ambapo ameahidi kuwasiliana na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea ili kutoa wataalamu wa upimaji waweze kwenda katika kijiji hicho kuwapima wanawake wanaotaka kupima kwa hiari.
“Wananchi waliojitokeza kutaka kupimwa kwa hiari watasaidia serikali kupata takwimu sahihi za maambukizi ya virusi vya UKIMWI na namna ya kuwasaidia watakaobainika kuathirika,tatizo la ,maambukizi ya virusi vya UKIMWI bado kubwa katika wilaya ya Songea’’,alisema.
Sera ya afya Tanzania ya mwaka 2007 inatamka wazi Serikali inafanya juhudi kubwa kukabiliana na janga la UKIMWI. Hata hivyo, kutokuwepo mwitikio sahihi wa kukabiliana na janga la UKIMWI miongoni mwa wananchi, kunaendelea kuathiri juhudi za kukabiliana na janga hili.
Kulingana na sera hiyo, hali hiyo, inaendelea kuathiri nguvu kazi, kuongeza vifo, yatima, umaskini na gharama za matibabu pamoja na kuathiri ustawi, uchumi na usalama wa taifa.
Kudhibiti maambukizi na ya Virusi vya UKIMWI nchini na kutoa matunzo na tiba ya kupunguza makali ya UKIMWI.Serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika kukabiliana na janga la UKIMWI katika nyanja zote zikiwemo, kinga, huduma za tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya na majumbani, ili kupunguza athari zinazosababishwa na VVU/UKIMWI.
Kulingana na takwimu za UKIMWI kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Mkoa wa Njombe, Mbeya Iringa na Ruvuma ni vinara wanaoongoza kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini.
Njombe inaongoza kwa asilimia 14.8 ikifuatiwa na Iringa kwa asilimia 9.1 na Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya tatu kwa asilimia 9.
Mikoa mingine na asilimia za maambukizi katika mabano ni Ruvuma (7.2), Shinyanga (7.4), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7).
Kwa mujibu wa takwimu hizo mkoa wa Mara (4.5), Mwanza (4.2), Mtwara (4.1), Kilimanjaro (3.8), Kigoma (3.4), Simiyu (3.6), Morogoro (3.8), Singida (3.3), Dodoma (2.9), Manyara (1.5), Lindi (2.9), Tanga (2.4), Unguja (1.9) na Pemba (0.3).
Takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanyika mwaka juzi hadi mwaka jana. Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti ya Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzani maambukizi ya Ukimwi yanapungua kwa kasi ndogo.
Hata hivyo shirika la Afya Ulimwenguni WHO limetoa takwimu zinazoonyesha kuwa maambukizi mapya yamepungua kwa asilimia 50 katika nchi 13 za kusini mwa jangwa la sahara ikiwemo Tanzania.
Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 1999 inakadiriwa kuwa watu wazima na watoto milioni 33.6 walikuwa wanaishi na virusi vya UKIMWI na watu milioni 16.3 walikuwa tayari wamefariki dunia katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara.
Pamoja na takwimu za shirika la afya duniani kutoa matumaini makubwa kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara bado nchi za Afrika mashariki zinawajibika kuongeza jitihada za kukabiliana na maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI hasa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto pamoja kutoa huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.
Wednesday, April 2, 2014
MAMA MJASIRIAMALI..ANAPIKA POMBE
Mama huyo hayupo nyumba katika kutaka kuitunza familia hapa anapika pombe. Kupika pombe ni kazi kubwa kwa kweli kwanza maandalizi yake ni makubwa halafu kuungua moto. Pia kupata kipato inategemea hiyo pombe "inoge" iwe nzuri. Nimewahi kutazamia jinsi inavyopikwa hii pombe wakati mama akipika hasa ile ya mihogo MYAKAYA si mnajua kila pombe huwa na jina lake baadhi ni kama vile kindi /komoni pombe ya mahindi Mbege pombe ya ndizi. Na pia pombe si ni kinywaji tu cha kujifurahisha au kupata uchumi, kwa kifupi hasa sisi WANGONI kwa asili hupenda sana kunywa maji wakati akila chakula ila baada ya chakula hupenda kupata pombe/ugimbi kidogo kushushia ugali/chakula. Pia pombe huweza kuwashirikisha watu kwa kufanya kazi pamoja, kama vile kulima/kuvuna, kwenda kilabuni, pombe ya harusi, na pombe ya sadaka. Na kwa kawaida huwa mtu/watu maalumu ambao huja mapema alfajiri kuonja kama pombe ipo safi "imenoga" kabla haijachunjwa na kwenda kilabuni au kunywewa.
