Showing posts with label urafiki. Show all posts
Showing posts with label urafiki. Show all posts

Sunday, July 29, 2012

POLE DADA MDOGO EDNA/FAMILIA YA ÖHDMAN KWA MSIBA/WAMEPOTEZA MTOTO WAO ...

 Blog ya Maisha na Mafanikio inapenda kuungana na Familia ya Öhman kwa pigo lililowapata mwanzoni wa wiki hii inayoisha leo. Mwanablog mwenzetu Edna alikuwa anasubiri mtoto. Bahati mbaya kiumbe kime kimewatoka. POLENI SANA, TUUNGANE NAYE KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU..NIMEONGEA NAYE ANAENDELEA VIZURI...http://ednaohman.blogspot.se/.

Wednesday, June 6, 2012

SALAMU NI NUSU YA KUONANA

Au tu kwa vile ni jumatano ya marudio basi ngoje turudie  na hii. nimeipata hapa
Tusalimiane japo kwa maneno machache wakati wowote bila kujali majukumu yetu ndani mikikimikiki ya maisha kwa kuwa kila mmoja anamhitaji mwenzake kwa nyakati tofauti ijapokuwa nyakati nyingine waweza kuhisi kuwa mtu fulani siyo muhimu sana kwako lakini wakati wa uhitaji ndiyo unatambua bila fulani mchakato wa maisha na mafanikio hauwezi kufikia tamati.
Kama wingi wa viungo mwilini kwa kutazama lakini wakati wa mahitaji kila kimoja kwa nafasi yake humtimizia binadamu haja yake.
"Salamu ni daraja la urafiki"
Wasalamu na shukrani;
 

JUMATANO NJEMA!!!

Saturday, February 18, 2012

FIKRA/WAZO LA JIONI YA JUMAMOSI HII!!!

1. Je?Kuna mtu yeyote amewahi kukuambia ni jinsi gani una umuhimu kwa wengine?
2. Unajua ya kwamba kuna mtu/watu wanatabasamu kwa upendo wako wa kweli?
3. Je kuna mtu yeyote amewahi kukueleza ni kiasi gani anakupenda? Basi, leo rafiki yangu nakuambia. Naamini ya kwamba bila kuwa na rafiki utakosa mengi. Uwe na jioni/siku njema , nina furaha ya kuwa sisi ni marafiki. URAFIKI UENDELEE NATUMAINI SIKU YAKO ITAKUWA/IMEKUWA NJEMA..NA ITAENDELEA KUWA NJEMA. KAPULYA.!!!

Tuesday, December 13, 2011

Hongera kaka John Mwaipopo kwa kuongeza mwaka"!!!

Katika pitapita zangu nimekuta kaka mwaipopo anatimiza miaka leo. Lakini sijui
ni miaka mingapi umetimiza?. Hongora kaka JOHN KWA SIKU HII MAALUMU. Na hapo naona unashereheke kwa ULANZI... tena linusu lizima wewe kaka weweee nakuamini.

Monday, November 14, 2011

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA MTANI WANGU FADHILI MTANGA!!

Leo ni ni siku huyu kijana alizaliwa na blogg ya Maisha na Mafanikio inapenda kumtakia HONGERA KWA SIKU HII. Kwani ni siku muhimu sana kwake na pia kwetu kwani tumekuwa kama ndugu sasa. Basi ngoja tuselebuka siku hii pamoja na kaka huyu kwa wimbo huu nina imani ni nyimbo azipendazo.....

HONGERA FADHY!!!

Thursday, October 6, 2011

FIKRA/WAZO LA JIONI HII!!!

1. Je?Kuna mtu yeyote amewahi kukuambia ni jinsi gani una umuhimu kwa wengine?
2. Unajua ya kwamba kuna mtu/watu wanatabasamu kwa upendo wako wa kweli?
3. Je kuna mtu yeyote amewahi kukueleza ni kiasi gani anakupenda? Basi, leo rafiki yangu nakuambia.

