Monday, July 30, 2012

WANAUME NA KUFUNDISHWA!!!!

Mwanamke anaweza kufikiri ataimarisha upendo kwa kumwambia mwanaume, "fedha unazopata, tungetumia sehemu na sehemu tukaweka akiba,, tukatafuta kiwanja. halafu tukatafuta sehemu kama shamba, halafu..." Anaweza kushangaa sana akiona mwanamume badala ya kushukuru kwa ushauri huo, akimwambia, "unadhani ni rahisi kiasi hicho, ingekuwa ni wewe unayetafuta fedha hizo wala usingesema hivyo. Nyie wanawake ndiyo matatizo..."
Halafu yanaweza kufuata maneno mengine ya "ajabuajabu" kutoka kwa mawamume hadi mwanamke akanywea. Mwanamke ataanza kujiuliza kosa lake kwa ushauri wake huo uliouona ni wa upendo. Ni wazi hataliona kosa lake, hivyo atajua kwamba, mumewe hampendi tena,  atajua kwamba upendo umekwisha. kama si kujua kwamba upendo umekwisha, atajua kwamba mumewe hamsikilizi wala kumjali, ni dikteta na asiyeambilika.
Ni kwa sababu tu ya kutokujua hata hivyo. Kosa la mke huyu ni kushindwa kwake kujua kwamba, yeye na mwanamume wanatofautiana. Mwanamume hataki kabisa kufundishwa, hataki kabisa kuelekezwa au kushauriwa kabla hajaomba mambo hayo kutoka kwa mkewe. Kwa asili manamume ni mbabe na angependa kuona kwamba mwanamke anamtazama kwa jicho la kuwa yeye ni shujua na anayejua kila kitu. Anaposhauriwa bila kuomba, masikioni mwake husikia kama vile anaambiwa kuwa hayuko kamili na hajimudu na hivyo analaumiwa. Katika hali hiyo hujikuta akijitetea, ambapo matokeo yake ni hayo ya kumuuliza mke kama anadhani jambo hilo ni rahisi kama anavyoliongelea. Kuuliza huku kuna maana ya kumpa taarifa mkewe kwamba siyo kuwa ameshindwa ni ka sababu jambo hilo ni gumu. Anataka kumpa taarifa kwamba, huko "kumlaumu" kwake hakuna maana yoyote. Lakini kwa upande wa mke majibu hayo hayatoi maana hiyo, hutoa maana kwamba, mume hampendi tena na hajali ushauri wake.
Wanaume siku zote wanataka kuachwa watafute suluhu wenyewe, wanataka kuona wanahangaika na kupata wenyewe ufumbuzi wa tatizo au matatizo yanayowakabili. Wakipata wenyewe ufumbuzi bila msaada wa wake zao, huhisi kuwa uanaume wao umekamilika. Wake zao wanapojipeleka kimbelembele kutaka kuwapa ushauri kabla hawajaombwa wanatafuta kukorofishana kusiko kwa lazima. Hii ina maana kwamba, wanawake wasiwape ushauri waume zao? Hapana, haina maana hiyo.
Kwa kuwa mwanamume hataki kufundishwa au kuelekezwa na mwanamke, anachotakiwa mwanamke kufanya ni kumpa mwanamume "chakula" chake, ambacho ni sifa. Aanatakiwa kuanza kwa kuonyesha kwamba mumewe amemudu au amefanikiwa katika mambo fulani kabla hajaingiza ushauri wake. Kwa mfano, Mariam anataka kumfahamisha mumewe kwamba amejisahau kuhusu maisha yao ya baadaye kwa sababu ya matumizi mabaya ya fedha. Anachotakiwa kufanya ni kutafuta yale mazuri ambayo mumewe ameyafanya au anayafanya. Inaweza ikawa kujali familia au ndugu wa mke ama kingine chochote.
Baada ya hapo ndipo anapoweza kuanza kuzungumzia kuhusu haja ya kufukiria kuhusu maisha yao ya baadaye. "Uzuri wako mume wangu ni kwamba unapenda kusikiliza na kizingatia ninachosema, wanaume wengine siyo rahisi, tunaona wanavyowadharau wake zao..., Mwanamke anaweza kuanza maelezo yako hivyo. Halafu akaendelea, "Ehe, sasa vipi kuhusu kutafuta kiwanja cha bei rahisi kwa ajili ya kuja kujenga tukiwa na uwezo baadaye. Najua sasa hivi una majukumu memngi, lakini bila shaka siyo vibaya kufukiria kuhusu jambo hilo. " Ni wanaume wachache ambao baada ya sifa kama hizo watacharuka wakielezwa kuhusu kufikiria kuhusu mustakabali wa maisha ya baadaye. Ni vizuri kwako mawamke kujaribu kufanya hivyo, ili uthibitishe kuhusu ukweli wa maelezo haya.
Chanzo:- kitabu cha Maisha na Mafanikio na Munga Tehenan.

1 comment:

ray njau said...

10 Mke mwenye uwezo, ni nani anayeweza kumpata? Thamani yake inapita sana ile ya marijani.

11 Moyo wa mume wake umemtegemea, wala hakuna faida inayokosekana.

12 Amemthawabisha mume wake kwa mema, wala si kwa mabaya, siku zote za maisha yake.

13 Ametafuta sufu na kitani, naye hufanya kazi yoyote inayopendeza mikono yake.

14 Amekuwa kama meli za mfanyabiashara. Huleta chakula chake kutoka mbali.

15 Tena huamka kabla usiku haujaisha, na kuwapa watu wa nyumbani mwake chakula na kuwapa vijana wake wa kike fungu lao lililoamriwa.

16 Amefikiria shamba, akalinunua; amepanda shamba la mizabibu kutokana na matunda ya mikono yake.

17 Amejifunga nguvu viunoni, naye ameitia nguvu mikono yake.

18 Ametambua kwamba biashara yake ni nzuri; taa yake haizimiki usiku.

19 Amenyoosha mikono yake kushika kijiti cha kusokotea uzi, nayo mikono yake mwenyewe imeshika gurudumu la kusokota nyuzi.

20 Amewanyooshea mkono wenye kuteseka, na mikono yake amemkunjulia maskini.

21 Hana wasiwasi juu ya watu wa nyumbani mwake kwa sababu ya theluji, kwa maana watu wote wa nyumbani mwake wamevaa mavazi mawili.

22 Amejitengenezea matandiko yenye mapambo. Mavazi yake ni ya kitani na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau.

23 Mume wake ni mtu anayejulikana malangoni, anapoketi pamoja na wanaume wazee wa nchi.

24 Hata ametengeneza mavazi ya ndani na kuyauza, nao wafanya-biashara amewapa mishipi.

25 Nguvu na fahari ndiyo mavazi yake, naye anaucheka wakati ujao.

26 Hufungua kinywa chake kwa hekima, na sheria ya fadhili zenye upendo ziko katika ulimi wake.

27 Anaangalia shughuli za nyumba yake, wala hali mkate wa uvivu.

28 Wanawe wamesimama na kumtangaza kuwa mwenye furaha, mume wake husimama, naye humsifu.

29 Kuna binti wengi ambao wameonyesha uwezo, lakini wewe—wewe umewapita hao wote.

30 Uvutio unaweza kudanganya, nayo sura yenye kupendeza inaweza kuwa ubatili; lakini mwanamke anayemwogopa Yehova ndiye anayejiletea sifa.

31 Mpeni baadhi ya matunda ya mikono yake, nazo kazi zake na zimsifu malangoni._Methali 31:10-31