Hapa naona ni ile POMBE ya kilabuni. Huyu baba kaona anachelewa kaamua kuchukua ndoa nzima ameona "dumla" au kisonjo wangoni wanaita KIJOMELA. Nitawaonyesha siku yake. Kwa leo tuishia hapa. ANGALIZO:- TUSISAHAU SASA NI KWARESMA TUSINYWE KUPITA KIASI POMBE SI MAJI. Kapulya.

Friday, February 7, 2014
UJUMBE WA IJUMAA YA LEO KUTOKA KWA KIBARAZA CHA MAISHA NA MAFANIKIO NI KAMA UFUATAVYO!!!!
Bila ubishi wala maswali mengi katika maisha ya Taifa letu tunategemea sana uwepo wa wanawake.
NAWATAKIENI WOTE MWANZA MWEMA WA JUMA HILI MAANA LEO NI IJUMAA WENGI WANAANZA MAPUMZIKO BAADA YA KAZI YA JUMA NZIMA.
NAWATAKIENI WOTE MWANZA MWEMA WA JUMA HILI MAANA LEO NI IJUMAA WENGI WANAANZA MAPUMZIKO BAADA YA KAZI YA JUMA NZIMA.
Tuesday, May 14, 2013
WANANDOA NA KAULI HIZI: HATA VIKOMBE KABATINI HUGONGANA, ITAKUWA SIE?
Je unadhani au kuamini kwamba kuna ndoa
ambazo wanandoa wake hawagombani kabisa? Kama unaamini hivyo, basi unajidanganya
na labda unaishi katika dunia ya peke yako.
Ni jambo lenye ukweli wa
kutosha kabisa kwamba wanandoa wote duniani hutokea kugombana, lakini kugombana
huko hutokana na migongano au mizozo ya muda tu ambayo huweza kutatuliwa na
pande mbili kama wakiamua kufanya hivyo.
Wewe unayesoma hapa, napenda
kukuambia ukweli kwamba usiogope migogoro ya ndoa, kwani hicho ni kitu ambacho
kamwe huwezi kukiepuka. Kuna msemo mmoja unatumika sana huko nyumbani usemao, "
hata vikombe kabatini hugongana itakuwa wana ndoa?" Hii ina maana gani, ina
maana kwamba haiwezekani watu kuishi pamoja halafu msiwe mnatofautiana, na kama
ukiona hivyo, jua kwamba hiyo ndoa si salama kwani siku yoyote bomu litapasuka
na madhara yake yatakuwa ni makubwa kuliko kawaida.
Kuna watu ambao hata
kama wamekosewa na wenzi wao hunyamaza kimya na kumeza hasira zao, wengine
huogopa kuwakabili wenzi wao na kuzungumzia jambo linalowakera kwa kuhofia
kuonekana kama wana kasoro au ghubu. Jambo hili ni hatari sana.
Kumkabili
mwenzi wako na kumwambia hisia zako kama amekukosea au amekwenda kinyume na
matarajio yako ni jambao la maana sana katika kudumisha uhusiano. Lakini naomba
nitahadharishe kwamba, ni vyema kufanya hivyo bila kumshusha, kubeza au
kusimanga kwani hiyo sio dalili nzuri ya upendo.
Inashauriwa kwamba
wanandoa au wapenzi wanapokwaruzana inabidi wajadili tofauti zao bila
kusigishana, kila mmoja akitaka kuwa mshindi, hiyo haitasaidia kuimarisha ndoa
bali itaongeza tatizo. Ni vyema upande unaohusika na tatizo, uwajibike na kuomba
radhi kwa ustawi wa ndoa, huo ndio ukomavu.
Kutojadili mgogoro kwa
wanandoa na kuupatia ufumbuzi wa tatizo huwafanya wandoa kuwa mbali kihisia, na
athari zake ni kuwakuta wanandoa wakiwa wageni wa kila mmoja kwa mwenzake, yaani
hakuna mawasiliano, kila mtu na lwake.
