Monday, July 2, 2012

TUANZE JUMATATU HII YA MWEZI HUU MPYA KWA UJUMBE HUU :- KILA KITU KINA MUDA WAKE....!!!



NAWATAKIENI WOTE MWANZO MWEMA SANA WA WIKI..

3 comments:

ray njau said...

Mhubiri 3:1-22

1 Kuna wakati uliowekwa wa kila kitu, hata kuna wakati wa kila jambo chini ya mbingu: 2 wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa; wakati wa kupanda na wakati wa kung’oa kilichopandwa; 3 wakati wa kuua na wakati wa kuponya; wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga; 4 wakati wa kulia na wakati wa kucheka; wakati wa kuomboleza na wakati wa kurukaruka; 5 wakati wa kutupa mawe na wakati wa kukusanya mawe; wakati wa kukumbatia na wakati wa kuepuka kukumbatia; 6 wakati wa kutafuta na wakati wa kuacha kutafuta kilichopotea; wakati wa kuweka na wakati wa kutupa; 7 wakati wa kupasua na wakati wa kushona, wakati wa kukaa kimya na wakati wa kusema; 8 wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia; wakati wa vita na wakati wa amani. 9 Mtendaji ana faida gani katika jambo analofanyia kazi ngumu?

10 Nimeona shughuli ambayo Mungu amewapa wana wa binadamu wajishughulishe nayo. 11 Amefanya kila kitu kiwe chenye kupendeza kwa wakati wake. Tena wakati usio na kipimo ameuweka ndani ya moyo wao, ili mwanadamu asiweze kugundua kazi ambazo Mungu wa kweli amefanya tangu mwanzo mpaka mwisho. 12 Nimekuja kujua kwamba hakuna jambo lingine bora kwao kuliko mtu kufurahi na kufanya mema maishani mwake; 13 na pia kwamba kila mtu ale, naam, anywe na kuona mema kwa ajili ya kazi yake yote iliyo ngumu. Hiyo ndiyo zawadi ya Mungu.

14 Nimekuja kujua kwamba kila jambo ambalo Mungu wa kweli hufanya, litadumu mpaka wakati usio na kipimo. Haliongezewi kitu wala kuondolewa kitu; lakini Mungu wa kweli amelifanya, ili watu waogope kwa sababu yake.

15 Jambo ambalo limekuwako, limekwisha kuwako, na litakalokuja, limekwisha kuwako; na Mungu wa kweli anatafuta kile kinachofuatiliwa.

16 Tena, nimeona chini ya jua mahali pa haki palipokuwa na uovu na mahali pa uadilifu ulipokuwa uovu. 17 Mimi mwenyewe nimesema moyoni mwangu: “Mungu wa kweli atahukumu mwadilifu na mwovu pia, kwa maana hapo kuna wakati wa kila jambo na kuhusu kila kazi.”

18 Mimi, naam mimi, nimesema moyoni mwangu kuhusu wana wa binadamu kwamba Mungu wa kweli atawachagua, ili wapate kuona kwamba wao wenyewe ni wanyama. 19 Kwa maana kuna mwisho ambao huwafikia wana wa binadamu na mwisho ambao huwafikia wanyama, nao hufikiwa na mwisho uleule. Anavyokufa mmoja, ndivyo anavyokufa yule mwingine; nao wote wana roho moja, hivi kwamba mwanadamu si bora kuliko mnyama, kwa kuwa yote ni ubatili. 20 Wote wanaenda mahali pamoja. Wote wametoka katika mavumbi, nao wote wanarudi mavumbini. 21 Ni nani anayejua roho ya wana wa binadamu, ikiwa inapanda juu; na roho ya mnyama, ikiwa inashuka chini duniani? 22 Nami nimeona kwamba hakuna jambo bora kuliko kwamba mwanadamu afurahie kazi zake, kwa maana hilo ndilo fungu lake; kwa kuwa ni nani atakayemleta aone mambo yatakayokuwako baada yake?

Mija Shija Sayi said...

Kabisa Yasinta, kila kitu kina muda wake...

Uwe na wakati mwema.

Salehe Msanda said...

Ni kweli kila kitu,wengine wanasema tukio na wengine wanasema jambo. Ujumbe unatakataka kuwa waangalifu wa masuala mbalimbali yanayotukabili na yanayotokea katika maisha yetu ya kila siku bila ya kusahau wajibu wetu wa kuwarithisha vizazi vyetu hasa ss watanzania masuala mazuri na yanayojenga umoja na uvumilivu na kuthamini utu.
Kila la kheri.