Sunday, July 15, 2012

JUMAPILI/DOMINIKA NJEMA NA WIMBO HUU WA DADA EMMY KASIGEI ALAKARA!!


Katika waimbaji niwapendao dada Emmy yupo kwenye orodha hata kama sielewi anaimba nini lakini ni raha ilioje kumsikiliza. Pia nampenda dada huyu kwa jinsi alivyo na pia mavazi yake.
JUMAPILI NJEMA SANA KWA WOTE NA YEYOTE ATAKAYEPITA HAPA ABARIKIWE SANA. AMINA....

8 comments:

Ester Ulaya said...

Jumapili njema pia mdada

Ester Ulaya said...

Jumapili njema pia mdada

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante Ester...yaani leo nimekuwa mvivu ile mbaya hata kwenda kanisani sijaenda nipo nipo tu baada ya kubeba mabox wiki nzima mwili umekubali sheria..Pamoja na yote namshukuru MWENYEZI MUMGU kwa yote mema aliyonitendea.

ray njau said...

@Yasinta;
Asante sana kwa salamu za maisha na mafanikio kwa siku ya Jumapili.Pole sana na uchovu wa kubeba maboksi kwa wiki nzima.Siyo wewe pekee yako na hata sisi wenzio.Kwenda kwenye ibada ni jambo jema sana lakini huenda siku hizi likaonekana kuwa ni jambo lilipitwa na wakati na wengi sasa tumeendelea kuwekeza nguvu zote kwenye kubeba maboksi saan 24 kwa siku 7 lakini inapofikia suala la ibada vinaanza visingizio lukuki.
Huu ni wakati ufaao kwetu sote kutafakari maneno haya:
----------------------------------
2 Timotheo 3:1-5
-----------------------------------
1 Lakini ujue jambo hili, ya kwamba katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo. 2 Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda pesa, wenye kujidai, wenye majivuno, wakufuru, wasiotii wazazi, wasio na shukrani, wasio washikamanifu, 3 wasio na upendo wa asili, wasiotaka makubaliano yoyote, wachongezi, wasiojizuia, wakali, wasiopenda wema, 4 wasaliti, wenye vichwa vigumu, wenye kujivuna kwa kiburi, wanaopenda raha badala ya kumpenda Mungu 5 wakiwa na namna ya ujitoaji-kimungu lakini wakizikana nguvu zake; nawe geukia mbali kutoka kwa hao.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Asante kwa wimbo huu Da Yasinta kwani nazipenda sana nyimbo za Emmy Kosgei...

Bwana Ray Njau - asante kwa mahubiri mazuri. Ni vizuri tukiendelea kukumbushana kwani misukosuko ya hapa duniani ni mingi. Mungu Aendelee kutubariki wapendwa !!!

Rachel siwa Isaac said...

asante sana kwa Wimbo pia Natumai J'2 ilikwenda vizuri.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! ahsante kwa neno..Pia najua kwenda kanisani ni muhimu lakini pia kumwomba Mungu waweza kuomba sehemu yoyote ile pale unapozidiwa...
Kaka Matondo! Kumbe tupo wengi ambao tunampenda. Karibu sana.

Rachel/kachiki J2 yangu ilienda safi namshukuru Mungu. Ahsante kwa kuuliza.

Antonio Urdiales Camacho said...

Una canción con unas voces preciosas y un ritmo que atrapa.

UN saludo.