Naamini ya kwamba bila kuwa na rafiki utakosa mengi.
Uwe na jioni/siku njema , nina furaha ya kuwa sisi ni marafiki.
URAFIKI UENDELEE NATUMAINI SIKU YAKO ITAKUWA/IMEKUWA NJEMA..NA ITAENDELEA KUWA NJEMA.

Saturday, September 24, 2011

UJUMBE WA JUMAMOSI YA LEO!!!

Binadamu ni kama baisikeli, ikisimama inaanguka chini.
NAWATAKIENI WOTE JUMAMOSI NJEMA BINAFSI ITAISHIA KWENYE MAJUKUMU:-(

Wednesday, September 21, 2011

YASINTA NGONYANI NA JOHARI YA MATUMAINI

Kama kawaida kile kipengele chetu cha marudio ya Makala/mada, picha au kwa ujumla tuseme matukio mbalimbali KUTOKA BLOG HII YA MAISHA NA MAFANIKIO NA BLOG NYINGINE MBALIMBALI. Ni kipengele kitujiacho kila siku ya JUMATANO. Leo nimefanya upekuzi na nimekukutana na simulizi hii kwa vile inanihusu nimeona ni vema niiweka hapa kama kumbukumbu/mkusanyiko. Ukitaka kusoma maoni yaliyotolewa na wasomaji mara ya kwanza bonyeza Nyasa. karibuni sana.
Nafungua anuani pepe nakuta ujumbe, najiuliza kulikoni ni nani huyu? Alaah kumbe mwana wa nyasa, aliye ughaibuni? Ni mwanzo wa kumbukumbu, furaha na burudani. Mzaha wa hapa na pale kustawisha gumzo. Mtandaoni kwa saa nyingi mazungumzo yasokwisha hamu? Hatimaye ndiyo huyu tupo uso kwa uso tunazungumza tunapiga gumzo hapa na pale najiuliza maswali kadhaa kuhusu huyu mtu lakini najua ni mungu ajuaye mengi.
Mawazo yangu yaavaa uhodari wa kujua na kutaka kuona kile ninachoamini. Siku zinapiga miezi, mwaka na saa zote. Nipo ghorofa ya pili, nasoma ghafla ujumbe mfupi unaingia katika simu, salamu toka ughaibuni, najiuliza nitende vipi kwa mwandada huyu? nafunika vitabu na daftari, namtazama mwenzangu pembeni ananikodolea macho anashangaa vipi naacha kusoma halafu nachezea simu? Namweleza kuna jambo, nataka kuongea na mtu kwanza.Tayari tunajadili hili na lile najadili mambo kadhaa yenye maudhui ya nyasa, halafu tunakumbushana mambo ya Lundo na maisha kwa ujumla.
Inawezekana usinielewe msomaji wangu mpendwa, lakini mantiki yangu ni kukupa mwanzo wa YASINTA NGONYANI na MARKUS MPANGALA. Ni kama andiko la wakristo la yesu alivyowaambia msihangaike kwa lolote wala msibebe vyakula bali mwendako mtajaziwa. YASINTA ni kiumbe mwenye sifa ambazo kila siku naziwazia, najaribu kutafakari, nakumbuka stori zetu za hapa na pale, nakumbuka yale mambo ya WAOOOOOOOOOOO!!!!1 Hee kumbe hatuko peke yetu, tunatulia na kutafakari, tunaleta mzaha kidogo na kustawisha gumzo, mambo ya hapa na pale. Usisahau tupo umbali wa maili nyingi lakini ikawa dakika kuwepo ana kwa ana.