Jambo la msingi kwa wanandoa ni
kujadili tofauti zao pindi linapojitokeza jambo linalomkera mmoja wa wanandoa,
kwani hakuna jambo linaloweza kujitatua lenyewe bila kutatuliwa na wandoa
husika. Kuacha jambo lolote bila kulitafutia suluhu ni sawa na kutega bomu,
ambapo siku likilipuka madhara yake ni makubwa sana.
Unaweza kukuta
mwanandoa anakereka na mambo madogo madogo ya mwenzi wake lakini hasemi, ingawa
yanamkera kupita kiasi akitegemea huyo mwenzi wake atajua na kuacha,
thubutu…..inapotokea siku yeye amekosa jambo dogo tu na huyo mwenzi wake
akamsema, basi atatumia fursa hiyo kuanza kujibu mapigo kwa kueleza yale
yanayomkera kutoka kwa mwenzi wake, na hapo itakuwa kila mtu anavutia kwake kama
mwamba ngoma………na aamini nawaambia kuwa kamwe hawezi kupatikana mshindi katika
jambo hilo, kwani mjadala huo unaweza kutoka nje ya mada kila mmoja akijitahidi
kutafuta makosa ya mwenzi wake hata yale yaliyotokea wakati wa uchumba wenu ili
mradi vurugu tupu.
Inatakiwa wanandoa wajadili kila jambo linalojitokeza
hadi kulipatia suluhu, vinginevyo ni kuichimbia ndoa yenu kaburi la mapema.
Wakati mwingine unaweza kukuta mwanamke analalamika juu ya kutoridhishwa kwake
na matumizi ya mumewe, na hapo mume naye ataanza kukumbusha juu ya matumizi
yasiyo ya lazima yaliyofanywa na mke huko nyuma. Mke naye hataridhika
atakumbushia jambo lingine na lingine hadi hata mada iliyokuwa ikijadiliwa
inasahaulika.
Jambo lingine ni kujumuisha mambo, matumizi ya maneno kama,
mara nyingi, kila wakati au mara kwa mara si mazuri sana. Unaweza kukuta mtu
mwenzi wake amekosea jambo halafu mwenzie anamwambia “Kila mara huwa unafanya
hivi” au mara nyingi huwa unafanya hivyo…..Hii ni hatari kwa ustawi wa wanandoa,
kwani kwa kujumuisha ni sawa na kumwambia mwenzi wako kuwa kila mara yeye ndiye
mkosaji.
Kwa haya niliyoyaeleza hapa sina maana kwamba huu ndio
muarobaini pekee wa kuimarisha mahusiano kwa wanandoa, bali ni moja ya mambo
muhimu kati ya mengi ambayo yakizingatiwa na wanandoa wote basi ndoa yao itakuwa
imara Tujadili pamoja………..
Thursday, May 2, 2013
WANAWAKE NA MIGOROLI ..HAWA NI WAMTINDO/WAREMBO WA WIKI HII...JE UNAWAFAHAMU?
Wanawake/wadada hawa wanaonekana kupenda sana kuvaa mgoroli ..umegundua kitu hapa ni kwamba wote wameachia mkono wa upande mmoja..:-)
Halafu unajua kitu kingine huyo wa juu katabasamu lakini huyu wa chini au mwenye kijani anaonekana yupo mbali kweli kifkra...Unajua ni kitu gani kingine wadada/wanawake hawa wanapenda kufanya?...Karibuni ....
Wednesday, April 10, 2013
PICHA YA WIKI:- WANAWAKE WANAWEZA HATA KABLA HAWAJAWEZESHWA.....
Hapa nimejiuliza mara kumi kumi hivi anawezaje huyu mama....maana kuendesha baiskeli unahitaji balansi na kuubeba huyo mzigo pia halafu mtoto mgongoni na mtoto nyuma ya baiskeli naye kabeba mtoto ...mmmmhhh hapa kazi kwelikweli....Lakini kweli hii ni haki kweli/Uungwana kweli??? KILA LA KHERI !!!
Tuesday, April 2, 2013
WANAMITINDO NA WAREMBO WA WIKI ..JE? UNAWAJUA HAWA WADADA??
Hawa ni kati warembo,wanamrindo waliokuweka katika COVENTRY WOMEN Kwa picha na mambo mengine zaidi bonyeza KACHIKI. Ahsanteni wote...
