Wednesday, July 4, 2012

MAMA MZAZI NA MAMA WA KAMBO.!!!!

NIMEONA TU TUENDELEA NA HII PIA ...Hata mie huwa najiuliza kila siku hivi akina mama kwa nini wanawatesa watoto wasio wao? Uchungu si uleule jamani? Nimesikiliza sana wimbo huo hapo chini sijaelewa wanasema nini ila matendo nimeelewa. Mada  hii hapa chini nimeipata hapa.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------
Naamini HAKUNA mama anapenda kuwa MAMA WA KAMBO.Hakuna mwanamke anazaliwa kuwa MAMA WA KAMBO.Mama yeyote yule anaweza kuwa MAMA WA KAMBO baada ya kuwa na sifa ya kuwa MAMA.
Sifa moja wapo ya kuwa mama ni
..Uwezo wa kubeba, kuzaa kiumbe, kunyonyesha, kuhudumia, kukitibu kiumbe mtoto...
Mwanamke bila mtoto hawezi kuitwa MAMA.
Sasa basi......Mwanamke yeyote yule ambaye kajifungua mtoto anaweza kuwa MAMA wa KAMBO.
Baadhi ya Sifa za MAMA WA KAMBO.
KATILI.
JEURI.
MBINFASI.
Kabla Mama hajaitwa MAMA WA KAMBO hana hizo zifa za MAMA WA KAMBO lakini akishaukwaa UMAMA WA KAMBO basi ananyakua hizo sifa.
SWALI.
Hii siku ya mama duania inawahusu na MAMA WA KAMBO?

Labda twende mpaka huko Botswana na kumalia na wimbo huu STEPMOTHER/MAMA WA KAMBO...

TUACHE UKATILI AKIMA MAMA..MTOTO WA MWENZAKO NI WAKO NA WAKO WA MWENZAKO.....

9 comments:

emu-three said...

Mama wa kambo ni yule ambaye hakukuzaa,....anaweza akawa mwema au mbaya,ndivyo nionavyo mimi! Au?

Rachel siwa Isaac said...

Da'Yasinta si mama wa kambo wote wabaya, japo wengi wao wanatabia hiyo.
Pia wapo watoto wa kambo wajeuri na kukosa adabu, dhArau haswa akijua huyo si mama yake.

Pia kuna ndugu,jamaa, mama wadogo,shangazi pia wanaweza kumtendea mtoto ukatili pia.

Pia wazazi wakatili wanaotupa na kunyanyasa watoto wao nao jee tutawaitaje?

Mungu atusaidie kwakweli jee da'Kadoda au Msomaji ulishawahi kulelewa/kuishi nje ya wazazi wako ukiwa bado hujajitegemea?

Jee maisha yalikuwa tofauti sana?

ray njau said...

Mama wa Kambo naye ni mama!!
Mama ni dhahabu isiyoisha thamani!

sam mbogo said...

Bisikuti yangu za siku,yaani umepiga palepale,mimi maisha yangu yoote shele ya msingi,sekondari,chuo nimelelewa/kulia/tunzwa na kaka chini ya usimamizi wa shemeji.hivyo najuwa mzikiwake ulivyo.mama wa kambo kwa ujumla inategemea, siwote ni wabaya. ila nilicho gundua katika mama wakambo nimtazamo tu na hisia kuwa wana tesa.vitu vya kuangalia hapa ni uhusiano kati ya baba na mtoto,mama huyo wa kambo na mtoto,bila kusashau tabia ya huyo mtoto huko aliko toka kwa mama yake.pia ilikuwaje mama huyo kuwa mama wa kambo.wakati mwingine yawezakuwa nitatizo la baba akawa ndo sababu ya mtoto kuteswa. ila ningumu sana kumlea mtu asiye mtoto wako wa kuzaa,na pia ni ngumu sasa tena sana kukaa kwa mtu na mambo yakawa sawa kwako kwa asilimia mia mengine ni kusameheyana ,hata mama wakambo akikutesa mwisho ukishakuwa mkubwa msamehe endelea na maisha ndo mitihani ya maisha hiyo. kaka s

Yasinta Ngonyani said...

Mama wa kambo:- Sio lazima awe ameolewa na baba ndio awe mama wa kambo, Kama walivyosema waliotangulia maisha ni changamoto. Binafsi nimeishi sana tu na walezi ambao sio mama na baba yangu wazazi. Na ningependa kusema nawashukuru sana kwani walikuwa wakinifunza jinsi ya kuishi. Lakini kuna mateso mengine hakika nakuambia inauma kama huyo kijana kwenye hiyo video nimemuhurumia sana. Mnajua sipati kabisa picha ile kwanini kumchukia mtoto wa mwenzako kihivyo? je hivi akina baba wa kambo nao wanakuwa hivyo/wakatili?

Rachel siwa Isaac said...

Bisikuti yangu sisi wazima kabisa,umepotea sana, nategema kuwa pande hiyo nanyi mnanendelea vyema.

Pole sana kaka S. mimi sijawahi kulelewa nje ya Wazazi na hata Mzee alipofariki tulibaki nyumbani japo msaada mkubwa ulikuwa kutoka kwa dada na kaka na mwenyewe mama.

Nafikiri isingewezakana kunitenda au kuhisi na Nyanyaswa kwani bado nipo kwetu. ni ile kugombezwa kwa kawaida.

Likini nilikuwa nikiona au kusikia watu wanapo nyanyasika walipolelewa na pia wengine kujinyanyasa wenyewe kutoka na Tabia zao.

Naungana nawe kabisa hisia pia zinachangia na wengine wananyanyaswa,

Nikweli inabidi usamehe tuu.

Da'Yasinta ni kweli inabidi kushukuru kwa malezi.

pia Tabia zinatofautiana dada yangu Yasinta,baba wa Kambo wabaya na wema wapo pia.

chib said...

Ukatili ni tabia ya mtu, awe baba au mama.

Mija Shija Sayi said...

Yaani leo watu mmmeamka na mapoint humu sijawahiona.... kwa ufupi mmesema yote, sina la kuongeza.

cytotec said...

obat telat bulan i think your blog very informative obat penggugur thanks for sharing obat cytotec