Mimi sinywi soda, situmii pafyumu, wala mafuta makali, siweki dawa nywele zangu daima ni rasta. Nauliza swali aaaahh ndiyo maana Erick naye anapenda sana Rasta siyo? Kicheko kidogo..., namtazama kwa shauku ya kujua mengi....LAKINI nagundua kama kile alichosema Koero kuwa YASINTA NGONYANI ni binti wa kitanzania. Sifa moja kubwa aliyonayo ni MAZOEZI na ukimtazama ni unaweza kubabaika ukasema umri wake ni 23 au 26 hivi kumbe huyooooo.
Hapa nyumbani nina bustani ya matunda na mambo mengi ya nyumbani wala siwezi kubabaikia hayo mambo ya wazungu. Mi hee unaweza kudhani mtu unayezungumza naye anatania lakini kukweli ni binti mwenye itikadi msimamo mkali. Nakumbuka nipo Mbeya, nikabandikwa maaswali lukuki, stori nyingi lakini kikubwa ni faraja za hapa na pale.Msomaji wangu, huyu Yasinta nina mengi ya kumwelezea lakini nafupisha na kutoa vipande ili upate msingi kamili. Hata hivyo nimemlazimisha kucheza muziki wa KWAITO anacheza usipime kabisaa, majuzi nikamwambia ebu selebuka na MYEKE BABA ya Mandoza... akacheka kidogo.
Nikumbushe msomaji YASINTA ni mkarimu, mtulivu, mkali, mwenye upendo, smikivu, mdadisi ndiyo maana nilimwita Mama Maswali magumu, mchokonozi. Nakumbuka kuna kitu alinichokonoa lakini nikajua udadisi ukaanza.... tusijali hayo lakini nakwambia kama huwezi kuishi na YASINTA basi wewe ni kiumbe wa ajabu. Mara nyingi utamsikia Markus mdogo wangu unatakiwa kujali muda wa kupumzika, utulivu na kujenga afya kwa kufanya mazoezi....Wakati mwingine inakuwa kama unaota kulala gizani na kulamba mchanga halafu huchafuki kumbe upo ukwelini na unawaza ukweli uleule wa siku zote.
Sikiliza mimi nataka kufanya kitu fulani katika blogu, nifanyeje? Ahh tunachapa gumzo tunafundishana haya na yale. Na fundsho letu kuu la mwisho lilikuwa pale ufkweni kuhusu NeoCounter. Ni mambo matamu ya teknolojia.SWALI UNAJUA ALIANZAJE KUBLOGU NA KUIJUA BLOGU YA KARIBUNI NYASA?Kuna kisa cha YASINTA katika blogu yangu hii ambayo naomba msomaji ukitafute. na mara nyingi amenihimiza kuandika tena kwani amevutiwa nacho.Kumbe kuna siku alikuwa akitafuta akina YASINTA wenzake wapo wangapi duniani, .... ndiyo hapo akutana na KARIBUNI NYASA na kisa kile cha Yasinta mwenzake. vilevile nilimpatia kazi ya kuchoma samaki kama unakumbuka msomaji kuna TANGAZO LA KAZI NYASA, yeye ndiye alishinda. Ila anapenda sana kula MAEMBE halafu na tabia yake ya KUNYWA CHAI ISIYO NA SUKARI yaani CHINGAMBU ni moja ya