Monday, July 9, 2012

TUANZE WIKI/JUMATATU KWA KIFUNGUA KINYWA HIKI UBWABWA CHAI!!!

Huu ni ubwabwa , ambao ulikuwa mlo wangu wa asubuhi ya leo ukiambatana na chai. Chai ni tamu kwenye kikombe kikubwa wandugu ....nawatakieni Jumatatu njema sana...Oh Ubwabwa upo mwingi tu KARIBUNI:-)

7 comments:

ray njau said...

@Kadala;
Tusiposema asante tutakuwa tumekunyima haki yako ya msingi kama mama wa familia.Asante sana kwa kushirikiana nasi kwa huo mlo wa asubuhi ambao umetuthibitishia kuwa hujasahau mema ya kwetu kabisa.Uwepo ughaibuni kimuonekano tu lakini hisia zako zote zipo kwenye ardhi ya wazazi na walezi wako.Swali kubwa kabisa ni hili:NI NINI UNACHOENDELEA KUKIKOSA KABISA KUTOKA HAPA KWENYE ARDHI YA WAZAZI NA WALEZI WAKO KADALA?

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa kujumuika nami kaka Ray.Nikikosacho kutoka ardhi ya wazazi na walezi wangu ni WAZAZI NA WALEZI WANGU.

emuthree said...

Duh, mimi nahisi unakosa mengi, huko kuna kukatika kwa umeme, kuna vumbi kama huku?
Nakukumbusha tu,nahisi yapo mengi unayakosa,ila mwenzetu alitaka kujua kwani ameona unpata ubwabwa,ugali, na nini tena,kama huku, labda mimi nikuulize ni chakula gani unakikosa sana ambacho huko hukupiti?

ray njau said...

@Yasinta;
Na mengine mengi bila kutaja hesabu.
Afrika ni Afrika kwa ajili ya waafrika wenye asili ya kiafrika katika mazingira kiafrika yaliyohanikizwa na ladha maridhawa!

Yasinta Ngonyani said...

EMU3! ni kwamba sikosi kitu ila tu chakula cha nyumbani ni cha nyumbani. Na hayo mengine hata hapa yapo vumbi nk.

kaka Ray..Umenipiku kabisa ni kweli naikosa Afika. Ahsante kwa hili.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Naufagilia sana huo ubwabwa bana!

ray njau said...

@Yasinta;
Umeendelea kukosa mambo mema ya Ruhuwiko na utamaduni wa mswahili unaotia ndani ujirani mwema uliohanikizwa na upendo wa mama Kadoda umebakiza mboga ya majani ya matikiti nikamlizie kiporo changu cha ugali ugali?Huo ndiyo uafrika wetu nasi kwa hilo acha tuendelee kujivunia.Mulioyaona mema ya ughaibuni tunaendelea kuwatakia mema katika maisha yenye changamoto lukuki.