Tuesday, March 12, 2013
NAPENDA NGUO NDEFU MWENZENU..NA HII NI KAZI YA DADA SUBIRA WAHURE...
Hili gauni limenivutia mpaka basi ..yaani ningependa nilimiliki kabisaaaa..ebu angalia lipo rahisi rahisi kweli lakini ni bonge la kitu ...mavazi ya heshima hayaa ...
Na hapa hii sketi imenimaliza kabisa ndefu, pana, rangi zake zinavutia yaani kama nipenzavyo...Nakutakia kazi njema sana dada Subira ...kwa kuona kazi zake nyingine inga hapa. NAWATAKIENI JUMANNE NJEMA SANA WOTE.

Monday, October 8, 2012
HEBU FIKIRIA KIDOGO KUHUSU HILI!!!
Tafiti nyingi zinaonyesha kwamba, ndoa sita katika kila kumi huvunjwa na wanaume au wanawake kutoka nje. Lakini inaonekana pia kwamba, wale wanaotoka nje ya ndoa zao, wengi ndiyo ambao huacha au kuachwa. Ni karibu ndoa nane katika kila kumi, ambazo hufikia ukomo kutokana na kutoka nje.
Wanawake ambao wako chini ya umri wa miaka 30, hutoka nje kwa kiwango karibu sawa na wanaume. Umri huo ndiyo hatari sana kwa wanawake kutoka nje.
Inaonyesha kwamba, bado dini haiogopwi sana linapokuja suala la kutoka nje. Waumini na viongozi wengi wa dini mbalimbali wanadaiwa kutoka nje kwa kiwango kikubwa kuliko inavyodhaniwa.
Karibu wanawake wawili katika kumi na wanaume watatu katika kumi, huwa wametoka nje ya ndoa zao katika maisha yao hapa duniani.
Uhusiano mwingi wa kiuzinzi hudumu kwa miaka mitatu tu na wapenzi huachana au kuachanishwa kwa kufumaniwa. Lakini mwingine hudumu maisha, ingawa na madhara yake nayo hudumu maisha.
Ni mwanamume mmoja kati ya kila kumi, ambao huwaacha wake zao na kuoa nyumba ndogo. Wengi hubaki na wake zao huku wakiwa na nyumba ndogo, au kuwaacha wake zao, lakini hawaoi nyumba ndogo.
Hata hivyo, wanane kati ya kumi miongoni mwa wale wanaowaacha wake zao na kuoa"nyumba ndogo," nao huja kuachana na nyumba ndogo hizo. Kwa hiyo, ni wawili tu kati ya kumi ambao hudumu na "nyumba ndogo" walizozioa baada ya kuachana na wake zao kwa sababu ya "nyumba ndogo" hizo.
Halafu wanane kati ya kumi ya kila aliyevunja au kuvuruga uhusiano wake na mume au mke kwa sababu ya hawara, huja kujuta baadaye. Ni wawili tu kati ya kumi, ambao uvurugaji wa uhusiano wake kwa sababu ya hawara, hawaji kujuta. Hawa ni wale ambao ndoa zao zilikuwa tayari na mashaka makubwa.
Huchukua mwaka mmoja hadi mitatu kwa ndoa ambayo imeingiliwa na fumanizi, wanandoa kuanza kuelewana tena kama awali. Hapo uhusiano huwa imara kuliko awali, au huingia mashaka ya sirisiri.
Chanzo:- kitabu Mapenzi kuchipia na kunyauka na Munga Tahenan.

Wednesday, October 3, 2012
Mwanamke maarufu kuliko wote duniani....
Kila mtu akiulizwa ni mwanamke gani maarufu au aliye ngangari zaidi, kama anatafakari vizuri, atasema kuwa ni mama yake, hasa kama alimlea kwa uadilifu. Pengine mwingine atasema ni mkewe, kutegemea na namna wanavyoishi kwenye uhusiano wao wa kindoa.
Lakini, linapokuja suala la mwanamke ambaye hakuhusu, ambaye unaamini au kudhani kwamba, ndiye ngangari zaidi hapa duniani, hasa katika siasa na uchumi, inaweza kuwa mtihani mgumu kwako kutoa jibu sahihi.