vionjo vyake na ambavyo nakiri ni MTANZANIA.Nikamwambia niseme au nisiseme kile kitu fulani....... aaaah Msomaji wangu utanichoka nadhani unaweza kudhani nafanya mzaha. Lakini kiini chake ujue tu ni binti ambaye naona tofauti yake na wengine ni mtazamo na misimamo yake isiyotetereka. Ni mdadisi sana huyu kiumbe, hachoki kujifunza kila mara lakini ndoto yake ilikuwa SISTA yaani wale watawa... utakumbuka ndoto yangu ilikuwa kuwa Padre lakini yamepita...SAHAU. Nakumbuka nikawa namlazimisha kumsoma kaka Ansbert Ngurumo....
Upendo wake na namna anavyoweza kujadili na watu ni kitu ambacho kinanifanya wakati mwingine nimwambie nina wivu sana, na hilo sifichi na nimesema daima ana anajua hilo. Mungu kamleta kwa kusudio la kupendwa na watu wala hana mengi. JE UNATAKA NIKUWEKEE PICHA TULIZOPIGA? aaaaaaahh msomaji nadhani hii stori ndogondogo ni habari kamili ingawaje imekaa mshazari. mtanisamehe kwa kutoweka picha tulizopiga.....Watoto wake anawaeleza kabisaaa..... nakumbuka anasema na Camilla.... mwanangu funga kanga , lazima kutii utamaduni wetu sawa? Camilla huyoooo anatoka ndani ya bwawa... anaiendea kanga.... mrembo huyu anachukua na kuifunga mwendo wake wa maringo taratibuuu kama twiga najongea mezani. Pembeni Erick sijui kiswidi chao wanasema Irik au? Kijana mpenda mazoezi kama mamake... anafuga rasta.... lakini siku hizi kazinyoa bwana...... a ha ha ha ha!
YASINTA GERVAS NGONYANI.... ngoja nikutaji jina leke jingine..... aaaah hapana siyo ruksa ni mimi tu nalijua au vipi usitake kujua sana. Ni kweli Yasinta mpenzi wa lugha ya nyumbani na bahati nzuri ni mtundu wa kujua lugha za wengine, najua ni wachache wanamudu hilo... lakini ameweza kujifunza lugha za wanyasa wale wanaongea kama wamalawi.... zile MULIBWANJI.... halafu tunahamia mazungumzo katika kimatengo... kingoni chenyewe, kimanda, kimpoto.... kinyakyusa..... nk. ukitaka kufanikiwa maishani ni lazima ujue utamaduni wako na kuheshima na utajua wapi unatoka.....YAKO MENGIIIIII SAANAAAAAAA............................... tutahabarishana siku nyingine.... manake kuna siri, mafanikio, shubiri na mwenendo mzima wa maisha yake.... harakati zake........ NITAKUMEGEA MAMBO MSOMAJI WANGU, na usisahau kumsoma pale kwa dada Koero( huyu naye subiri simulzi zake nimekuandalia ndugu msomaji na nitajibu maswali ya wanablogu fulani walioniuliza kuhusu YASINTA na hata huyu Koero) sawa? we tulia tuuuuuu Mwisho wa juma mwema!!! NA TUONANE TENA JUMATANO IJAYO!!!!

