Tuesday, July 10, 2012

Mtoto wa miaka miwili abakwa na mjomba wake achinika hadi kutoka damu .!!!

MTOTO wa miaka miwili na nusu, (jina linahifadhiwa), anayeishi katika Kijiji cha Buseresere kilichopo Wilaya ya Chato, mkoani Geita, anasadikiwa kubakwa na mjomba wake, Tatizo Lubalaza (20).

Taarifa za awali zinadai tukio hilo lilitokea Julai 5, mwaka huu, saa tatu usiku, baada ya mjomba huyo anayesadikiwa alikuwa amelewa kufika nyumbani hapo na kuingia ndani na kumkuta mtoto huyo akiwa sebuleni, huku mama yake mlezi, Pelesi Lubalaza, akiwa chumbani pamoja na wadogo zake na kisha akambeba na kuanza kumfanyia ukatili huo wa kinyama.

Baada ya kuanza kufanyiwa kitendo hicho, alianza kulia huku akilalamika anaumizwa, ndipo mjomba wake, Tatizo alipomwachia na kutoka nje, huku mtoto huyo akikimbilia chumbani kwa mama yake mlezi akilia.

Akisimulia tukio hilo huku akibubujikwa na machozi, Pelesi, alisema hakuamini kama kaka yake angeweza kufanya kitendo hicho cha kinyama kwa mtoto wao na mtoto huyo, ambaye aliingia chumbani huku akikamata sehemu zake za siri na kulitaja jina la mjomba wake, ndipo alipomkagua na kugundua damu zikitiririka miguuni mwake.

Alisema baada ya kugundua mtoto huyo kafanyiwa kitendo cha kinyama alichukua uamuzi wa kwenda Kituo Kidogo cha Polisi cha Buseresere kwa lengo la kutoa taarifa na kupewa barua ya matibabu ambapo alipelekwa katika Zahanati ya Buseresere kwa ajili ya matibabu kutokana na maumivu makali aliyoyapata.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Buseresere, Dk. Joram Nyanza, alithibitisha kumpokea Victoria na kudai alikuwa amechanika sehemu zake za siri na kumpatia matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paul, hakupatikana kuzungumzia tukio hilo.

chanzo: MTANZANIA


8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Jamani, jamani, hivi tunakwenda wapi..mtoto wa miaka miwili tena inawezekana bado ana nepi...Huyu mjomba atakuwa si mzima kwa kweli. inasikitisha,inaumiza na sijui hata niseme nini?

EDNA said...

Dunia inaelekea ndiko siko,hivi wanawake wote walijaa uende ukabake kitoto cha miaka miwili? phuuuh!

Yasinta Ngonyani said...

Edna yaaani huyu ana shida kubwa tu kichwani ..halafu mtoto wa dadake kweli jamani.....na wala asisingizie eti alilewa..kama ulivyosema Edna wanawake walivyo wengi..nashindwa kufikiria maumivu aliyopata mtoto huyu....pole sana mtoto pia familia

Mija Shija Sayi said...

Tumekwisha wazazi..

emu-three said...

Inatisha,...halafu utashangaa kesi kama hizo zinzmalizwa kindugu, watu wanaendelea kufuga nyoka, .....!

ray njau said...

Huu ni ujumbe wenye hisia zenye maumivu makali sana moyoni na hakika huu ni unyama mkubwa na usiojali kabisa utu wa binadamu.

Penina Simon said...

Jamani mbona watu wana ukatiri wa ajabu!!!!!!!

Mary Damian said...

watu wa namna hii hawafai kwenye jamii...Mungu amsaidie mtoto huyu isimhahiri kisaikolojia baadae. ni unyama wa kutisha