Ni kweli, unaweza kutoa jibu, lakini siyo lazima jibu lako liwe sahihi.
Kama ni sahihi, itakuwa ni kwa sababu tu, unamjua huyo uliyemtaja, na wengine huwajui.
Hivi ndivyo ambavyo imetokea kwenye kura iliyofanyika ya kuwataja wanawake wanaodhaniwa kuwa maarufu hapa chini ya jua kwenye nyanja ya siasa na uchumi.
Karibu kila Mtanzania angetarajia kuwa wakitajwa wanawake 100 duninai ambao ni maarufu kwa sasa, huenda Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro angetajwa. Matarajio hayo yangetokana na sababu mbalimbali.
Kwanza, unaibu wa Katibu Mkuu wa UN, siyo nafasi ndogo hapa duniani. Pili, kwa mwanamke kutoka Afrika tena kwa nchi ambayo ni miongoni mwa zile maskini kabisa, kushika nafasi hiyo, ni jambo la kinasibu zaidi kwa mitazamo ya mgawanyo wa dunia. Tatu, ingetarajiwa naibu atoke angalau bara Amerika, kwani Katibu Mkuu anatoka Asia, bara maskini karibu sawa na Afrika kwa uwiano.
Kwa bahati mbaya, jarida maarufu duniani kwa kufanya tathmini za viwango mbalimbali kuanzia utajiri, uzuri na umaarufu wa binadamu, la Forbes linaonesha katika taarifa zake za wiki mbili zilizopita kwamba, Migiro hayumo kwenye orodha ya wanawake 100 maarufu duniani katika nyanja za uchumi na siasa.
Kutoka Afrika ni wanawake wawili tu walio kwenye orodha hiyo. Kwanza ni , Waziri Mkuu wa Msumbiji, ambaye anashikilia nafasi ya 89 diuniani kwa umaarufu. Halafu anafuatiwa na Rais wa Liberia, , ambaye anashikilia nafasi ya 100.
Hii ina maana kwamba, Waziri Mkuu wa Msumbiji ni maarufu zaidi duniani, ukilinganisha na Rais wa Liberia, , nchi iliyoweka historia duniani kwa vurugu kubwa za kisiasa, zilizopelekea marais wawili kuuawa kinyama na mmoja kupamba vyombo vha habari dunia kuhusiana na mashtaka ya mauaji ya kimbari.
Rais Ellen Johnson ndiye Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika, lakini anakuwa Rais baada ya uchaguizi huru na wa haki uliofuatia umwagikaji wa damu nyingi ya kutosha. Bado huyu anashikilia nafasi ya 100, wakati Waziri Mkuu wa Msumbiji anashikilia nafasi ya 89!
Hapa ndipo ambapo matokeo haya ya jarida la Fobes yanatia mashaka. Ni kweli kwamba, uchaguzi huo umefuatia kura kutoka kwa watu duniani kote.
Bahati mbaya ni kwamba, kura hizo kwa sehemu kubwa zimehusisha matumizi ya vyombo vya kisasa ambavyo havipo kwa wingi Afrika, hasa mtandano wa intaneti.
Katika orodha hiyo kuna majina ya wanawake ambayo huenda kwa umaarufu, akili ya kawaida inaweza kukuonesha kwamba, hawawezi kumzidi Asha Rose Migiro. Hebu kwa mfano, tuchukulie mwanamke kama , ambaye ni mtendaji kuuu wa Benki ya Leumi ya Israeli. Je, huyu mama uliwahi kumsikia au hata kumsoma kwenye chombo chochote cha nje? Huyu anashikilia nafasi ya 83 kwa umaarufu.
Huenda inabidi Afrika nayo sasa iwe na utaratibu wa kutafuta maoni ya dunia nzima ambapo waafrika nao watashiriki sawa kusema kuhusu nini wanaona, sawa na watu wengine duniani. Inaonekana wazi kwamba, hata viwango vya umaskini vinavyopangwa kutoka Ulaya na Marekani ni kwa vigezo ambavyo havifutu na kukidhi ukweli mkubwa zaidi unaowahusu Waafrika.
Kwenye orodha hiyo, inaonekana kuwa, Rais wa Ujerumani, , ndiye mwanamke maarufu zaidi duniani. Wu yi, ambaye ni makamu mwa Rais wa China anashikilia nafasi ya pili.