Monday, August 22, 2011

MWANABLOG YASINTA NGONYANI/KAPULYA ALIVYOKUTANA NA KAKA SAMWELI MBOGO/KAKA S!!!




Picha ya pamoja ,Yasinta/kapulya, kaka S na binti yake Yasinta dada Camilla hapa ni Rwaha (mbuyuni)



Mama Maisha na Mafanikio a.k.a Kapulya akiwa na kaka S

Kweli wahenga walisema milima haikutani bali wanadamu hukutana... Nimetoka zangu Ruhuwiko/Songea mida ya mchana mchana hivi . Giza likaingia na kituo cha kwanza kikawa Njombe..Asubuhi yake safari ikaendelea , kufika Iringa tukapumzika na kupata soda moja na bila kusahau kuchimba dawa. Mara Mnyasa nikaona Samaki nikashindwa kuvumilia nikanunua samaki wawili...Safari ikaendelea mpaka kufika Rwaaha na hapo ikawa ni muda wa kupata chochote/chakula cha mchana. Basi mnyasa huyu na binti yake wakakaa na kuanza kuwatafuna wale samaki huku wakitelemshia maji..wakati wengine waliamua kula sambusa.

Sasa ngoja nikuambia nilichotaka kusema ni kwamba wakati nakula samaki hao...mara akaja kijana/kaka mmoja. Akasimama mbele yangu nami nikawa nakereke, na nikajiuliza huyu kijana/kaka anataka nini? au anataka samaki wangu nini? kwanini anasogea sana nilipokaa na nilivyo mwoga nikaanza kuogopa. Lakini kaka huyu akawa ananisemesha utazani anaifahamu au kama vile tumeonana miaka mingiiiii iliyopita. Kila nikimtazama sipati kabisa picha yake. EEeeh, nikaona hapa kaaazi kwelikweli nikawa najiuliza ananifanananisha au?...Baadaye akajieleza kuwa yeye ni msomaji, mchangiaji na mtembeleaji mzuri sana wa Maisha na Mafanikio... Hata hivyo nikawa sipati kabisa picha yake...unajua kwa nini? yeye hana picha ndio maana sikumjua maana sikuwahi kuiona picha yake. Hakika hapo ndio niliposema kweli unaweza kujuana na mtu bila kuijua sura yake, kweli MILIMA HAIKUTANI BALI WANADAMU HUKUTANA. Na pia kusafiri kwa usafiri wako ni kuzuri unaona mengi na unakutana na usiokutana nao. Ahsante!!

Friday, December 10, 2010

KUMBUKUMBU+MAISHA

miti ya miembe
Najua hii habari/makala nilishawahi kuiweka lakini leo nimeamka na bado namfikiria/namkumbuka rafiki yangu Claire Mputa yaani kokote ulipo Claire jaribu kunitafuta nitafurahi kuwasiliana nawe tena.Haya ebu jikumbushe tena habari hii.
Nakumbuka ilikuwa mwaka 1983 nilikuwa naishi Lundo (Nyasa) wakati huo. Siku moja mchana nilikuwa naosha vyombo. Nilikuwa nasugua sufuria na vyungu hii ilikuwa kazi yangu. Kama mjuavyo Nyasa ni kula samaki sana. Kuna mtu alitupa miiba ya samaki ovyo na kwa mimi kutojua ni sehemu ile ile niliyokuwa nikiosha vyombo. Kwa bahati mbaya nilipiga magoti bila kujua napiga magoti kwenye miiba. Mmh kazi kwelikweli.

Baada ya siku goti lilianza kuvimba, nilichofanya tangu siku ile ya kwanza sikumwambia mtu nini kimenipata. Sababu kubwa ni kwamba ningeambiwa nibaki nyumbani. Sio kwenda shule ni mgonjwa. Na goti lilizidi kuvimba, lakini nilijikakamua na kuvumilia na maumivu yote. Kisa nilikuwa sitaki kubaki nyumbani bila kuhudhuria masomo.

Lakini siku moja wakati nipo shule nilikosa raha sana kwa maumivu. Rafiki yngu mmoja aitwae Claire Mputa aliona goti langu limevimba sana. Akanishauri niende hospitali naye atanisindikiza. Hata hivyo nilikataa kisa ni kile kile kuogopa kukosa masomo yatanipita. Lakini Claire aliweza kunishauri.

Ilichukua muda mrefu kufika hospitali kwani sasa goti lilikuwa limevimba mno na nilikuwa nachechemea na pia lilikuwa linauma sana, kwani kidonda kilianza kutunga usaa (infection). Kwa hiyo tulikuwa tunatembea polepole sana. Na hapo hatukuwa sisi tu kulikuwa na wanafunzi wengine pia waliokuwa wagonjwa wao walitangulia . Baada ya muda, yaani tulikuwa tunakaribia kufika hospitali tukawakuta wale wanafunzi wenzetu waliotangulia wamechepuka maporini ambako kulikuwa na miembe mingi iliyoshonana. Claire akaniambia; Yasinta twende tukaangalie wanafanya nini? Basi tukaenda kuangalia wote mie na Claire, tulipofika, tukawakuta wanafanya ule mchezo unaofanywa na wanandoa (ngono). Tulishangaa sana na kuondoka, kumbe wao walikuwa si wagonjwa walitaka tu kukwepa masomo na kwenda kufanya ule uchafu. Yaani ilikuwa kinyume kabisa na mimi, na sikutarajia kama wanafunzi kwa umri ule tuliokuwa nao wangeweza kufanya yale tuliowakuta wakiyafanya.

