Monday, October 17, 2011

MICHEZO/HIVI NDIVYO WIKIENDI YANGU ILIVYOKUWA!!

Kuwa na watoto ni raha sana, ila kua wakati unaweza kusema kaaazi kwelikweli. Maana hakuna kupumzika. Kama uonavyo hapa hivi ndivyo wikiendi yetu ilivyokuwa da´Camilla alikuwa katika mechi, hapa yeye ni huyo karibu na kipa huyo mwenye jezi nyeupe na nywele nyeusi ...bahati mbaya timu yake ilishindwa ila kwa kweli walijitahidi na mchezo ulikuwa mzuri sana. Ni handboll/mpira wa mikono.

6 comments:

Simon Kitururu said...

Poa sana yuko active hivyo maana watoto wengi siku hizi michezo inamaana ni kukaa mbele ya kompyuta au TV!

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli Simon usemayo. Nashukuru wanetu wao wanafanya sana mazoesi maana wote wanapenda michezo

sam mbogo said...

Ukiwa nchi dunia ya kwanza,tegemea hayo unayo yaona,ndiyo maana wenzetu vipaji huanza tangu udogo kuvikuza.na unakuta wanafanikiwa bado wadogo sana.yote haya nikutokana na kuwa navitendea kazi vya kuaminika.sikunyingine huwa najiangalia vipaji nilivyo navyo nakusema ningekuwa nimezaliwa huku mbona ningekuwa mbali sana au ninge kata shauri la kuja huku ningali kijana .halafu wakati mwingine najiambia nimapenzi ya mungu kunifikisha hapa nilipo,ya wezekana nifunzo tosha kuto kuzaliwa huku.muhimu sasa ni hawa watotowetu kuwawezesha.kaka s

Yasinta Ngonyani said...

Kaka S. hakika umesema kitu. Lakini pia kama ulivyosema ni lazima tumshukuru Mungu kuwa tupo kama tulivyo au tumezaliwa nchi tulizozaliwa...Kaka S unataka kusema wewe ni mzee? Nilivyokuona niliona bado kakijana au nisema kijana bado.

sam mbogo said...

Dada yangu ukisha fikisha miaka 40......? kauze kana kimbilia.sema tu mazoezi yamenisaidia sana kuonekana naweza kuongeza mke mwingine!!? kazi yangu au ajira ya ngu nakutana na watoto navijana kwa wingi,nafundisha dance,drama mashuleni(workshop) pia ni Therapist.nafundisha dance therapy katika special need school.napiga ngoma kiasi(matamasha). pia najitahidi kuimba,hufundisha nyimbo za asili kwenye matamasha.mwishokabisa ni mwigizaji . hivi ndiyo vinani fanya nionekane kijana .nafikiri umenipata .kaka s

Mija Shija Sayi said...

Sipati picha alivyonuna baada ya mechi...