Nafasi ya tatu inashikiliwa na ambaye ni mtendaji mkuu wa kampuni ya Temasek Holdings, ya Singapore.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, anashikilia nafasi ya nne.
Wengine ni , mwenyekiti wa kampuni ya PepsiCo ya Marekani. Namba sita ni , Rais wa India. Namba saba imeenda kwa, mtendaji Mkuu wa kampuni ya Anglo American ya Uingereza.
Nafasi ya nane anaishikilia ambaye ni mwenyekiti, kampuni ya Archer Daniels Midland ya marekani.
Namba tisa ni , mwenyekiti kampuni ya Kraft Foods ya Marekani, na namba kumi ni , Mtendaji Mkuu wa Alcatel-Lucent ya Marekani.
anashikilia nafasi ya 21, wakati Malkia Elizabeth anashikilia nafasi ya 23.
Mke wa Rais wa zamani wa Marekani, , anashikilia nafasi ya 25.
Kama orodha hii ya Forbes inaonesha ukweli na uhalisia wa umaarufu unaotokana na michango ya wanawake katika jamii zao au jamii ya dunia, ina maana kwamba, kwa Afrika, wanawake hawajafanya lolote kwa jamii zao na jamii ya dunia.
Lakini, huo utakuwa pia ni uongo mkubwa, kwa sababu kuna idadi kubwa ya wanawke hapa Afrika ambao wamejitahidi kwa viwango vya kimataifa kubadili hali za watu wengine katika jamii.
Kama ni umaarufu kwa maana ya kujitangaza na kutangazwa sana na vyombo vya habari, ni wazi suala zima linakosa mantiki na linajaribu tu kuwavunja moyo wanawake wa Afrika. Orodha hiyo ni wanawake maarufu duniani katika nyanja za siasa na uchumi, ambapo ni uongo kudai kwamba, kati ya wanawake 100 duniani, Afrika inaambulia nafasi mbili, tena za mwisho.
Hii ina maana dunia inawatambua wanawake wawili tu Afrika katika nyanja hizo? Ndiyo maana naamini kwamba, Migiro angepaswa kuwemo kwenye orodha hiyo, kama kweli inakagua mambo kwa uhalali.
Lakini, mtu akikagua orodha hii tena na tena anaweza kupata picha kubwa zaidi na kuikubali, ingawa baadaye anaweza kuipinga. Ni matokeo ya kura yenye utata. Kwa mfano, Hilary Clinton anafahamika, kama ilivyo kwa Oprah Winfrey, lakini nao wametupwa hadi nafasi za 20, kama ilivyo kwa Malkia Elizabeth.
Lakini, hapohapo kuna majina kati ya namba 11 hadi 20, ambayo ni ya wanawake ambao hata watazamaji, wasomaji na wasikilizaji wazuri wa vyombo vya habari vya nje hawajawahi kuwasikia.
Kama ilivyo kwenye nyanja nyingine, hasa uchumi, vyombo vya habari vya Magharibi, bado vinaitendea Afrika kama vile ni bara wanamoishi wanyama, badala ya binadamu.
Vyombo vyetu vya habari, kwa bahati mbaya, navyo ni kama sauti za vyombo vya habari vya Magharibi.
Vikifanya tafiti zao, vinafanya kwa njia finyu na iliyofubaa, isiyoweza kuwahamasisha Waafrika.
Hii iliandikwa kwenye gazeti la jitambue iliandikwa na Hayati Munga Tehenan.

Tuesday, September 18, 2012
UJUMBE WANGU WA LEO:- WASICHANA NA WANAWAKE WANA HAKI!!
Watu wote ni sawa, watu wote wana thamani sawa. Hii ina maana kuwa wanawake na wanaume, wasichana na wavulana, wana haki sawa. Lakini katika jamii zetu wanawake na wasichana wananyimwa haki zao.
Hatua ya kwanza kuleta usawa ni kuielewa na kutokuukubali unyanyasaji wa wanawake na wasichana
JUMANNE NJEMA NDUGU ZANGUNI!!!
Hatua ya kwanza kuleta usawa ni kuielewa na kutokuukubali unyanyasaji wa wanawake na wasichana
JUMANNE NJEMA NDUGU ZANGUNI!!!