Haya, tulipofika hospital kama kawaida kukaa foleni. Mara ikaja zamu yangu Claire Mputa akanishika mkono na kunisindikiza ndani ya chumba ambacho kilikuwa maalum kwa mambo ya vidonda. Nakumbuka yule daktari alikuwa mzee kidogo, aliitwa Kataulaki. Alinitisha alipochukua mkisu mkubwa nilifikiri anataka kuukata mguu wangu. Lakini hakufanya hivyo alinitibu na mimi na Claire Mputa tukarudi tena shuleni.

Kikubwa ninachotaka kusema hapa ni kwamba kama Claire asingenishauri kwenda hospitali basi leo hii nisingekuwa na mguu wa kushoto. Na pia nisingeyaona yale nilioyaona kule miembeni, kwani yalinifunza kwa kiasi fulani. Napenda kuchukuwa nafasi hii kuwashukuru rafiki yangu Claire Mputa na pia yule Daktari Kataulaki
Napenda kuwaambia ahsanteni sana. IJUMAA NJEMA TUTAONANA TENA WAKATI MWINGINE!!!!!

Wednesday, October 13, 2010

HONGERA SHANGAZI YANGU PAULINA ARIANNA BANDIO KWA KUTIMIZA MWAKA MMOJA

mtoto Paulina mwaka mmoja leo
Binafsi nitakuita Shangazi/rafiki yangu. Lakini kuna wengine watakuita
binti, mtoto, binamu, mpwa n.k.
Shangazi/rafiki yangu Paulina leo ni siku kubwa sana kwako. Ni mwaka sasa
umepita tangu uyaanze maisha yako. Yaani leo unatimiza mwaka 1(mmoja) kwa
kweli miaka inakimbia sana, ni juzi tu ulikuwa kachanga leo hii umekuwa
binti wa kuweza kukutuma utuchotee maji ya kucnywa na karibuni tu utatupikia
na hata ugali.
Blog ya Maisha na Mafanikio inapenda kutoa pongezi nyingi sana kwa wazazi wa binti Paulina ambao ni Mubelwa na Esther Bandio kwa malezi
mazuri wampayo mtoto Paulina. Mwenyezi Mungu awazidishia nguvu ili muzidi
kumlea mtoto huyu na awe kama ninyi wenyewe.
Unaweza kuwatembela Mubelwa.

Tuesday, October 12, 2010

Hongera kwa siku ya kuzaliwa kwenu Dada Subi na Kaka Chib!!

Kaka Chib
Dada Subi
Blog ya Maisha na Mafanikio inapenda kuwatakieni siku hii ya kumbukumbu yenu ya kuzaliwa kwenu. Na pia muwe na Baraka tele na maisha mema na pia mafanikio mema. HONGERENI SANA.!!!!!


Friday, October 8, 2010

Labda KUNA ambao HAWANA furaha mpaka wapate MTU MWINGINE au KITU KINGINE kisicho chao cha kukichukia au tu kukiona ni USHUZI!

Mt. Simon Mkodo Heriel Kitururu anasema...

Ukichunguza ,....
.... unaweza kupata MAFILINGI kuwa kuna wengi YAO huleta maana tu kama kwao YAWENGINE ni ushuzi.:-(

Ze mfano:

Labda MWENYE tabia nzuri furaha yake katika UPATAJI WAKE maana katika furaha zake ni kwa kuwa wengine anafikiri wana TABIA mbaya kwa hiyo yeye katika jamii anathamani zaidi .:-(

