Yaani hapa nimetamani hicho kisamvu halafu nimeangalia nimeona pia kama kuna mlenda pori vile. Najigamba sikuchukua mbegu za mihogo. Eti hata ule wa kutafuna tu hakuna. Safari ijayo ntajitahidi..LOL.. Ukitaka kufaidi mambo mengine afanyayo mdada huyu basi gonga
hapa. Haya niwatakieni mwendelezo wa siku mwema...
7 comments:
@Wadau wa kibarazani;
Kisamvu kwa nazi na karanga utamu wake nani awezaye kuutungia shairi?
Hapa kwa upande wangu nitashindwa kuunga shairi..kwani ukitaka kunifukuza nyumbani kwako basi weka mboga zote karanga.
sehemu nzuri sana kwa kuchimba dawa.kisamvu cha karaka ni kitamu zaidi kuliko cha nazi.ila ziwe karanga za kukaanga,nahesabu siku tu nakuja nyumbani kula kisamvu na samaki bila kusahau majani ya maboga aka msusa. kaka s.
@Kadala;
Isiwe tabu wala shida na wala si tatizo kwako hapa kinachotakiwa kutunga sahairi la beti kumi linaloelezea utamu wa mboga ya kisamvu na kibaraza cha maisha kionyeshe mafanikio yake kwa kutangaza na kutoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu.Ni jukumu lako mama maisha kutangaza nia kwa wadau!!
Dada Yacinta nawe kwa uchokozi. Unaleta stori za kisamvu kwa watu tulioko mbali na nyumbani si hatari. Ajabu kuna kipindi nilikuwa nikiagiza vyakula toka nyumbani kuanzia dagaa hadi unga wa ulezi lakini watoto wangu hawakupenda vitu hivi. Wao mipizza na upuuzi mwingine. Ila kisamvu huwa hakina mjadala hasa kikiozeshwa kwa karanga.
nimekumbuka mbali jamani, kisamvu cha karanga za kukaanga kitamu zaidi.
Sam nimechekaaaeti pazuri kwakuchimba dawahahaha.
hilo siyo shamba langu, nilienda kufanya kazi eneo hilo, na hilo ni shamba la secondary iitwayo Mboga - Chalinze
Post a Comment