Wednesday, September 5, 2012
VAZI HILI LA KITENGE NIMELIPENDA SANA..MAMA SALMA KIKWETE NA DKT ASHA-ROSE MAIGIRO
Ndugu zangu waTanzania hasa akina dada/akina mama hebu angalieni vazi/mavazi haya. Kwanza ni la heshima, pili wanapendeza yaani hata kuangalia tu kwa macho. Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza kwa nini kupoteza pesa nyingi kununu nguo kama mitumba nk. Wakati kuna vitenge vizuri ajabu ambavyo twaweza kushona na kupendaza kama akima mama hao hapo juu. Angalia mishono yao ni rahisi rahisi tu si ya ajabu. Hakika mwenzenu niMEPENDA SANA HII.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------
Hapa ni wote mnawafahamu hawa akina mama ila nitasema tena ni:- Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akiwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt Asha-Rose Migiro baada ya Mama Kikwete kuzindua Mpango wa Kasi ya Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana Agosti 24, 2012 katika ukumbi wa Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam.
JUMATANO NJEMA KWA WOTE!!!!
Tuesday, September 4, 2012
ELIMU :- KISOMO CHA WATU WAZIMA!!!
Elimu haina mwisho hapa akina mama wapo darasani kwa ajili ya kupata ELIMU..angalao kuweza kuandika tu..Inafurahisha kuona walezi wetu wana moyo wa kutaka kupata elimu. Ila nimejiuliza hivi hili darasa ni kwa ajili ya akina mama tu? Maana sioni akina baba hapa.
Monday, August 13, 2012
TUANZE JUMATATU HII NA PICHA HII YA WAREMBO WA KINGONI!!!
Picha:- Ni ya wanawake wa KINGONI (mzimba) hapa ni mapema miaka ya 1900.... Nimeipenda picha hii maana inaonyesha jinsi wanawake hawa wanavyojali urembo wa asili ebu watazame...inavutia kwa kweli. JUMATATU NJEMA...
Monday, July 30, 2012
WANAUME NA KUFUNDISHWA!!!!
Mwanamke anaweza kufikiri ataimarisha upendo kwa kumwambia mwanaume, "fedha unazopata, tungetumia sehemu na sehemu tukaweka akiba,, tukatafuta kiwanja. halafu tukatafuta sehemu kama shamba, halafu..." Anaweza kushangaa sana akiona mwanamume badala ya kushukuru kwa ushauri huo, akimwambia, "unadhani ni rahisi kiasi hicho, ingekuwa ni wewe unayetafuta fedha hizo wala usingesema hivyo. Nyie wanawake ndiyo matatizo..."
Halafu yanaweza kufuata maneno mengine ya "ajabuajabu" kutoka kwa mawamume hadi mwanamke akanywea. Mwanamke ataanza kujiuliza kosa lake kwa ushauri wake huo uliouona ni wa upendo. Ni wazi hataliona kosa lake, hivyo atajua kwamba, mumewe hampendi tena, atajua kwamba upendo umekwisha. kama si kujua kwamba upendo umekwisha, atajua kwamba mumewe hamsikilizi wala kumjali, ni dikteta na asiyeambilika.
Ni kwa sababu tu ya kutokujua hata hivyo. Kosa la mke huyu ni kushindwa kwake kujua kwamba, yeye na mwanamume wanatofautiana. Mwanamume hataki kabisa kufundishwa, hataki kabisa kuelekezwa au kushauriwa kabla hajaomba mambo hayo kutoka kwa mkewe. Kwa asili manamume ni mbabe na angependa kuona kwamba mwanamke anamtazama kwa jicho la kuwa yeye ni shujua na anayejua kila kitu. Anaposhauriwa bila kuomba, masikioni mwake husikia kama vile anaambiwa kuwa hayuko kamili na hajimudu na hivyo analaumiwa. Katika hali hiyo hujikuta akijitetea, ambapo matokeo yake ni hayo ya kumuuliza mke kama anadhani jambo hilo ni rahisi kama anavyoliongelea. Kuuliza huku kuna maana ya kumpa taarifa mkewe kwamba siyo kuwa ameshindwa ni ka sababu jambo hilo ni gumu. Anataka kumpa taarifa kwamba, huko "kumlaumu" kwake hakuna maana yoyote. Lakini kwa upande wa mke majibu hayo hayatoi maana hiyo, hutoa maana kwamba, mume hampendi tena na hajali ushauri wake.