Labda Mkristo katika kufurahia UKRISTO wake- kunaleta maana tu pale astukiapo kuna WAISLAMU na WENGINE wenye dini za KIGAGAGIGIKOKO ambao afikiriao hawataenda mbinguni kwa kuwa si WAKRISTO kitu kimleteacho faraja katika UKRISTO wake ambao anaamini ni YESU tu ndio njia ya kwenda kwenye utamu.:-(

Kwenye Ukristo wa KISABATO labda faraja ni kustukia kuna WAKATOLIKI , Walutheri na hata wale WALOKOLE wa KIKAKOBE ambao kwa kisabato kuna kitu wanakosea katika mwendo wa maringo wa kulenga mbinguni kitu kifanyacho USABATO mtamu.:-(

Wenye akili kwa kuwa wanapasi MITIANI labda furaha ni kwakuwa kuna wajinga waliofeli naa ambao hata kushusha hoja kisomi hawawezi.:-(

Kwa KIMWANA mzuri SURA KAMA CHUNUSI -labda faraja huletwa na uwepo wa VIMWANA wenye sura kama JIPU kitu kisababishacho Kimwana mwenye sura kama chunusi kujisikia ahueni kwa kuwa anasifiwa zaidi ya mwenye sura kama jipu na katika kuchuna buzi akaunti yake hujaa kirahisi zaidi.:-(

Wayahudi labda huhitaji walimwengu wengine ili wajisikie kuwa wao ndio Taifa lililochaguliwa na Mungu kwa hiyo wao spesho.:-(

Ndio ,....
.... labda hakuna mwenye FURAHA kamili kivyake kama hakuna WENGINE na vya wengine vya kunyoshea vidole,.....

.... ili kuhalalisha kuwa vyangu vinaunafuu kitu ambacho husaidia baadhi ya watu ndani ya kibano KUSAIDIA ombaomba mtaani ikiwa ni MOJA YA NJIA ya kujisaidia kupata Uahueni kuwa angalau pamoja na kuwa MAISHA ni magumu lakini angalau mimi bado sijafikia kuwa ombaomba mtaani ingawa ni malaya kidooooogo.:-(

Swali:

SI kuna waonao mgonjwa nakupata unafuu kuwa angalau WAO ni wazima kama tu vile WEWE ukiona MZEE aliyefikia kujinyea ujisikiavyo vizuri kuwa angalau wewe bado kijana na BADO wewe unaweza kwenda mwenyewe chooni kushusha kilo kadhaa za kilichowahi kuwa chakula kwa MAMA N'TILIE?
SI kuna MKE WA MTU akiona MME wa mwenziye ni MZURI zaidi hupunguzwa faraja ya kuvumilia angalau vijambo a.k.a MASHUZI ya MME WAKE YA KILEVI aliyelala naye kitanda kimoja baada ya huyo MME kutoka BAA na kudai kwa nguvu chakula cha usiku cha ushindi wa haraka haraka kimagoli?
Ndio,....
....labda faraja zako hutegemea sana ufikiriavyo mapungufu ya wengine hata wasiokuhusu.:-(
Habari hii imeandikwa na Mzee wa mawazo Mt. Simon Kitururu . Nimeona si mbaya kama nikiibandika hapa kibaraza cha Maidha na Mafanikio.

Tuesday, September 28, 2010

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KAKA YANGU SHABAN KALUSE


Kaka Shaban Kaluse
Napenda kukutakia HONGERA kwa siku yako ya kuzaliwa, na nakutakia kila la kheri kwa kila jambo utakalotenda liwe jema na pia nakutakia maisha mema, upendo na amani itawale katika familia yako. Na halafu uwe na mafanikio kwa kila utakalo tenda. Halafu najiuliza hivi siku hizi sijui upo wapi wewe kaka wa utambuzi ? HAYA HONGERA SANA KWA SIKU HII MUHIMU KATIKA MAISHA YAKO. HONGERA KAKA SHABAN!!!!!. Kwa kutaka kujua mambo ya mwanautambuzi huyo gonga hapa.

