Friday, July 13, 2012

HOMA YA NGURUWE YAUA NGURUWE ZAIDI 110 IRINGA, SERIKALI YAPIGA STOP ULAJI KITIMOTO!!!!


Mbunge wa jimbo la Kilolo Iringa Prof.Peter Msolla akitazama nyama ya kitimoto iliyokuwa ikiuzwa mnadani eneo la Nyanzwa mapema mwaka jana

SERIKALI Iringa yapiga uchinjaji na uraji wa nyama ya nguruwe (kitimoto) baada ya kuibuka upya kwa ugonjwa wa homa ya Nguruwe uliopelekea nguruwe zaidi ya 100 katika Manispaa ya Iringa na Iringa vijijini kufa kwa ugonjwa huo.
Ugonjwa huo unatishia maisha ya Nguruwe 36,179 wenye thamani ya shilingi bilioni 5, 426,850,000 kwa upande wa wilaya ya Iringa vijijini pekee huku katika Manispaa ya Iringa nguruwe 2812 zenye thamani ya shilingi milioni 421,800,000 wapo hatarini kukumbwa na ugonjwa huo.
Kaimu afisa mifugo wa wilaya ya Iringa vijijini Said Kolwa aliueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com leo kuwa kutokana na kuwepo kwa ugonjwa huo katika wilaya hiyo ya Iringa tayari serikali imechukua hatua mbali mbali za kunusuru maambukizi zaidi ya ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuzuia uchinjaji wa nguruwe katika wilaya nzima ya Iringa.
Alisema kuwa Halmashauri ya Iringa ilipokea tarifa ya kuwepo kwa vifo vya nguruwe katika kata ya Lyamungungwe juni 28 mwaka huu ambapo ufuatiliaji ulifanyika kuanzia Juni 30 hadi Julai 2 na kubaini kuwepo kwa ugonjwa huo katika vijiji vya Kikombwe ,Igunda hivyo kuchukuliwa Sampuli ambazo baada ya kupimwa ilibainika ugonjwa huo.
Kwani alisema katika kijiji cha Kikombwe jumla ya mazizi 5 yenye nguruwe 14 yalikuwa yameambukizwa na kati ya nguruwe 7 walikufa na kijiji cha Igunda jumla ya mazizi 10 yenye nguruwe 14 yalikuwa yameambukizwa na kati yao nguruwe 28 walikufa kwa ugonjwa huo.
Kolwa alisema kuwa ugonjwa huo unadaiwa kuingizwa na mmoja kati ya wafanyabiashara wa nyama ya nguruwe ambaye aliingiza kwa siri nguruwe katika kijiji cha Igunda akitokea kata ya ukumbi wilaya ya Kilolo ambayo imekubwa na ugonjwa huo.
Hata hivyo alisema kuwa kutokana na ugonjwa huo tayari ofisi ya mganga mkuu wa wilaya hiyo Dr .Mathias Matandala imetoa tangazo la tarantini juu ya ugonjwa huo wa homa ya nguruwe (African Swine Ferver) ikiwa ni pamoja na kuzuia biashara zote za nguruwe na nyama ya nguruwe katika wilaya hiyo pia kuingiza wala kutoa nguruwe katika wilaya hiyo.
Wakati kwa upande wake afisa mifugo katika Manispaa ya Iringa Dr .Augustino Nyeza alisema kuwa katika Manispaa ya Iringa ugonjwa huo ulibainika Juni 24 katika kata ya Mkwawa ambapo wafugaji wa nguruwe katika eneo la Don Bosco na Makanyagio ndio nguruwe zao zilianza kukumbwa ugonjwa huo na kusababisha vifo vya nguruwe 80.
Hata hivyo alisema hatua zilizochukuliwa hadi sasa ni kufunga machinjio mawili yalipo katika Manispaa ya Iringa katika eneo la Ipogolo na mjini pia kufunga vibanda vyote vya kitimoto na maeneo yote ya uuzaji wa kitimoto mjini Iringa .
Alisema kuwa mizoga yote ya nguruwe waliokufa kwa ugonjwa huo ilifukiwa chini ya ulinzi makali na mabanda 118 ya nguruwe yalipulizwa dawa .
HABARI NA PICHA KUTOKA http://francisgodwin.blogspot.se.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Duh! bila kitimoto mbona kazi sana pole sana ndugu zangu/watani wangu..

ray njau said...

@Yasinta;
Kuadimika kwa kitimoto hazuii kasi ya gurudumu la maisha na mafanikio kwa kuwa kitimoto ni hamu tu lakini mboga ni dagaa na matembele.