Wanaume siku zote wanataka kuachwa watafute suluhu wenyewe, wanataka kuona wanahangaika na kupata wenyewe ufumbuzi wa tatizo au matatizo yanayowakabili. Wakipata wenyewe ufumbuzi bila msaada wa wake zao, huhisi kuwa uanaume wao umekamilika. Wake zao wanapojipeleka kimbelembele kutaka kuwapa ushauri kabla hawajaombwa wanatafuta kukorofishana kusiko kwa lazima. Hii ina maana kwamba, wanawake wasiwape ushauri waume zao? Hapana, haina maana hiyo.
Kwa kuwa mwanamume hataki kufundishwa au kuelekezwa na mwanamke, anachotakiwa mwanamke kufanya ni kumpa mwanamume "chakula" chake, ambacho ni sifa. Aanatakiwa kuanza kwa kuonyesha kwamba mumewe amemudu au amefanikiwa katika mambo fulani kabla hajaingiza ushauri wake. Kwa mfano, Mariam anataka kumfahamisha mumewe kwamba amejisahau kuhusu maisha yao ya baadaye kwa sababu ya matumizi mabaya ya fedha. Anachotakiwa kufanya ni kutafuta yale mazuri ambayo mumewe ameyafanya au anayafanya. Inaweza ikawa kujali familia au ndugu wa mke ama kingine chochote.
Baada ya hapo ndipo anapoweza kuanza kuzungumzia kuhusu haja ya kufukiria kuhusu maisha yao ya baadaye. "Uzuri wako mume wangu ni kwamba unapenda kusikiliza na kizingatia ninachosema, wanaume wengine siyo rahisi, tunaona wanavyowadharau wake zao..., Mwanamke anaweza kuanza maelezo yako hivyo. Halafu akaendelea, "Ehe, sasa vipi kuhusu kutafuta kiwanja cha bei rahisi kwa ajili ya kuja kujenga tukiwa na uwezo baadaye. Najua sasa hivi una majukumu memngi, lakini bila shaka siyo vibaya kufukiria kuhusu jambo hilo. " Ni wanaume wachache ambao baada ya sifa kama hizo watacharuka wakielezwa kuhusu kufikiria kuhusu mustakabali wa maisha ya baadaye. Ni vizuri kwako mawamke kujaribu kufanya hivyo, ili uthibitishe kuhusu ukweli wa maelezo haya.
Chanzo:- kitabu cha Maisha na Mafanikio na Munga Tehenan.

Friday, June 29, 2012
MAISHA:- NIMEGUSWA SANA NA HABARI HII NA NIMEKUMBUKA MENGI, AMA KWELI MAISHA NI CHANGAMOTO KUBWA YA MAISHA!!!
MAMA MJAMZITO AKIPELEKWA HOSPITALI
Ni juzi tu nilikuwa nasikiliza/angalia habari. Mama mmoja mjamzito alipatwa ghafla na maumivu ya tumbo. Na alipotoa taarifa kwa gari la kubeba/kuchukua wagonjwa lilichelewa kuja . Lilikuja baada ya kama nusu saa. mama mjamzito huyo maumivu ya tumbo yakazidi na akawa anatoka damu. Alikuwa na ujauzito wa miezi saba. Kiumbe kilizaliwa kimekufa.....Na ndiyo nimekuja kukumbuka jinsi wanawake wengi wanavyo poteza maisha kutokana na umbali wa hospitali na usafiri. Nakumbuka wakati tunaishi kijiji cha Kingoli kulikuwa na gari moja la kijiji, duka moja kanisa moja, shule moja. Sasa hapo mtu uwe mjamzito hakuna nafasi ya kupona kama kunakuwa na shida kama ya huyu mama. Maana kutoka hapo kijijini hospitali ni Peramiho na kufika huko ni siku mbili kweli kuna kupona hapa? Ndo nikawa najiuliza sasa kama unapiga simu na watu wanachelewa kuna kuna maana gani sasa si sawa na kule kwetu Kingoli tu baiskeli au machela.... Ebu tumalizie kijana Side boy na wimbo huu JIFUNGUE SALAMA...
IJUMAA NJEMA KWA WOTE NA MWISHO WA JUMA UWE MWEMA.!!!
Subscribe to:
Posts (Atom)