Friday, September 24, 2010

IJUMAA NJEMA NA WIMBO HUU WA MATATIZO NA DADA NAKAAYA SUMARI

WIMBO HUU NIKIWA NAUSIKILIZA KILA MARA NA UNANIFANYA MAFIKIRISHO SANA-:) SIJUI WENZANGU NANYI ITAKUWA KAMA MIMI!! IJUMAA NJEMA NDUGU ZANGU !!!!!

Thursday, September 23, 2010

SHUKRANI KWA WOTE!!!


Kwa ajili yenu wote kutoka kwa Yasinta Ngonyani!!!

Wanablog wenzani leo napenda kutoa shukrani zangu nyingi sana na za dhat kwa UWEPO wenu na pia UPENDO wenu kwangu, kwa familia yangu na kwa blog ya MAISHA NA MAFANIKIO.

Kwanza kabisa napenda kuwashukuruni kwa UWAZI wenu kwangu, hapa nina maanisha kwa kuniambia yale niliyokuwa nayajua kuhusu mimi na yale ambayo sikuyajua kuhusu mimi. Ni jambo la kujivunia sana pia kufurahisha kuona unaambiwa mambo kama haya kabla hujaiacha dunia hii. Kama tunavyojua wengi wameiacha dunia hii bila kuja wametenda nini hapa duniani na wao ni akina nani? Na siku ile ya safari ya mwisho ndo watu wanapotamka yale yote mazuri na mabaya. Na mimi naweza kusema nina bahati kwani nimebahatika kuyajua na pia wengine kunijua. AHSANTENI SANA.

Kwa kujikumbusha unaweza kusoma hapa kwa mdogo wangu wa hiari Koero Mkundi na hapa kwa Mzee wa lundunyasa Markus Mpangala, pia hapa kwa Diwani ya Fadhili kwa mtani wangu Fadhy Mtanga na halafu hapa.

Pia kwa wengine wengi walioniandika na ambao sijawataja hapa, nawashukuruni sana wote wote kwa ujumla kwa UPENDO wenu.

Tuesday, September 14, 2010

Hii nimeipenda sana!!!


Nadhani wote mnajua huyu ni nani na ukiangalia kwa makini utaona anafanya nini na anaangalia nini au labda anasoma . Sijui ilikuaje hapa?

Tuesday, September 7, 2010

HONGERA BLOG YA LUNDUNYASA KWA KUTIMIZA MIAKA MINNE!!!

Markus Mpangala wa lundunyasa


Miaka yaenda kasi mno tarehe 31/8/2007 blog hii ya LUNDUNYASA ilitimiza miaka 4. Blog ya MAISHA NA MAFANIKIO yakutakia yote utakayotenda yawe na mafanikio mema. Hongera sana na uwepo wako unathaminiwa sana. Ingia hapa utakuta mengi

Friday, September 3, 2010

Huyu ni mrembo wa wiki hii, Je? unamfahamu huyu??

Napenda kuwatakieni wote Ijumaa njema. Picha hii nimeipenda na nimeona iwe ni picha ya wiki hii. Jipende kwanza mwenyewe na wengine watakupenda!!! Juma ndio linaisha sasa, kwa wengi ni wakati wa kumpumzika, na wengine kazi kama kawaida. Basi nasema tena nawatakieni wote muwe na wakati mzuri. IJUMAA NJEMA!!

Wednesday, August 25, 2010

HATIMAYE MIAKA MIWILI IMETIMIA TANGU BLOG YA CHANGAMOTO YETU IANZISHWE. HONGERA!!!


miaka yaenda kasi mno yaani leo ni miaka miwili blog hii ya CHANGAMOTO YETU tangu ianze kublogu. Blog ya MAISHA NA MAFANIKIO yakutakia yote utakayotenda yawe na mafanikio mema. Hongera sana na uwepo wako unathaminiwa sana. zaidi ingia hapa utapata mengi zaidi.