Thursday, October 6, 2011

FIKRA/WAZO LA JIONI HII!!!

1. Je?Kuna mtu yeyote amewahi kukuambia ni jinsi gani una umuhimu kwa wengine?
2. Unajua ya kwamba kuna mtu/watu wanatabasamu kwa upendo wako wa kweli?
3. Je kuna mtu yeyote amewahi kukueleza ni kiasi gani anakupenda? Basi, leo rafiki yangu nakuambia.

Naamini ya kwamba bila kuwa na rafiki utakosa mengi.
Uwe na jioni/siku njema , nina furaha ya kuwa sisi ni marafiki.
URAFIKI UENDELEE NATUMAINI SIKU YAKO ITAKUWA/IMEKUWA NJEMA..NA ITAENDELEA KUWA NJEMA.

7 comments:

Nampangala said...

Asante sana Mlongo, ni kweli kabisa kuwa utakosa mengi kama huna rafiki. Nafurahi kuku fahamu, Ubarikiwe

Mija Shija Sayi said...

Aaaaaaa!!..Asante sana Mwanafalsafa wangu.. Sikujua kama Yasinta ni mwanafalsafa hivi..

Kweli Mr Klaesson kapata...lol!

sam mbogo said...

Asante/asanti sana. kwa wazo la leo/jioni. ila nina wasiwasi kidogo,kwa sisi binaadamu wa leo juu ya neno NAKUPENDA, kama huwa halichukui muda upendo huo kupotea/kubadilika.maranyingi uvumilivu katika kupenda huka ni wa mashaka. sijuwi nyie wengine mnasemaje, kaka S.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Aksante Da Yasinta!

ray njau said...

Tunapodadavua mada ya upendo ni muhimu kuweka angalizo.Kwa kuwa aina ya agape ni upendo wa Mungu kwa viumbe wake.Upendo wa kupenda kisichopendeka.Upendo usiojali maslahi binafsi.Lakini wanadamu wanonyeshana upendo kulingana na mahusiano husika.

Yasinta Ngonyani said...

Nampangala mlongo! hata mimi nafurahi sana kukufahamu!

MIja! Ahsante na wewe kwa kuliona hili najaribu jaribu..Mtamsalimia Mr. K....LOL

Kaka Sam! Ahsanti na wewe, ni kweli hili neno KUPENDA linaweza kuleta matata kama utalifanya lilete matata. lakini ukifikiri ya kwamba:- Binadamu wote hupendana kwa vile wote tumeumbwa kwa mfano na sura yake basi kutakuwa hakuna mashaka. Na pia kuna kupenda yaani ule UPENDO WA KIMAPENZI. Natumaini umenielewa.

Kaka Chacha! ahsante nawe:-)

Kaka Raynjau! nakubaliana nawe. Ahsante sana.

Anonymous said...

obat telat bulan i think your blog very informative cytotec thanks for sharing obat cytotec