Sunday, July 8, 2012

JUMAPILI YA LEO TUANGALIE:- HESHIMA YA MWANAMKE NA WITO WAKE!!!!




"Mwnamke kama Mama na mlezi wa kwanza wa mwanadamu ana haki ya pekee kabla ya mwanaume. Umama kwa upande wa utu na maadili unaonyesha uwezo wa mwanamke wa kuumba ulivyo muhimu sana ambao unadhihirisha wito wa pekee na ni changamoto ya pekee inayomchochea mwanmume na ubaba wake"
"Heshima ya mwanamke hutegemea utaratibu wa upendo, nao ni hasa utaratibu wa haki na wa kupendana.."
"Hongera kwa mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha!" Yesu akajibu, "Barabara; lakini heri yake zaidi yule anayelisikia neno la Mungu na kulishika" (Lk 11:27-28). 
NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA  WOTE MTAKAOPITA HAPA NA AMANI PIA UPENDO WA MUNGU UTAWALE NYUMBANI MWENU!!! 

8 comments:

Rachel Siwa said...

Ameen dada wa mimi, Mungu atubariki sote, Asante sana kwa NENO.

NENO LITASIMAMA MAMBO YOTE YATA PITA LAKINI NENO LITASIMAMA!!!!!!

Mwanasosholojia said...

Ahsante kwa neno lenye ujumbe lukuki Da'Yasinta, Amani na Furaha kwako!

Simon Kitururu said...

Mie nasimamia haki sawa kati ya Mwanamke na Mwanaume. Ya nani zaidi... mie huko simo!

Yasinta Ngonyani said...

Rachel, Kaka Mathew na Simon ahsanteni kwa kuwa pamoja nami jumapili hii.

sam mbogo said...

Katika uzoefu wangu hapa duniani,namkubali mwanamke kwa jambo moja kubwa ambalo ni uwezowake wa kujaaliwa kubeba mimba/ujauzito kwa muda wa miezi 9 iliyo hakika,japo yaweza kutokea ikawa zaidi au pungufu.kwa hilo nawapa heshima yenu kubwa.ila kikija kipengere cha kulea inategemea sioni kama ni jukumu la mama pekeyake,japokuwa mazoea yana tabu,iko hivyo na akina mama wameiweka hivyo kuwa wao ndo walezi wakuu wa watoto. na hao kwa aslimiakubwa ni mamazetu wazamani kwakiasi kikubwa wao walikuwa ndo kilakitu.kwa siku hizi mambo yamebadirika nayanaendelea kuwa hivyo.akina dada wa kazi ndo walezi wa watoto wetu sikuhizi,kina mama wasikuhizi nikidogo sana labda itokee yuko nyumbani na anamuda.sehemu nyingine hata akina sisi wababa hasa huku ulaya malezi ya watoto/mtoto hajalishi sana mama,na hii nikwa wale tu waswahili wenzangu wenye kujaribu kuvunja hizi tofauti yakuwa mtoto na mama.kaka s

Mija Shija Sayi said...

Sam sikubaliani na wewe kabisaaaaaaa!

Pamoja na kwamba mazingira yamebadilisha mambo lakini mama bado anavutwa zaidi na utu kwa watoto kulikokina baba. Na hii ni nature, kwa sababu wanawake wana aina ya cells (nimezisahau jina, lakini nitazitafuta) ambazo zinawafanya wawe watu wa kujali zaidi
Jiulize kwa nini wanaume ni wepesi ku-give up watoto kuliko mama katika familia zetu?..

Jiulize pia ni kwa nini waalimu wengi duniani ni wanawake?

Wanasayansi wanasema ni kwa sababu ya hizo genes ambazo wanaume hawana.. na inasemekana mwanaume akiwa nazo kuna uwezekano mkumbwa akawa homosexual..

ray njau said...

Hakika mama ni dhahabu isiyoisha thamani lakini baba anaendelea kubakia kuwa kichwa cha familia na ili familia isiyumbe ni vema kila mhusika aepuke kucheza rafu kwenye nafasi yake.

sam mbogo said...

Da mija ,waweza kutokubaliana namimi kwa asilimia mia hili silipingi kwa upande wako yawezekana unaiangalia hoja hii kimazowea. kaka s