Monday, October 17, 2011

LEO KAPULYA AMEPATIKANA /MWILI UNAPOSHINDWA KUVUMILIA!!!

Nimeamka asubihi nikawa najisikia uchovu uchovu nikadharau na kudhani ni uchovu tu wa kawaida. Lakini nikaona nazidi kuchoka na mwili wote unauma na joto kali ....Kama kungekuwa na mbu basi ningesema malaria lakini sasa....NAUMWA:-(

21 comments:

Baraka Chibiriti said...

Pole sana Dada....pengine ni hali ya hewa, au homa za hapa na pale kama kawaida ya sisi binadamu. Uguapole.

sam mbogo said...

Pole sana,itakuwa ni haliya hewa tu.ila yasinta sasa na kubaliana na kitururu,kipengere cha JICHO mweeee tena basi tu.ugua pole.kaka s

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Pole sana da Yacinta Mungu atakuafu upate nafuu tuendeleze libeneke. Get well soon

ray njau said...

UGUA SALAMA DADA YASINTA.
----------------------------
Zaburi 41:1-3

Kwa kiongozi. Muziki wa Daudi.

1 Mwenye furaha ni mtu yeyote anayetenda kwa kumfikiria mtu wa hali ya chini;

Katika siku ya msiba Yehova atamwokoa.

2 Yehova mwenyewe atamlinda na kumhifadhi hai.

Atatangazwa kuwa mwenye furaha duniani;

Nawe huwezi kamwe kumtia mkononi mwa nafsi ya adui zake.

3 Yehova mwenyewe atamtegemeza katika kitanda cha ugonjwa;

Kitanda chake chote hakika utakibadilisha wakati wa ugonjwa wake.

ray njau said...

MALARIA HAIKUBALIKI LAKINI.......
-----------------------------
Hii ni malaria kali na dozi yake kamili ni mpaka upate ushauri wa daktari mahiri na makini katika tasnia ya afya na utabibu.Wanamuziki wanaimba na wanazuoni wanasomesha lakini malaria bado inatutesa kila mawio hadi machweo.Watafiti wanazidi kuota vipara huku wadau wanalia na malaria na yenyewe ni kiziwi.Ushauri wa kila aina umetolewa na ubunifu unaendelea lakini kuangamiza mazalia ya mbu katika makazi ya binadamu yabakia kuwa njia makini na maridharawa ya kutokomeza malaria.Mimi nimesema na wadau nao waseme kwanini malaria haikubaliki lakini bado inatutesa?

EDNA said...

Pole sana mdada.KRY PÅ DIG.

Anonymous said...

pole da Yasinta niko nchi za baridi kabaridi kameanza kwa mbali naamini unakumbuka kunywa mafuta ya samaki, stay, sometimes miili yetu inalack too much some vitamins inaanza kunyong'onyea...stay blessed

Mija Shija Sayi said...

Pole sana Yasinta, Mungu akupe nguvu utapona tu..

Ugua pole.

Raymond Mkandawile said...

Pole sana dada Yasinta,nakuombea Mungu akujalie upone haraka...

Goodman Manyanya Phiri said...

Umeusikilliza mwili wako na kwenda kitandani; ni jambo jema sana! (Kesho au keshokutwa ya kitanda mfururizo hivyo utarudia hali yako kama kawaida bila hata labda kumuona daktari).

Ugua pole!

Rik Kilasi said...

GET WELL SOON DA YASINTA, POLE SANA PENGINE MABADIRIKO YA HALI YA HEWA AU MALARIA FANYA UPIME.

ISSACK CHE JIAH said...

hoo mtani wangu wiki mzima sijasoma mtandao wako leo hii nimefungua tu nimekuona umelala nimestuka pole na homa nadhani leo hii j4 utakuwa mzima sina cha kukupa kama ungekuwa nyasa supu ya mbelele tu ingemaliza kabisa homa hii usijali utakuwa fresh mtani wangu mwambie mkandawile akutumie likungu ,unajuwa ni dawa sana ya homa hujaipata siku nyingi
che jiah

fita lutonja said...

pole dada yangu yasinta ila nakuomba tuwasiliane kwa sms nimebadilisha e mail natumia jikomboe1@gmail.com

fita lutonja said...

pole dada yangu yasinta ila nakuomba tuwasiliane kwa sms nimebadilisha e mail natumia jikomboe1@gmail.com

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii kwa kuwashukuruni wote kwa maombi yenu..Najisikia nafuu jioni hii...AHSANTENI SANA:-)

Jacob Malihoja said...

Oooo! Pole na homa! na pia nafurahi kujua kuwa umeendelea vizuri .. ni matumaini yangu hadi leo upo pouwa kabisa!

Yasinta Ngonyani said...

Mlongo Jakob! hali yangu leo si mbaya sana na si nzuri sana ila niko katika mwelekeo wa kupata nafuu..Ahsante kwa pole.

Simon Kitururu said...

Pole sana Yasinta ingawa nimechelewa!

Yasinta Ngonyani said...

Simon! kumpa pole mtu au hongera sijui kama kuna kuchelewa...Ahsante ndugu yangu...

Mbele said...

Pole sana. Mungu akusaidie haraka na vizuri.

Yasinta Ngonyani said...

Prof. Mbele ! Ahsante leo naona nafuu hadi nimeweza kutoka nje ila nilibanwa kweli naona maombi yenu Mungu ameyasikia.