Friday, July 6, 2012

MAENDELEO YA BUSTANI YA KAPULYA ILIVYO LEO....!!!

Haya ndiyo matokeo/maendeleo ya bustani ya kapulya  kutoka  siku hii na siku hii na hapa ni leo mambo ndiyo haya... karibuni wote ila msisahau UNGA WA MUHOGO/MAHINDI...KAPULYA....

 Figiri
 Mchicha
mboga maboga tena kutoka Njombe/Iringa

9 comments:

Anonymous said...

Hongera kwa hatua ya mboga kufikia hapo, tunajiandaa kuja kujumuika nawe muda sio mrefu sana. Ingawaje Unga wa mahindi na muhogo sina. Ama kweli mtu kwao.

emu-three said...

Mtu kwao, na muungwana haachi mila yake. Hongera sana kwa mbogamboga, nitakuja kudowea

Rehema said...

Mbona ukuninogesa sana makolo ago,nitayarisha uhembe wa mayau kabisa.

ray njau said...

@Yasinta;
Hakika mola hamtumpi mja wake na muomba Mungu kamwe hachoki na jembe halimtupi mtu bali watu hulitupa jembe na kulitelekeza.
Hongera na shukrani ni kwa titi ulilonyonya na mikono salama iliyokukuza!

Rachel siwa Isaac said...

Mkulima mmoja walaji wengi, tupo njiani kuja kuchuma mboga!!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina KARIBU sana hata kama huna unga twaweza kula na wali au mboga tu...

emu3! wala usikonde ni mboga nyingi sana ...
Rehema..Bwela tu mlongo

Kaka Ray! Ahsange kwa pongezi

Kachiki! Yaani kimbia uje usichelewa....usisahau unga.

Mija Shija Sayi said...

Hahahahaa Rachel waniacha hoi mie.. waso wakulima utawajua tu..

Yasinta mzahamzaha mwisho wake tunakula mboga duh!!

Next time, panda matembele ili uyakaushe ututumie na huku..

Bless ya!

Rachel siwa Isaac said...

Hahahahaa Mija mwana wa Sayi!!umeona eehh.natafuta sehemu ya kulima sasa.

Yasinta Ngonyani said...

Mija! Lakini haukuwa mzaha na sasa karibu maana huyo mchicha sasa unavyofumuka we acha tu...Usikonde nshapanga kupanda matembele..hivi mchachi, chainizi na figiri haiwezekana kukausha? maboga najua inawezekana.
Rachel/Kachiki! Tafuta hilo eneo na mie ntakuwa bibi shamba wako...LOL